Waziri Angela Kairuki akabidhi vifaa vya michezo jimbo la Same

Huyu Mama ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Umoja wa Vyama vya Wafanyakazi(Yaani anawakilisha wanawake wafanyakazi Bungeni)Lkn ndio huyohuyo kapewa Wizara ya Wafanyakazi anaooaswa kuwatetea huko Bungeni.Maajabu haya!!!

Huyu kwao ni Chome-Same kule Upareni juu milimani.Unapitia hii njia ya Mkomazi National Park hadi huko mbele.Mama kaanza kujiandaa kwa ajili ya Jimbo la Same Magharibu 2020 ili kumuondoa Mathayo David Mathayo ambaye ushindi wake 2015 dhidi ya MBANJO wa CHADEMA ulikuwa ni wa "FFU".

Mama kaanzisha Mashindano ya Mpira ya Wilaya Nzima ya Same...Yanaweza kuchukua hata mwaka mzima kwa jinsi team zilizvyo nyingi.Shughuli zote zilifanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki pale jimbo la Same.Na ndio huyu Mama hufika hapo mara nyingi...Na alitoa mchango kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mapadre pale Jimboni Same.

Mathayo akae macho;lkn nitashangaa sana hawa watu wa Same....Toka Uhuru wao maji ya bomba ni anasa,dumu la maji linauzwa 500 hadi 1000 wakati wa ukame,na tena maji ya chumvi halafu bado wameikazania tu hiyo "Iyena iyena".
Nashkuru saana kwa ufafanuzi wako usio acha swali mkuu..mm nkajua kuwa ni mbunge wa jimbo
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Mh Angellah j.Kairuki ameanzisha mashindano yatayojulikana kama Angellah Kairuki Cup yanayotegemewa kuanzia tarehe 7.1.2017 katika wilaya ya Same, akibidhi vifaa hivyo jezi na mipira kadhaa waziri kairuki amesema wanamichezo wadumishe nidhamu katika kuendeleza michezo nchini

Chanzo: ITV Sauda Shimbo Kilimanjaro
Kazi kweli kweli.....Usikute ndio kipaumbele cha wapiga kura ktk jimbo hilo. Sorry I mean kipaumbele cha Waziri
 
mathayo apeleke malalamiko ya kutishiwa kuporwa jimbo chamani kama alivyolalamika mama Anne Kilango baada ya aliyekuwa DC wa Mbozi dk Michael Kadeghe kwenda Same huku gari ikipeperusha bendera ya DC.
 
Bora bwana kumbe ndugu yetu, wazo zuri la kujitambulisha ss keep up tuko pamoja. Sasa kwa kuwa umejitambulisha look over your shoulder.
 
..kumbe ni wa kaskazini.

..basi amekalia kuti kavu.

..atatumbuliwa hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom