Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,505
- 9,286
Wazee, Watoto na wagonjwa wa Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita na mikoa jirani wameshauriwa kuaga mwili wa hayati Rais John Magufuli kwa kufuatilia kwenye vyombo mbalimbali vya habari vinavyorusha mubashara badala ya kwenda uwanjani.
Uamuzi huo unatokana na eneo la uwanja wa Magufuli ulipo wilayani humo uliotengwa kwa ajili ya shughuli za kuaga kuwa mdogo na hautaweza kuhudumia wananchi wote.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Machi 23, 2021 mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema eneo la uwanja litatumiwa na familia, viongozi wa Serikali, dini na wawakilishi wa wananchi.
Amewataka wananchi wa Mkoa wa Geita hususan wa wilaya ya Geita kujitokeza barabarani Machi 24, 2021 ili waweze kutoa heshima za mwisho, akiwataka kufanya hivyo tena Machi 25.
“Chato hapatoshi ni padogo mno niwaombe wenye changamoto, wazee, watoto na wagonjwa naomba wakae nyumbani yapo maeneo yenye luninga mnaweza kuaga kwa kuangalia mubashara na eneo la maziko litahudhuriwa na watu wachache sana ambao ni familia na viongozi wakuu.
Niwaombe sana Machi 26 ni kwa ajili ya watu wachache mno naomba mkae nyumbani mtazame luninga,” amesema Gabriel.
Chanzo: Mwananchi