Wazee waichagua CHADEMA Arumeru Mashariki

Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
803
472
Vijana waliokuwa na umri wa miaka chini ya 18 (<18) mwaka 2010 hawakujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa kuwa umri wao ulikuwa chini ya miaka 18 kikatiba na taratibu. Vija hao ambao SASA ni wa miaka 18, 19,20 na hata 21 hawakupiga kura siku ya uchaguzi jana kwa kuwa hawakuwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, kwa kifupi damu changa na inayochemka jana haikupata haki ya kikatiba kuchagua muwakilishi wao bungeni.

Wachenguzi wa maswala ya kisiasa wanadai kazi ya vijana hawa ilikuwa ni kutoa somo la uraia kwa wazazi wao na wazee wao na katika uchaguzi wa jana, wazee na kinamama walikuwa wengi kwenye vituo vya kupigia kura kuliko vijana.

Hii ni dhahiri kuwa wazee sasa wanaweza kubadilika na kuchagua kwa hoja na sera na si kwa mazoea kama hapo nyuma, hii ni hatua kubwa katika democrasia ya nchi yetu.

Kumbe hata wazee wakiwezeshwa na vijana wao, wanaweza, sasa wazee waichagua CDM Arumeru Mashariki je tutarajie nini kwenye chaguzi nyingine au hii ya Arumeru ilikuwa exceptional .?
 

Mbona kana aliyeandika hii certificate alikuwa na wasiwasi na woga mkubwa, ona hiyo hand writting inaonyesha wasiwasi na kutokujiamini, au alikuwa anatumia kalamu ya Lema, maana huyu kaka jana alimkalia shingoni mkurugenzi hata leo asubuhi alikuwa naye bega kwa bega kiasi mkurugenzi akawa anakosea kusoma figures kwenye katatasi ya matokeo.

Hongereni CDM, lakini mjue CCCM wataendeleza vikao ili kubaini makosa yao yalikuwa wapi na kuyarekebisha.
 
Hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,
wazee wakiwezeshwa wana weza kufanya mabadiliko lets change the mind set of our elders.

Daima mbele nyuma ni mwiko.
 
Hii hati imenifurahisha zaidi...Tujifunge kiume kueneza elimu ya uraia kwa nchi nzima, ili watu wote watambue haki zao za msingi, na watoke kwenye giza la U-CCM, sasa wawe tayari kwa mageuzi ya ukweli.
 
[/QUOTE] Hongereni CDM, lakini mjue CCCM wataendeleza vikao ili kubaini makosa yao yalikuwa wapi na kuyarekebisha.[/QUOTE]


Toka lini wakajirekebisha. Jeuri ya pesa mbaya sana. Wanashauriwa lakini hawataki kusikia. Wenzao CDM wanawafuata wataalam wa siasa (wasomi) kutafuta ushauri na kuona wapi wajirekebishe, CCM hawaoni kwamba sasa hivi wanatakiwa kwenda kisayansi zaidi kuliko kuendeleza campaini tu zisizo na mwelekeo.

Wakati wa kuwaburuza watu umekwisha. Tujipange, tuangalie udhaifu wetu na tuwe na nia thabiti ya kujirekebisha siyo za unafiki. Wasomi wengi tunao, lakini hatuwatumii wala hatuwathamini kwamba wanaweza wakatubadilisha. CDM wanawakuza vijana kwa kuwafundisha kwa gharama lakini baada ya muda wanakuwa wazuri sana kisiasa. Uongozi mzuri ni kuanza na watu wapya na kuwafundisha yale unayoamini yatakuletea mabadiliko. CCM tumeshindwa nini wakati tunazo fedha na vijana wasomi tunao. Hapa ni kuwa na dhamira ya kweli kuelekea mabadiliko. Tuamke enzi za ujanja zimekwisha, tusome alama za nyakati!! Hongereni CDM.
 
Back
Top Bottom