Wazee wa mipango nipo juu ya mawe, sielewi nishukie wapi

Chief Kumbyambya

JF-Expert Member
Jun 16, 2022
490
1,461
Wasalaaaam waungwanaaa, nawasalimu kwa jina la upendo wa dhati.

Hivi sisi wazee wa mitungi ni vipiii? Wazee kama nilivyosema hapa niko juu ya mawe sielewi. Hii ni baada ya kupiga mtungi heavy jana. Sasa leo nimejikuta nimeamka na elf kumi na tano tu, naona hamjanielewa, yaani 15,000/= tu mfukoni.

Na ukicheki leo ndiyo kwaanza tarehe 13, yaani mwisho wa mwezi nauona kuuuleeeeee mbaaali yaani ni kama kuna mtu anazivuta siku nyuma zisitembee ili mradi tu anikomoe, ndani unga umekataa, mchele umekata, maharage yamekata, dagaa kwa makadirio zimebaki kama kijiko kimoja kile kikubwa cha kupakulia mboga. Nafikiri mmepata picha ndugu yenu niko juu ya jiwe kubwa kiasi gani.

Wajumbe wa ule uzi wetu pendwa wa mitungi wanasapoti sana kule ila ukitua tu juu ya jiwe kama hivi wanahepa.

Naamini humu kuna wataalam wa uchumi, bajeti na mipango mikali. Naomba mnisaidie kuibajeti hii 15,000/= ninunue nini na niifanyieje ili walau inifikishe tarehe 27 mwezi huu. Hapo nataka bajeti ya msosi tu.

Kuhusu kunyoa nywele nina kamashine kale ka 25,000= huwa najinyoa mwenyewe maana mimi ni mzee wa upara yaani DMX style. Kwahiyo bajeti ya kunyoa msiiweke hapo hiyo imepona.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom