Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Nao hawajitambui, ni kupiga makofi tu..... wastaafu wengi Dare salama, na baadhi yao wamezeekea hapa hapa na hawana vyanzo vya mapato, wakisikia mwaliko kutoka ikulu basi masikio huwasimama, wengi tunaishi nao na tunaona maisha yao kitaani! wamebakia kuwa makada na wana vikundi vya chama,

Sijui SERIKALI YA UKAWA itakuj nampngo kma huu na kama wataikia vile vile mwaliko wa awamu ya tano chini ya UKAWA?!?
 
ukitaka kujua wazee wa DAR anza na SAIGON .... Kama huifahamu SAIGON basi wazee wa dar waache tu!

DSCN1856.JPG

DSCN1853.JPG

SAM_0051.JPG

zaidi pitia hapa

au pitia hii thread

[h=1]SAIGON Club na siasa za Tanzania[/h]
 
Ni Wazee wote wa kiswahili wacheza bao na chuma ulete hapa Dar na pia ni makada watiifu kwa CCM sababu ya njaa na elimu yao ndogo. Ukienda Majiji na Mikoa mingine huwezi kukuta Wazee wasiokuwa na misimamo na wanaonunulika kirahisi kama hawa wa Dar. Na pia wao wanaamini sana kwenye ndumba kuliko Shule.
 
kuna watu katika jiji la dsm wazee kwa vijana , ukishawahakikishia wali na fanta take away utawakusanya mara moja , shida yao ni kula tu hawana shida na nyumba za kuishi maana tayari wana vijinyumba vyao vya urithi japo ni vya udongo ! hao ndio wazee wa dar es salaam , wengi ni wachumia tumbo tu .
 
Ndugu zangu,

TANGU Enzi za Mwalimu, kukiwa na jambo kubwa kitaifa, basi, Mwalimu aliliongea kupitia kwa Wazee Wa Dar Es Salaam. Na mahali haswa wanapokutana Wazee wa Jiji kumsikiliza Mkuu Wa Kaya ni pale Upanga kwenye Ukumbi wa Diamond.

Jambo hilo lililoasisiwa na Mwalimu sasa limekuwa ni utamaduni wa kisiasa. Mathalan, ni pale Upanga Diamond Jubilee ndipo Mwalimu alipotangaza vita dhidi ya Idi Amin kupitia Wazee Wa Dar Es Salaam.

Nilipokuwa mtoto pale Ilala, nilitamani sana nikue nije kuwa mtu mzima, kisha niwe mmoja wa Wazee wa Dar Es Salaam ! Ndoto yangu hiyo imefutika! Naam, nimepoteza sifa ya kuwa Mzee wa Dar Es Salaam!

Ndio, sifa ya kwanza ya kuwa Mzee wa Dar Es Salaam ni lazima uwe na zaidi ya miaka 50, uwe mkazi wa Dar Es Salaam kwa miaka isiyopungua 20 mfululizo! Hilo halijaandikwa popote lakini Wazee wenyewe wa jiji wanauzingatia utaratibu huo.

Siku za karibuni kuna Kijana wa Dar es Salaam kaninongoneza kuwa wako mbioni kuwashawishi wazee wa jiji waongeze sifa za kuwa mzee wa Darisalama. Kwamba ili uwe Mzee wa Dar Es Salaam ni sharti, ama uwe umezaliwa na kukulia Dar, au umezaliwa nje ya Dar lakini ujana wako wote umeishi Dar. Hivyo basi, unapoteza sifa ya kuwa Mzee wa Dar es Salaam kama umekuja Dar ukubwani! Marekebisho hayo ya taratibu na sifa yakifanyika, huenda hata mie nitakuwa na sifa ya kuwa Mzee wa Dar es Salaam.

Na Wazee wa Dar Es Salaam wana Mwenyekiti wao. Kwa kawaida siku ya shughuli ya wazee, huvalia kanzu, kibagharashea na kizibau. Ndiye huyu ambaye huwa wa kwanza kumpokea Mkuu wa Kaya anapoingia ukumbini kuwahutubia wazee.

Ni kwa namna gani basi Mwenyekiti wa Wazee wa Dar Es Salaam anachaguliwa?

Jibu: Hilo ni swali la kizushi na usithubutu kuliuliza mbele ya Wazee wa Dar es Salaam- watakutoa mbio kwa bakora! Lakini lililo dhahiri ni kuwa, Wazee Wa Dar Es Salaam hawajawahi kuwa na Mwenyekiti mwanamke. Hata Bi. Titi Mohammed hakupata kufikiriwa. Heshima ya kumpa barabara kuitwa kwa jina lake ilitosha, na amshukuru Julius, wanasema Wazee orijino wa Dar Es Salaam.

Ndio, Mkuu yeyote wa Kaya katika nchi hii atashauriwa aongee mbele ya Wazee wa Dar Es Salaam kama ana kubwa analotaka liwafike wananchi. Ni mara moja katika miaka ya karibuni nimemsikia Rais wa nchi akilihutubia taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dodoma.

Inasemekana jambo hilo liliwashtua baadhi ya Wazee wa wa Dar Es Salaam. Na kuna siku nilitembea kwa miguu mitaa ya Kariakoo Kusini; Livingstone, Mahiwa, Swahili na mingineyo. Hatimaye nikafika kwenye kijiwe cha chai na kahawa pale Mtaa wa Lumumba. Nilianzisha mjadala juu ya Wazee wa Dar Es Salaam. Na hapo nikayasikia manunguniko.

Ndio, baadhi ya Wazee wa Dar Es Salaam wanaamini kuwa Ilala ndio Dar Es Salaam. Na kwamba ni Wazee wa Ilala ndio waliompokea Julius Nyerere alipoingia mjini. Wanahoji; Iweje Wazee wa mashambani Kinondoni na Temeke nao waitwe Wazee Wa Dar Es Salaam? Swali linabaki; Wazee Wa Dar Es Salaam ni akina nani?

Maggid Mjengwa,
Iringa,
Wamesahaulika sana awamu hii
 
kuna watu katika jiji la dsm wazee kwa vijana , ukishawahakikishia wali na fanta take away utawakusanya mara moja , shida yao ni kula tu hawana shida na nyumba za kuishi maana tayari wana vijinyumba vyao vya urithi japo ni vya udongo ! hao ndio wazee wa dar es salaam , wengi ni wachumia tumbo tu .
Wanalimia meno zama hizi, sasa hivi tupo na Wazee wa Chato
 
Tuliwasahau kidogo lakini kwa vile mmetukumbusha basi kama sio wa Chamwino basi watakuwa wa nilikozaliwa
 
Sijajua masuala mazito yahusuyo hatima ya nchi yetu kupitia mchakato wa Katiba mpya kuzungumzwa kwa "wazee wa CCM wa Dar es Salaam!" Najua baadhi yenu mtasema kuwa Rais alikuwa anaongea kwa Taifa zima lakini implication iliyoonekana imekaa kichama zaidi kuliko kitaifa!

Hivi nchi hii imebaki ya hawa wazee wa DSM tena wa CCM au namna gani? Si ingekuwa ni vema Rais angeandaa kipindi ambacho watu wengi wangeshiriki tena kwa kuuliza maswali, kuliko kuhutubia hao wazee ambao wengi wao walikuwa wamelala usingizi na kushtuka baadhi yao wakiwa wanapiga makofi!
Wazee waabdamizi was ccm
Viongozi was dini
Viongozi wa mitaa
Wazee wenye biashara kubwa
 
Sijajua masuala mazito yahusuyo hatima ya nchi yetu kupitia mchakato wa Katiba mpya kuzungumzwa kwa "wazee wa CCM wa Dar es Salaam!" Najua baadhi yenu mtasema kuwa Rais alikuwa anaongea kwa Taifa zima lakini implication iliyoonekana imekaa kichama zaidi kuliko kitaifa!

Hivi nchi hii imebaki ya hawa wazee wa DSM tena wa CCM au namna gani? Si ingekuwa ni vema Rais angeandaa kipindi ambacho watu wengi wangeshiriki tena kwa kuuliza maswali, kuliko kuhutubia hao wazee ambao wengi wao walikuwa wamelala usingizi na kushtuka baadhi yao wakiwa wanapiga makofi!
Hao ni wachawi wa nchi
 
kuna watu katika jiji la dsm wazee kwa vijana , ukishawahakikishia wali na fanta take away utawakusanya mara moja , shida yao ni kula tu hawana shida na nyumba za kuishi maana tayari wana vijinyumba vyao vya urithi japo ni vya udongo ! hao ndio wazee wa dar es salaam , wengi ni wachumia tumbo tu .
Kesho kutakuwa na futari na nauli
 
Baada ya Uhuru ilikuwa na maana. Na zaidi Mwl alikuwa akikutana na wazee wa Mikoa mingine. Wale waliokuwa kwenye harakati za kupigania uhuru wetu.
 
Ni wale unaoenda kuwaomba wakushike kichwa wakutemee mate na wakutengezee wepesi katika majambo yako wakuweke kwenye dua...

Pia wawe wale wenye busara ....nguvu zile na pia wanaoweza kulaani au kubariki...watunmashuhuri wanaoijuwa nchi kutokea kijiweni....kahawa,,,, Sunderland,,,, wanaoijuwa historia ya tanu...msimbazi.....uhusiano wa karume na yanga....wale wajuaji wakikwambia tunakuwashia Moto unawashika kweli kweli......

Ni wale ukiona Mambo yanakuwa mazito unaenda kuwashtakia wanaokusumbua

Kuna
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom