Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Nikiwa ni mmoja wa washiriki kupiga kura, nimebaini kwamba nchi yetu ina majasusi imara kabisa katika ukanda huu wa Afrika.
Kuna mambo ya msingi kabisa kuhusu usalama na mstakabali wa nchi ambayo yanahitaji kuweka itikadi ya vyama pembeni.
Kama mheshimiwa Edward Lowasa "angetoka" katika uchaguzi huu, basi Tanzania ingekuwa katika hali ingine kabisa.
Kama kweli Edward Lowasa ambae hapo mwanzo niliweza kumpinga na baadae kuyumbishwa kidogo na kuhama kwake kwenda Chadema, amesaidiwa kwa hali na mali na baadhi ya watu kutoka nje, kuhakikisha anaingia Ikulu.
Kama kweli UKAWA waliajiri baadhi ya raia wa kigeni kuja Tanzania na kuvuruga matokeo pale kwenye maficho yao kwa kujaribu kurekebisha kuongeza idadi ya kura.
Kuna madai mengi mengi tu yanasemwa kuhusiana na matukio mbalimbali yalotokea nchi ilipokuwa ikielekea kwenye uchaguzi mkuu.
Lakini kazi ya kunusa, kufuatilia, kubaini na hatimae kufanya shambulizi pale ofisi ya ukusanyaji kura, ilikuwa ni kazi maalum na iliopangwa kwa ustadi mkubwa.
Sasa hatua ya kwanza imefanikiwa na ilobakia ni kumalizia kesi.
Ila yote tisa, kumi ni jinsi matunda ya vijana wa wazee Apson Mwango'onda na Hassy Kitine wanavyofanya kazi yao kwa uadilifu mkubwa. Wengi wa maofisa ni matokeo ya kazi ya wazee hawa wawili katika kuuhakikisha tunakuwa na maofisa mahiri kwenye kazi hii ngumu, ingawa mara kwa mara kumekuwepo na vijana wachanga ambao bado hawajamfikia Jason Bourne.
Idaya hii ya usalama au TISS ni idara imara, makini na inazidi kufanya kazi zake ikiwa kwa mwendo wa taratibu lakini makini.
Bila shaka yoyote raisi mteule Dr John Pombe Magufuli atazidi kuimarisha idara hii kwa mtindo mwingine kabisa, nikimaanisha kuwaondoka vijana ambao hawana dhamira ya dhati kufanya kazi hio, wenye kupoteza muda kwenye mabaa na kumbi za starehe na kuchezea magari ya serikali kiasi cha kupoteza fedha za kugharamia mafuta.
Je vipi mchango wako kwa wazee hawa wawili Apson Mwang'onda na Hassy Kitine?