Wazazi wenye watoto wa kiume kuna ujumbe wenu

Omesk

Member
Jan 24, 2020
34
232
Wazazi wenye watoto wakiume.

Dunia imebadilika hii, wafundisheni watoto kazi za nyumban, kuna leo na kesho. Sio kazi za nyumban ziwe za watoto wa kike tu. Dada yangu kapata wageni shemeji zake wadogo tu wamefunga shule..form 2, 4 , na 6. Hawafanyi kazi yoyote ndani kisa wa kiume.

Dada anaamka anafanya majukumu saa 2 anaenda kazini anamuacha bint na mtoto wa 1 yrs, bintI anadeki, anaosha vyombo, apike chai, afagie uwanja amwagilie maua, vijana wamelala chai ikiiva waamshwe wale mezanI hata kutoa vyombo hakuna, wakimaliza kula wanaamka wanaondoka....

YaanI sijui wamelelewaje tu hata kaka yao anaona kawaida tu.
 
Wazazi wenye watoto wakiume .
Dunia imebadilika hii,
wafundisheni watoto kazi za nyumban, kuna leo na kesho
Malezi naona sikuhizi yamebadilika sana..baadhi ya familia hakuna kupika, hakuna kufua, hakuna hata kuosha vyombo kisa eti watoto wa kiume.

Na hata kazi za mikono zingine kama kulima hata bustani tu za nyumba hawafanyi....wengi wanajificha kwenye kichaka cha kusoma..maisha bila kujua kazi za mikono sijui inawezekana vipi, hata kama watoto wa kiume lazima wafanye kazi za mikono...!
 
Wazazi wenye watoto wakiume .
Dunia imebadilika hii,
wafundisheni watoto kazi za nyumban, kuna leo na kesho
Sio kazi za nyumban ziwe za watoto wa kike tu.
Dada yangu kapata wageni shemeji zake wadogo tu wamefunga shule..form 2, 4 , na 6
Hawafanyi kazi yoyote ndani kisa wakiume.
Dada anaamka anafanya majukum saa 2 anaenda kazini anamuacha bint na mtoto wa 1 yrs , bint anadeki, anaosha vyombo, apike chai, afagie uwanja , amwagilie maua, vijana wamelala chai ikiiva waamshwe wale mezan hata kutoa vyombo hakuna, wakimaliza kula wanaamka wanaondoka....
Yan sijui wamelelewaje tu hata kaka yao anaona kawaida tu .
Wasukuma kiboko aiseee
Wasukuma gani hao awajafunzwa.... Ni hao hao wanaume wa Dar wanooa wanawake wa Dar mwisho wa siku ndo kama hivo. Wasukuma sio wanawake sio wanaume kila mtoto anapewa na kufundishwa kazi za nyumbani
 
Malezi ya hovyo tu.Mimi ni kijana sasa lakini tangu nikiwa mdogo nimekuwa nafanya kazi zooote kupika,kuosha vyombo n.k.

Sikuwahi jua kuwa hizi ni kazi za kiume ama za kike.Asante mama na baba kwa malezi yao.Yani mimi hata demu akija kwangu nampikia,naosha vyombo hata maji ya kuoga namchemshia,kwangu mimi ni kitu cha kawaida tu
 
Dada anaamka anafanya majukum saa 2 anaenda kazini anamuacha bint na mtoto wa 1 yrs , bint anadeki, anaosha vyombo, apike chai, afagie uwanja , amwagilie maua, vijana wamelala chai ikiiva waamshwe wale mezan hata kutoa vyombo hakuna, wakimaliza kula wanaamka wanaondoka....
Hizi tabia zinasambaa kama kunguru wa Zanzibar bara, zamani hizi tabia za kimwinyi zilikuwa pwani, kama sasa zimefika ungoshani basi kuna mahali tumeyumba na hasa huko elimu ya Msingi
 
Dah wajinga hao wengiw wakifa chuo wanashindwa kula kweny vibanda .Chuo nilikuwa raha getto napika sichangii ndo mchango wangu wengi wakishua ,ndo maana ukienda baadhi ya mageto ya masela mavyombo kibao uchafu wa kijinga kabisa
 
Oi! kila jinsia ibebe jukumu lake mwisho siku ndio mnakuja na diversity mara haki sawa na 50 kwa 50, my damn foot!
Mimi sijui kupika wala kuosha vyombo lakini nimefundishwa majukumu yangu ni kufanya kazi na kula kwa jasho, uongozi na kutawala, kutafuta pesa na kuhudumia familia na ulinzi wa familia na kazi zote ngumu zinazohitaji nguvu mimi mtoto wa kiume ndio nitazifanya.

Hayo mambo ya kukaa jikoni kulegeza mikono kuzungusha mwiko na kusugua vyombo wafanye wengine.
Kupika na kuosha vyombo nitafanya kama naishi mwenyewe tu yaani hakuna mwanamke ndani na sio zaidi ya hapo na ndio maana nitaoa mapema sababu hizo kazi ndogondogo ni vitu nisivyovipenda na kuvichukia kupitiliza na sitaki kuvisikia.

Kama hakuna kazi za kike wala za kiume je kuna mwanamke anaweza kubeba friji begani humu? kubeba gunia la kilo 70? kurekebisha waya za umeme? kupigana na wezi usiku na kutoka nje saa 9 ukisikia kelele za mlango au geti?

Na sio ajabu kukuta vijana wanahamasishana kutokuoa sababu hawaoni faida ya mwanamke ndani na ni waoga na wamelegea zaidi ya watoto wakike.
 
Dah, wameendaje mashemaeji watatu wote kwa kaka? Anyway mwambie dada yako awaamshe asubuhi wafanye kazi au dada anawaogopa.
 
Usinikumbushe hiyo kabila ilivo nzuri.

Rafiki angu aliolewa huko yani ni full fuluu maajabu. Ndugu wa mume wanakuja kuishi hapo home kwake. Mmoja anaweza kuja na watoto wawili mkubwa Kwa mdogo ..yule mdogo ana hulka ya kuchezea vyakula mfano kumwagia maji sukari,unga life lenyewe lilikuwa tait mtoto mkubwa akimkataza mama mtu anamwambia dada mtu....mwache mtoto acheze.

Shemekiii akiona hizo furugu za ndugu zake MBIOOO ANAJIPA SAFARI KIKAZI anamwacha bidada aparangane nao yeye anatifua. Asionekane mbaya Kwa ndugu zake.

Aseeeeeeee.

Nje ya mada.
 
Back
Top Bottom