Wazazi wanaweza kuwa na maono juu ya wenza wa watoto wao?

KOKUTONA

JF-Expert Member
Jan 29, 2011
8,649
6,088
Habari za maandalizi ya kuhesabiwa.

Nimekuja na hili swali sababu kuna incidents zimetokea katika mazingira ninayoishi na kwa baadhi ya rafiki zangu.

Incident ya kwanza kuna binti mmoja alitokea kumpenda mkaka mmoja, walipendana sana but dini zilikuwa tofauti, wazazi wake hasa baba yake alikuwa mkali mno, kupinga yale mahusiano, akisisitiza kusema moyo wake unasita kumuamini jamaa kabisa as the perfect husband. Na pia hakuwa tayari kuona mwanae anaolewa na mtu wa dini tofauti.

Binti kuona anabaniwa akaamua kushika mimba ya jamaa ili iwe rahisi. Na kweli familia haikuwa na jinsi. Wakati mipango ya ndoa inaandaliwa jamaa akaja kuaga kuwa amepata transfer so anaomba akaripoti kwanza then atarudi wakamilishe mipango. Ndo ilikuwa for good, na haikupita hata miez mi2 tukapata habari huko aliko ameoa, tena kwa harusi kubwa.

Binti akakalishwa chini akaambiwa tulikwambia, wazazi wakafanya mpango wakamuhamisha wilaya nyingine but ktk shirika alilokuwa anafanya kazi. Huko tena akapata wa kumpoza roho, dini tofauti tena but akafanya siri kubwa, but bahati mbaya shirika aliokuwa anafanya ni la dini mno, so mahusiano nje ya ndoa kwa mtmishi n tiketi ya kufukuzwa kazi,na waligundua hilo wakawa wanamlia mingo binti. Kabla hawajaprove wazazi wa binti wakapta taarifa wakafunga safari, kwenda wanakuta binti yao kawekwa kinyumba. Walirudi midomo wazi, but hawakusita kumwita bintti yao na kumweleza, walichomwambia ni kuwa mwanaume anaekupenda na mkweli hawez fanya mapenzi ya siri na mbona amekaa na was was. Binti akasema wa kwanzi mlisema na huyu mmeanza kusema, vyovyote alivyo mm nampenda.

Haikupita hata wiki wazazi wakaitwa kuambiwa mtoto wao (binti) anashikiliwa na polisi kuisaidia maana mwanamume anaeishi nae amekamatwa baada ya kugundulika anaficha na kutibia majambazi, wakaenda wakamtoa mtoto wao kwa influence. Wakiwa bado stressed wanapata barua toka shirika kuwa wana mpango wa kumtimua binti sbb ana mahusiano nje ya ndoa na wanataarifa kuwa binti is pregnant. (wazaz walikuwa wanafahamiana na baadhi ya vibopa wa shirika) Binti kuulizwa ikabidi awe mpole. Wazaz hawakuwa na jinsi zaidi ya kuwafungisha ndoa ya bomani kunusuru kazi but hawakuwa na baraka na mwanamume wakidai hawana imani nae.

Maisha ya binti huyo ambaye sasa ni mama wa watoto wa3 hayakuwa mazuri kabisa manyanyaso na kadhia zote, na bahati mbaya mradi ulipunguza wafanyakazi naye akiwemo (elimu ndogo). Hana furaha ile aliyoitegemea na wazazi km wamemsusa. JE? HII INAWEZA KUWA NA CONNECTION NA MAONO YA WAZAZI?

Incident ya pili huyu ni wa ndani ya familia yetu kwa kias flani, yeye alimpenda kijana mwenye mafanikio tu, pesa ya kutosha na maisha ya at least kupata luxury kwa sana. AKadata na hakuambiwa kitu na mtu. Then akawaambia wazazi rasmi kuwa amepata mchumba na anataka kuolewa, wazazi hawakupinga na wkapenda kuonana na muoaji na familia yao ikiwezekana.

Siku ya siku jamaa akatia timu, wakafanya mazungumzo na baba wa binti for long hadi watu wakawa na was was kulikoni. Baadae baba akamwita bintikumuuliza kama kweli pale ndo amefika bei na ni lazima aolewe na jamaa. Huku akimconvince binti yake km vp ahairishe, akitoa sbbu kuwa anahisi kuna siri nyuma ya macho ya jamaa, but binti msimamo na harusi ikafungwa.

Baada ya km nusu mwaka yule binti akaanza kupata msgs za ajabu ajabu, zingine zikimsihi amchunguze sana mume wake. Hakujali wala maana alikuwa kafika though wazazi walikuw bado warried sana, akapata mtoto wa kiume na maisha yakawa yanaendelea.

Siku ya siku akaja mdada asiyemjua akijitambulisha km hawara wa mume wake, she was shoked, mdada akamwambia usipate presha mapema kujitambulisha kwako nitheluthi ya utakayokwenda kuyaona, akamzoa wakaenda night club ambako alishuhudia mumewe akiondoka na malaya. It was shoaked day kwake alilia sana na mumewe hakurudi, na ilikuwa kawaida yake akitoa excusese safari za ghafla, biashara, vikao wakati huo alimwamini, but that day alijua ukweli.

Alichofanya asubuh yake ni kuanza kupekua vitu vya jamaa, kitu ambacho hakuwah kufanya maana alimwamini, alikumbana na box la vidonge, aliamua kwenda navyo hospt, akajieleza wakamwambia ni ARV, alichanganyikiwa akashauriwa kupima kupima,majibu hayakuwa mazuri, alimpima na mwanae, goodluck alikuwa salama. Alirudi kwa wazazi wake na kilio kikubwa ninge wasikiliza. Wazazi waikuwa waelewa wakampokea na hakutaka kurudi tena kwa mumewe pamoja vikao vingi vya familia kukaa kuyazungumza. HILI NALO JE?

Nina incidents nyingi but naogopa kuwachosha na maandishi mengi.

Karibuni.
 
Absolutely,wazazi huwa wana matashi over 99%.Halafu me nafikiri kile kitendo cha kutoridhia tu hata kama mwenzi ni mzuri tayari kinawawekea doa flani kwenye ndoa.nguvu ya ulimi
 
wazazi wana maono juu ya uchaguzi wa mwenza wa mtoto wao, me kaka yangu aliwahi kuambiwa akakataa...........leo ninavyoongea mkewe kamuacha analea watoto wake na hatamani kuoa tena... JAMANI WAZAZI WANATUFAHAMU SISI KULIKO TUNAVYOJIFAHAMU NA WAZAZI HUTOA BARAKA ME NAWASHUKURU WAZAZI WANGU KWANI KILA NIKIWASIKILIZA NAFANIKIWA ZAIDI.... SO GUYZ HAIJALISHI WAZAZI WAMESOMA AU HAWAJASOMA JUST LISTEN THEM
 
Possible kabisa jeneneke, maana cases nyingi wwazazi wakiweka mashaka tu mwisho unakuwa wa matatizo. Inauma zaidi mtu ndo umempenda kupitiliza. Blindly in love.
 
wazazi wana maono juu ya uchaguzi wa mwenza wa mtoto wao, me kaka yangu aliwahi kuambiwa akakataa...........leo ninavyoongea mkewe kamuacha analea watoto wake na hatamani kuoa tena... JAMANI WAZAZI WANATUFAHAMU SISI KULIKO TUNAVYOJIFAHAMU NA WAZAZI HUTOA BARAKA ME NAWASHUKURU WAZAZI WANGU KWANI KILA NIKIWASIKILIZA NAFANIKIWA ZAIDI.... SO GUYZ HAIJALISHI WAZAZI WAMESOMA AU HAWAJASOMA JUST LISTEN THEM

Inakuwaje pale unapokuwa umempenda mwenza kweli kweli na mshapanga mengi, then mwisho wasiku wazazi wanagoma.

Ni wakati mgumu kweli, ether ufuate moyo wako au ya wazazi wako.
 
Yah hii kweli sana.

Wazazi ni miungu ya hapa duniani.

Wana uwezo mkubwa sana wa maono juu ya watoto wao.

Kuna mifano mingi sana ya mapenzi na isiyo ya mapenzi.
 
Nimesoma nusu lakini mi ni mmoja wa watu nilokuwa nawaheshimu sana wazazi na hata mume alonioa tulioana baada ya wazazi kuweka tiki. Hakuna mzazi anayeweza kumpa mtoto ushauri usofaa unless hao wazazi wawe na kasoro fulani.

Hivyo basi kabla mtu hujafikia kusema huyu ni mchumba wangu unapaswa umpeleke kwa wazazi as boyfriend ili watoe marks zao. Wakimkataa uanze kujipanga polepole.

Na wazazi walio makini uwa wanawaambia kabisa watoto wao sifa za mume anayefaa...hivyo hata mtoto anakaa akijua kuwa nikimpeleka huyu wazazi watamkubali...huyu watamkataa.

Nina mdogo wangu alimpeleka boyfriend wake kwa wazazi wazazi wakasema huyu si mume. Mdogo wangu alilalamika saana; akasema baba na mama hawako fair...kijana hana kasoro yoyote. Mi nikawa nampoza lakini deep inside nilikuwa nasema lazima kuna ukweli kwa jinsi navyowajua wazazi wangu.

Waliendelea na urafiki...baada kama ya miezi sita wakaachana...nadhani mdogo wangu alianza kufanyia kazi taratibu maneno ya wazee na kuanza kuona dalili za waliyosema.

Wengi wa wanaojishikisha mimba kuwakomoa wazazi wanaishiaga pabaya...nina mifano kede kede. Ndoa ni zaidi ya mapenzi.

Ila zaidi ya wazazi mimi sikubali ushauri wa dada na kaka....as long as wazazi wamekubali inatosha. Nasema hivyo kwa sababu nina dada yangu huyo yani alikuwa anataka tuolewa na Mr. Perfect kwa kuwa yeye mume wake alikuwa anamuona ana mapungufu kibao...na kwa mapenzi yake kwetu alikuwa anataka kurekebisha makosa yake through us. Hii ni hatari sana... tungemsikiliza tungedoda. Maana kila unayempeleka kwake anasema piga chini.
 
Tushirikishe basi mkuu ili tupate elimu zaidi.
 
Nakubaliana na wewe kabisa nyumba kubwa, maana kwa uhalsia chochote kisichokuwa na baraka za wazazi msuko suko lazma itokee.

Swala la kumtambulisha mwezi wako kwa wazazi at early stage nalo lina umuhimu wake kuepusha mengi in furture. Muhimu sana sana.
 
Nimesoma nusu lakini mi ni mmoja wa watu nilokuwa nawaheshimu sana wazazi na hata mume alonioa tulioana baada ya wazazi kuweka tiki. Hakuna mzazi anayeweza kumpa mtoto ushauri usofaa unless hao wazazi wawe na kasoro fulani.

Hivyo basi kabla mtu hujafikia kusema huyu ni mchumba wangu unapaswa umpeleke kwa wazazi as boyfriend ili watoe marks zao. Wakimkataa uanze kujipanga polepole.

Na wazazi walio makini uwa wanawaambia kabisa watoto wao sifa za mume anayefaa...hivyo hata mtoto anakaa akijua kuwa nikimpeleka huyu wazazi watamkubali...huyu watamkataa.

Nina mdogo wangu alimpeleka boyfriend wake kwa wazazi wazazi wakasema huyu si mume. Mdogo wangu alilalamika saana; akasema baba na mama hawako fair...kijana hana kasoro yoyote. Mi nikawa nampoza lakini deep inside nilikuwa nasema lazima kuna ukweli kwa jinsi navyowajua wazazi wangu.

Waliendelea na urafiki...baada kama ya miezi sita wakaachana...nadhani mdogo wangu alianza kufanyia kazi taratibu maneno ya wazee na kuanza kuona dalili za waliyosema.

Wengi wa wanaojishikisha mimba kuwakomoa wazazi wanaishiaga pabaya...nina mifano kede kede. Ndoa ni zaidi ya mapenzi.

Ila zaidi ya wazazi mimi sikubali ushauri wa dada na kaka....as long as wazazi wamekubali inatosha. Nasema hivyo kwa sababu nina dada yangu huyo yani alikuwa anataka tuolewa na Mr. Perfect kwa kuwa yeye mume wake alikuwa anamuona ana mapungufu kibao...na kwa mapenzi yake kwetu alikuwa anataka kurekebisha makosa yake through us. Hii ni hatari sana... tungemsikiliza tungedoda. Maana kila unayempeleka kwake anasema piga chini.

Kumbe hili neno 'kudoda'
ni neno fair kabisa lol
 
Yote kwa yote, bado nina swali la kuuliza. Je? wale wazazi waokataa wenza wa wanao kwa chuki binafsi tu but anashikilia mwamvuli wa maono?

Na mara nyingi ni ngumu kujua, but wapo.
 
wazazi kinawasaidia 'upeo' kutokana na uzoefu wa maisha.

Watoto wanakuwa 'head over heels' wanasahau uhalisia.

Wazazi kweli wana upeo na macho ya kuona mbali.

Hapo head over heels, ni kwa sbb ya kupenda sana au ni nini?
 
Back
Top Bottom