Wazazi wakataa kupokea mahari ya binti yao anayeolewa

Mahari ni lazima si jambo la hiari mana binti yako si sawa na mfugo unamtoa tu..lazima uthamani uwepo
Na alietoa mahari huwa anapenda kumiliki binti kama chombo kwani amelipia, kitu ambacho humfanya binti anyanyasike na kudhalilishwa!
 
Hongera sana maana wanaume mlivyo simba hongera kwa kutomvua kyupi,
sisi nyumbani kwetu tuliishi na dada ambae mama alimchukua 1994 huko rwanda ametulea weee hadi tunafanana. 2004 aliolewa mahali mama alipokea sherehe tukafanya! Baada ya ndoa mama amewasaka wazazi wake bila mafanikio,

hela ilobaki dada bea alimwambia mama amununulie ng'ombe mpaka wa leo huyo ng'ombe yuko zizin kwetu anazaa dada bea akipata shida ndo wanamsaidia.

Watoto wa dada bea sasa hivi ndo wajuku wa mama wanaishi na mama ndo wa kuwatuma vocha dukani, wanampenda mama hadi kwao huwa wanatoroka wakaishi kwa bibi mama yangu.

So wewe pokea baadae jipange uwapelekee zawadi ya kudumu nyumbani!

Unaweza kuwanunulia mbuzi hata wa 5 kutokana na mahali utakayo pewa then uwapelekee wakafuge kwa ajiri ya matumizi ya nyumbani.

Tatizo kama kwenu mahali ni laki 2 kama baadhi ya wahaya hapo itabidi upeleke vizawadi vya kawaida. ila kama ni kwetu ng'ombe 8-15 basi mtagawana sawa.

Asante kwa kulea
 
Oh aisehhhh mkuu wewe una utu sana, viumbe vya aina yako bado vipo duniani kwa kweli nilihisi vimepotea, umenigusa sana mkuu, kwanza nianze kwa kukupa pongezi zangu za dhati kabisa,kubwa hasa kwa malezi mazuri yaliyo tukuka uliyompa huyo binti(house girl ),

Kwa upande wako kwa haraka haraka unaweza ona jambo la kawaida kwa mambo mazuri uliyomfanyia huyo binti ila umemfanyia mambo mazuri na kubwa hasa ya yote msaada wako kwa binti ni ya mikakati ya muda mrefu hasa kwenye elimu,

Mimi binafsi naona ndo namna hata wazazi wake wanachanganyikiwa kwa upendo uliompa mtoto wao na imefika mahala wanakupa heshima hiyo, mimi naona ukubali tu kupokea mahali hiyo halafu tafuta kitu cha thamani pitia hiyo mahali peleka kama zawadi kwa wazazi wa binti, kwa kweli you did abig role kumsaidia huyo binti na Mungu atazidi kukufungulia milango ya baraka, watu wanatakiwa wajifunze pitia wewe,

Wasiwasi wangu mwingine ni juu ya watoto wako punde dada atakapo ondoka dah yani nimewazia hapo sana koz i am the living example maana limeshawahi kunitokea na ilichukua muda sana kukubali uhalisia.
Familia nyingi zinachukulia house girl ni mtumwa na akina mama mji utakuta wamedeka na wanawanyanyasa sana wafanyakazi wa ndani,wanasahau kama wao ni binadamu na kuna siku unaweza toka duniani na kuwaacha watoto wakilelewa na house girl huyo.
 
Bibi vipi mbona umekalia kuangalia makosa tu zaidi ya kushauri..

Katika mila za kwetu za Kiislam mahari ni ya binti anaeolewa kwa hiyo kusingekuwa na utata huu wa kijinga wa mahari kuwa ya wazazi, huko ni sawa na kumuuza huyo binti.

Wapokee mahari wamkabidhi huyo binti, yote. Na yeye binti kwa kuwa ni haki yake hiyo ataamuwa aifanyie nini mahari yake.
 
Mtihani huu umekuwa mgumu sana kwangu sababu kwanza wale ndio "biological Parents" wa huyu binti,tena bado ni wazima na wana afya tu japo ni wazee.Lakini nawaza hii ya kupokea mahali kwa mtoto sio wako ina uhalali kweli?

Ndugu! Pokea mahari kwa niaba ya wazazi wa damu!
Umepewa heshima kubwa! Panga mahari kwa mujibu wa mila ya kwao ,mmtafute mzee wa huko waliko wazazi wake wa kumzaa siku ya kupokea mahari au hata mjomba mtu. Ukishapokea Mahari -mali hiyo fanya namna itawafikia wazazi bila wao kujua na usile hata senti mmoja. Miradi ya maendeleo iko mingi -inategemea ni wazazi wanaoishi maeneneo gani! Lakini kwa kumshirikisha huyo dada!
 
Afande kifimbo hebu boresha uandishi wako ili ueleweke,kingine ni sio swala rahisi kama unavyo liwazia, mtu mwenye busara hili jambo ni lazima likufanye uwaze sana na mabo kadha wa kadha, na kumuambia jamaa ukweli kwamba binti alikuwa housegirl kwa kweli sio kumsaidia na sio kila jambo kuliweka wazi linaweza kuwa ni msaada au kueleweka, mambo yanaweza badilika baadae katika maisha ya ndoa jamaa akaanza kumdharau na kumkejeri binti wa watu kwa kuwa alimkuta kwa mtu kama housegirl ni heri ajuwe anacho juwa sahivi.
Ok usipomuambia af akaja kujua baadae inafikiria nini juhusu hilo......concern yangu ni ajue kitu ulichoficha.......maana ataamua kumdharau kwa kuwa alikuwa house gl hupni kwamba tatizo ni lake na hatakuwa na upendo wa kweli........maana mi mawazi yangu ya akuli ndogo angejuajapp history kuwa ana wazazi wake nahapo alikuwa housegirl ila ukamlea kama mtoto wako...hiyo itamfanya aone upendo wenu wa hali ya juu hivo nate awe muwajibikaji...ni mawazo yangu tu
 
Pokea hiyo mahali wazee wamekuaminj na una baraka zao but unaweza kuitumia hiyo mahali kwa maandalizj ya sherehe au mpe binti mwenyewe

Ila huyo jamaa mwambie ukwelj kama kampenda huyo binti hakuna shida.ila kama kampenda sababu ni Mtoto wako heeee hilo ni tatizo.

Anyway tualikane coz daah sijaudhuria sherehe kitambo Nina hamu na ubweche aka wali mchafu
Usisahau kuja na limao na ndizi na pilipili walau moja.
 
Laiti kila familia zenye h/grls wangewafanyia hivi kweli familia zote vijjn zingeomba kheri watu wangekuwa wako paradso. Mwambie mkwe kuwa wewe ni mkwe kwaajili umemlelea bnt na bnt ulipewa na rfk za mkeo na mahari pokea tumia kwa ajili ya kuwaleta wazazi husika mjn kwa hrusi ya mwanawe na kuwapgsha pambaa nk siku ya harusi na kubalianeni na bint na mkeo
 
Mimi sana sikupongezi wewe ila nampongeza na big up kubwa mkeo, hawa aina ya wanawake ulionao wameishapotea katika ulimwengu, nahis amebaki yeye tu. Wanawake ni wakatili sana Kwa hawa wadada wa kazi mpaka unaona mambo mengine uingilie katikat, mnawachukulia wadada wa kazi kama punda, ndio maana wanafanya ukatili Kwa watoto,
Ukiona housegirl kafanya ukatili kwako jiangalie vizuri, wanawake hawataki kabisa kushiriki na wanaume katika malezi ya mabint hawa. Ukiongea tu umeishampenda.
Nazid kupongeza shemeji yangu hakika una mke mwema sana kaka,
Mimi ndoa miaka 5 tu housegirl 15 wameishaondoka yuko wa kumi na sita, nimeyataman sana maisha yako,
Mahali chukua na may be wakati wameogopa gharama za mjin za sherehe so wanataka wakuachie wewe mwenyeji wao ufanye yote, na ukweli hili ni jukumu lako usilikwepe,waite wazazi au ndugu zake wewe kama kiongoz mchukue Mahali then harus msindikize bint Kwa Aman. Nataman ndoa ya namna hii hapa hata michepuko huwez kuiwaza kabisaaaaa.
 
Wala hana point. Tunaosomesha mahausigelo ndio tunaelewa hizi mambo. QT ni mpango maalum, unaanza miaka 2 kupata cheti cha form 4, mwaka mmoja kupata cha form 6. Kama alirudia mtihani basi alisoma 3 yrs. Ukiweka ya chuo 3, that is 6yrs.
Acha kudanganya watu wewe. Mtu alifeli qualifying test mara 2 asome form 5&6 mwaka 1 afaulu? Afu hata form 3&4 hawezi kutoboa kwa NECTA labda miujiza.


NB: Mimi ni Mwalimu nawafundisha hao ma-house keepers mnawasomesha nyinyi. So, nawajua vizuriii
 
We kaka na familia yako mnae mioyo mikunjufu. Mungu awabariki na kuwazidishia ninyi na uzao wenu.
 
Hapo ume-describe ualimu wako ama utabiri? yaani unakuwa kama wale wasoma nyota? hahaha shkamoo ticha wa voda fasta.

Kuna ndugu yangu nampenda sana, ni mfano kuwa unaweza kubadili maisha yako. Alipata div 4 ya mwisho kabisa, akakaa kijijini mwaka mzima. Akaitwa na aunt yake akaingia lugalo akarudia mitihani. Akafanikiwa akaingia high school. Form 6 akang'oa div 1. Sasa hivi ana masters.

Haya ticha, endelea kukremisha sylabus
Acha kudanganya watu wewe. Mtu alifeli qualifying test mara 2 asome form 5&6 mwaka 1 afaulu? Afu hata form 3&4 hawezi kutoboa kwa NECTA labda miujiza.


NB: Mimi ni Mwalimu nawafundisha hao ma-house keepers mnawasomesha nyinyi. So, nawajua vizuriii
 
Pokea mahari then mkabidhi binti yeye ndo ataipangia matumizi.mahari ni haki na ni halali ya muolewaji hivyo yeye binti ndo mwenye final say.
 
Hapo ume-describe ualimu wako ama utabiri? yaani unakuwa kama wale wasoma nyota? hahaha shkamoo ticha wa voda fasta.

Kuna ndugu yangu nampenda sana, ni mfano kuwa unaweza kubadili maisha yako. Alipata div 4 ya mwisho kabisa, akakaa kijijini mwaka mzima. Akaitwa na aunt yake akaingia lugalo akarudia mitihani. Akafanikiwa akaingia high school. Form 6 akang'oa div 1. Sasa hivi ana masters.

Haya ticha, endelea kukremisha sylabus
Tatizo lako we ni mbishi bila facts. First, sija describe ualimu wangu bali nimekupa angalizo kama wewe ulivodai unawasomesha ma HG
PILI, huwezi kumfananisha mtu anaye reseat mtihani (alisoma mpaka IV) na mtu wa QT.

NB: punguza ubishi uso na maaana.
 
Sawa ticha.
Kwa hiyo tunakubaliana mie sina facts, na mtoa mada ni muongo?

Angalizo, kuna watu wameishi kwenye uhausigelo just because their parents were too poor to pay school fees ama traditions na hali haikuruhusu wao kwenda shule. Hawajawa mahausigelo kwa sababu they are dumb. Hapo sibishi nakupa angalizo tu baba
Tatizo lako we ni mbishi bila facts. First, sija describe ualimu wangu bali nimekupa angalizo kama wewe ulivodai unawasomesha ma HG
PILI, huwezi kumfananisha mtu anaye reseat mtihani (alisoma mpaka IV) na mtu wa QT.

NB: punguza ubishi uso na maaana.
 
Sawa ticha.
Kwa hiyo tunakubaliana mie sina facts, na mtoa mada ni muongo?

Angalizo, kuna watu wameishi kwenye uhausigelo just because their parents were too poor to pay school fees ama traditions na hali haikuruhusu wao kwenda shule. Hawajawa mahausigelo kwa sababu they are dumb. Hapo sibishi nakupa angalizo tu baba
Sijui nikwelezeje unielewe. Sikatai kwamba yaliyo kwenye mada hayapo, a big NO.
But nnachokielezea hapa ni hisia zangu binafsi, nilishindwa kuamini kwa 7bu nilizozitoa. Sijui umenielewa?
Binafsi naamini, mada si ya kweli but imeletwa JF kwa malengo kama kuelimisha au kuonya.
Au
Kuna chumvi zimeongezwa kwenye mada
NB: refer my first comment
 
Back
Top Bottom