Wazazi tuwaweke watoto na ndugu zetu wanaopambana na ufisadi mikononi mwa Mungu; kuna familia zinalinda madaraka kwa kumwaga damu.

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,124
Kuna watu wameingia kwenye mfumo wa siasa na biashara wanaishi Kwa dili. Ukisikiliza bungeni ni kama vile wanafanya siyo Kwa Siri tena Bali wanafahamika na hakuna wakuwafanya chochote.

Tumemsikia Msukuma kuhusu sakata stika za ushuru; anasema wazi kwamba kuna watu wanufaika na kwamba anaogopa kuwataja. Suala la stika liliibuliwa tena huko nyuma mwaka 2021 na Mhe. Secili bungeni na hakuna hatua zilizochukuliwa. Mhe. Msukuma anakwenda mbali zaidi kumtia moyo Waziri afanye maamuzi as if waziri pia anatishwa kufanya maamuzi. Kama waziri Hana nguvu yakuamua hata baada ya mkataba kuisha unategemea hao waliopo nyuma ya dili kubwa hivi ni wezi wenye nguvu kiasi gani?

Tumesikia sakata ya tigwa na Tanga cement..watu wanafungua kiwanda hewa cha Chalinze na kwenda kwenye mikono ya sheria kuomba Haki na hakuna wakuwafanya kitu. Waziri anaulizwa anasema tumekifuta kiwanda cha Chalinze Kwa Sababu kina usajili hewa....simple answers kwenye serious matters. Ukifuatilia waliokuwa wajumbe WA Bodi ya Tanga cement unagundua wapo matajiri nchi hii wameshindwa kulisaidia nchi wamebaki kuinyonya na kuwapa rasilimali wageni.

Twende kwenye ajali ya binti WA UDOM; inatokea ajali yenye utata vyombo vya dola vinashindwa kuondoa utata WA kifo cha mwanafunzi. Wanaeleza mambo yanayozua utata. Chuo nacho kinaandika taarifa isiyo eleweka. Nani yupo beyond hizi sarakasi? Means wapo watu wakubwa ambao kwao maadili si hoja Bali ulinzi wa matajiri na wanasiasa ndicho kipaombele.

Tumalize na ripoti ya CAG, watumishi wawili wamefariki kwa kufuatana na watu wametilia mashaka vifo vyao. Kufariki kwao kumezima kabisa mijadala ya ripoti ya CAG mitandaoni na Bungeni. Kwanini ukimya iambatane na kifo chao? Means wakubwa wanajua namna matajiri na familia Bora za nchi zinavyooperate.

Kwa mifano hii, inatosha kusema kwamba kuna familia zimejijenga kama familia za kifalme. Wao ndio wanashika deals za serikali, wao ndio wanaamua nani atawale na wao ndio wanaamua nani awajibishwe na Nani asiwajibishwe. Ukiwa na Taifa ambalo mafisadi wanaweza kutishia hata kiti cha Mhe. Waziri asifanye maamuzi na anaonekana ameshindwa kazi basi tuliombee Taifa

Tuwaombee Sana vijana wetu wanaofanya kazi kwenye vyombo vya dola wasirubuniwe na matajiri na wanasiasa wakawa watoa uhai WA watu wasio na hatia wakiaminishwa wanalitetea na kulinda Taifa kumbe wanalinda interest binafsi za watawala.

Tuwaombee vijana wetu wanaopambana na rushwa wasifikwe na mauti Kwa Sababu Tu wanalipigania Taifa letu. Mwenyenzi Mungu awafunike na kuwapa ulinzi waweze kusimamia Haki.

Tuwaombee waliotumika kama wasiojulikana wakiaminishwa wanatetea maslahi mapana ya nchi waweze kupewa msamaha huko mbinguni na kikombe cha laana kisiambatane na familia zao Kwa Sababu kitazalisha watu katili na wanaoweza kufanya maasi makubwa huko mbeleni

Dini zote zikimtanguliza Mungu tunaweza kuliponya Taifa; NI hatari Sana kuwa na watoto WA wakubwa ambao NI wezi na wanatumia rasilimali za nchi na pesa za walipa Kodi kuamua Nani awe kiongozi na akiwa kiongozi lazima awalinde wao. Failing state uanza na wezi wenye nguvu na kuishia kwenye mapinduzi.

Nimewiwa kuomba dua hii Leo kanisani na kusukumwa kuwaandikia wananchi wenzangu tuliweke Taifa mikononi mwa Muumba WA mbingu na nchi. Nimepata maono kwamba zipo familia zinaamini zinaishi vizuri kumbe wazazi wao mikono Yao inanuka damu....tuziombee familia zetu zile na kunywa riziki ya Haki siyo kunywa damu za yatima na wajane waliotokana na uchu WA Mali na madaraka.

Mwenyenzi Mungu amlinde Mhe. SSH na baadhi ya viongozi aliowateua wanaowaza kulisaidia Taifa. Mwenyenzi Mungu ampe ufunuo wakuziweka mbali na utawala wake familia za wachache zilizojaa kiburi na zinazowaza kushika dola Kwa gharama yoyote.

Jumapili njema 06/05/2023
 
Back
Top Bottom