Nelson Masaduki
JF-Expert Member
- Oct 27, 2017
- 346
- 380
Wanabodi,
Poleni kwa msiba wa MV Nyerere.
Nimetafakari sana kazi iliyofanywa na wenzetu, wazamiaji waliopo katika eneo la Ukara, kabla ya serikali kuanza kuifanya kazi ya kuokoa na kutoa miili ya waliofariji katika ajali ya MV Nyerere. Ninadhani, ingekuwa busara sana endapo serikali ingepata majina na taarifa za watu wote walioshiriki kazi ya kuzamia majini na kuwapa ajira serikalini. Ajira zao zisaidie katika maeneo waliyopo. Katika maeneo yote yenye maziwa, mito na bahari, waanzishe
"Rapid Rescue Team" ambayo itajumuisha watalaam wa asili na watumishi wa taasisi nyingine serikalini.
Ni wazo tu, wanaweza kulifanyia kazi
Nelson