Wavuta Bangi wote Duniani sasa ni ' Shangwe ' tupu kwani Coca Cola kuja na Kinywaji chake chenye Bangi tupu!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,744
109,186
Kampuni ya Vinywaji baridi bora kabisa Duniani ya Coca Cola inafikiria kuja na Soda ' Maalum ' ambayo itakuwa imetawaliwa na ' Mmea ' kamili wa Bangi / Bange ili iweze kuongeza Soko lake kwa Watu wote kwani wamegundua kuwa kama wakianzisha hicho Kinywaji Soko lao linaweza kuwa Kubwa.

Nawapongeza mno na sana Coca Cola kwani kuna uwezekano Wananchi wengi Ulimwenguni tukawa tunachangamka kila mara. Na najua hata wale Wavutaji sasa watahamia katika Soda hii ' Maalum ' ya Bangi / Bange ambapo watakuwa na Uhuru zaidi wa Kuitumia bila Kukamatwa au Kujulikana na ' Mapolisi / Mandata ' ambapo wengi wao watajua kuwa unakunywa tu Soda ya kawaida kumbe ' Mwanamume ' ndiyo Kwanza ' unalanduka ' ila safari hii kwa Kimiminika.

Shikamoo Coca Cola!

Source: CNN na Bloomberg

Nawasilisha.
=======

Kampuni maarufu ya vinywaji ya Coca-Cola ni maarufu zaidi kwa kutengeneza soda, lakini sasa inapanga kufanyia majaribio aina mpya ya kinywaji.

Kinywaji ambacho kitakuwa na bangi. Lakini je, kitalewesha?

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa BNN Bloomberg, kampuni hiyo itashirikiana na kampuni mwenyeji ya kutengeneza bangi kwa jina Aurora Cannabis.

Lengo kuu la kuwa na kinywaji hicho litakuwa ni kupunguza maumivu na si kuwalewesha watu.

Kampuni hiyo bado haijazungumzia hadharani mpango huo lakini imekiri kwamba inafuatilia kwa karibu matukio katika sekta ya vinywaji vyenye bangi.

"Kwa pamoja na wadau wengine wengi katika sekta hii ya vinywaji, tunafuatilia kwa karibu ukuaji wa soko la vinywaji vyenye bangi aina ya cannabidiol visivyolewesha kama kiungo katika vinywaji vya kuboresha afya maeneo mengi duniani," taarifa ya Coca-Cola imesema.

Cannabidiol, ni moja ya viungo vinavyopatikana ndani ya bangi, na inaweza kusaidia kupunguza kuvimba, maumivu na kuganda kwa misuli.

Lakini huwa haiwezi kulewesha.

Hatua ya Coca-Cola inajiri huku Canada ikijiandaa kuyafuata baadhi ya majimbo ya Marekani ambayo majuzi yameidhinishwa matumizi ya bangi kwa sababu za kujiburudisha, baada ya kukubali matumizi ya bangi kwa sababu za kimatibabu kwa miaka mingi.

Hatua hiyo imechangia kuibuka kwa biashara kubwa ya ukuzaji wa bangi, pamoja na kuundwa kwa ushirikiano wa kampuni kubwa katika biashara hiyo.

Mapema mwaka huu, kampuni kubwa ya utengenezaji wa bia ya Molson Coors Brewing ilitangaza kwamba itakuwa ikitengeneza vinywaji vyenye bangi kwa ushirikiano na kampuni ya Hydropothecary, huku kampuni inayotengeneza bia ya Corona, Constellation Brands, ikiwekeza zaidi ya $4bn zaidi katika kampuni ya bangi ya Canopy Growth.

Chanzo; BBC
 
Kampuni ya Vinywaji baridi bora kabisa Duniani ya Coca Cola inafikiria kuja na Soda ' Maalum ' ambayo itakuwa imetawaliwa na ' Mmea ' kamili wa Bangi / Bange ili iweze kuongeza Soko lake kwa Watu wote kwani wamegundua kuwa kama wakianzisha hicho Kinywaji Soko lao linaweza kuwa Kubwa.

Nawapongeza mno na sana Coca Cola kwani kuna uwezekano Wananchi wengi Ulimwenguni tukawa tunachangamka kila mara. Na najua hata wale Wavutaji sasa watahamia katika Soda hii ' Maalum ' ya Bangi / Bange ambapo watakuwa na Uhuru zaidi wa Kuitumia bila Kukamatwa au Kujulikana na ' Mapolisi / Mandata ' ambapo wengi wao watajua kuwa unakunywa tu Soda ya kawaida kumbe ' Mwanamume ' ndiyo Kwanza ' unalanduka ' ila safari hii kwa Kimiminika.

Shikamoo Coca Cola!

Source: CNN

Nawasilisha.
Hiyo msidhani kama itakuwa soda ya kulevya!

Kwani Coca cola inatengenezwa kwa mmea mithili ya bangi, lakini imeondolewa kilevi na watu wa kada zote wana enjoy!

Sasa na hilo la bhangi, itafanywa kinywaji laini kama ilivyo kwa coca cola inayotengenezwa kwa mali ghafi inayotumika kutengenezea madawa ya kulevya.
 
Najua bangi itapanda thamani...zamani kisadolini kilikuwa kinauzwa 50,000/= (hamsini elfu) sijajua kwa hivi sasa itakuwa inauzwa shilingi ngapi
Wito wangu kwa serikali;naiomba serikali iruhusu kilimo cha bangi kama zao la biashara hapa Tanzania!
 
Kampuni ya Vinywaji baridi bora kabisa Duniani ya Coca Cola inafikiria kuja na Soda ' Maalum ' ambayo itakuwa imetawaliwa na ' Mmea ' kamili wa Bangi / Bange ili iweze kuongeza Soko lake kwa Watu wote kwani wamegundua kuwa kama wakianzisha hicho Kinywaji Soko lao linaweza kuwa Kubwa.

Nawapongeza mno na sana Coca Cola kwani kuna uwezekano Wananchi wengi Ulimwenguni tukawa tunachangamka kila mara. Na najua hata wale Wavutaji sasa watahamia katika Soda hii ' Maalum ' ya Bangi / Bange ambapo watakuwa na Uhuru zaidi wa Kuitumia bila Kukamatwa au Kujulikana na ' Mapolisi / Mandata ' ambapo wengi wao watajua kuwa unakunywa tu Soda ya kawaida kumbe ' Mwanamume ' ndiyo Kwanza ' unalanduka ' ila safari hii kwa Kimiminika.

Shikamoo Coca Cola!

Source: CNN

Nawasilisha.

kaka... wataharibuuu.... GANJA inatakiwa ICHOMWE.. na sio iwe katika kiminika.... ahh sinunui
 
Hutonunua Wewe ila kuna Watu sasa wanaanza ' Kudunduliza ' Pesa zao ili ' Kitu ' kikiwa tu rasmi Sokoni waanze Kutiririka na Kuserereka nazo. Yaani itakuwa mjinga mjinga ' akikuzingua ' unakimbilia ' fasta ' kwa Mangi kununua Coca Cola Bangi kisha unamnywea halafu Kichwa kikishachangamka tu unamuanzishia bonge la ' tifutifu '. Kwa hili Kampuni ya Coca Cola naisifu sana na nina uhakika watauza sana na nina uhakika Mikoa kama ya Mara, Arusha na Iringa hizi Coca Cola Bangi zitakuwa zinaishia njiani kwa Kuuzika hata kabla hazijafika mijini.
 
tutaona... bangi ni ya kuchoma tu.. vinginevyo ni Mboga kama matembele
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom