Lisa
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 1,549
- 1,074
POLE SANA KWA KUTOKUVAA SHELA, HALAFU UNANUKA UZINZI, MAANA HUJIFICHI NI JINSI GANI UNAVYOIUZA, Loh!! CHANGU ASIYESIMAMA BARABARANI MKUBWA WEEEEE!!!!!!Hivi kati ya mi na wewe mla makombo yupi? Ngoja nikupe ratiba yake labda utaelewa. Kwanza utaratibu wetu hauna tofauti sana na ndoa nyingine za matala kasoro tu yeye mkiristo. Siku nyingine alala kwangu nyingine kule lakini nyingi kwangu. Sijali kama mwenzangu anakubali ratiba hiyo au anaipenda hiyo ni juu yake. Anapolala kule inakuwa hivi, saa kumi na mbili asubuhi yuko hapa twapata kustaftahi pamoja. Anaacha gari hapa nampeleka ofisini na gari yangu. Halafu naenda kufungua duka namwachia msichana halafu nampigia kujua kama ana kazi nyingi. Kama hana kazi nyingi narudi ofisini kwake kusoma email zangu kuangalia blogs na JF. Tunaenda lunch pamoja tunaagana huko naenda dukani hadi saa kumi. Narudi ofisini kumpitia namsubiria kama kuna mambo hajamaliza. Tunapitia dukani kwangu nafunga hesabu za duka. Tunaenda sehemsehem kupata moja baridi moja moto halafu tunaenda kwangu. Anaoga na kubadili tunakula na maongezi kadha wa kadha na watoto hadi watoto walale tunatumia muda wetu kufurahi saa sita anachukua gari yake anarudi kule. Asubuhi ratiba inaendelea kama mwanzo. Yule anapokuwa kwenye makongamano tunaamua wenyewe tulale kwangu au kwake, kwa raha zetu. Nani mla makombo hapo kwa mawazo yako?
Wewe kama ulivaa shela nishakupongeza tayari, hongera sana. Inakutosha hiyo. Mie shela sijavaa, kweli hilo sidanganyi. Lakini mwanamme ninaye. Wewe kaa na shela yako, ukikumbukia sana kaangalie zile DVD za harusi yako na mapicha kwenye album. Wewe unapofaidi mapicha mi nafaidi kitu cha live huku kwa raha zangu, upo? Na wine zikikupungukia uje dukani kwangu ninazo, tena nitakupa na za ofa.