Watu zaidi ya 400 Kilosa hawatashiriki zoezi la kupiga Kuura

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,493
54,900
Watu zaidi ya 400 waathirika wa mafuriko Mateteni Kilosa hawatashiriki zoezi la kupiga kura.

Zaid ya kaya 100 zenye watu zaidi ya watu 400 walioathirika na mafuriko wanaoishi katika Mahema ya mateteni wilayani kilosa mkoani morogoro wamesema haWawatashiiriki zoezi la kupiga kura kutokana na serikali kushindwa kuwapa makazi ya kudumu huku wakiendelea kuishi maisha magumu kwenye mahema yaliochakaa na wengine kulazimika kulala nje kwa kukosa makazi.

Wakizungumza kwa uchungu waathirika wa mafuriko huku wakionyesha mahema yalivyo chakaa wananchi hao wametupia lawama serikali kushindwa kutimiza ahadi ya kuwapa viwanja vya kujenga makazi mapya baada ya nyumba zao kubomoka kabisa na nyingine kusombwa na maji hali inyosababisha wananchi hao kuishi kwa mateso hasa wanawake na watoto kutokana na upepo mkali huku wakieleza zaidi ya vifo saba vya watoto wachanga vimetoea katika kambi hiyo kutokana na kuugua ugonjwa wa nimonea uliosabaishwa na baridi kali kutokana na watoto kulala nje na mama zao.

Nao viongozi kijiji cha Mateteni wamesema baadhi ya wananchi wamelazimika kurudi katika makazi yao ya awali ingawa si salama kutokana na kuchoshwa na maisha magumu katika kambi hiyo ambapo wamesema waathirika hao wa mafuriko walilazimika kulima vibarua ili kupata fedha za kuwapa viongozi wa kambi kufuatilia ahadi ya viwanja katika ofisi mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya mkoa hadi wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi lakini hadi sasa hakuna majibu ya kupata viwanja ingawa wanazungukwana mashamba pori makubwa ambayo hayajawahi kuendelezwa kwa madai ni ya wawekezaji.

Chanzo: ITV
 
Kweli hizo ndiyo zinaitwa akili za SAMAKI read Hasira ya mkizi furaha ya mvuvi.

Busara ya kawaida tu ingewalekeza hayo wananchi kwenda kupiga kura kwa WINGI kuiondoa hiyo SERIKALI iliyoshindwa kuwatimizia mahitaji yao.

Lakini maajabu ya dunia wao wanasusa kwenda kupiga kura ili waendelee kuishi kwenye mahema!
 
Kuna watu maamuma sana nchini kwetu...

Nawafananisha watu hawa na wale wanaume wanaojinyonga kwa kuwa tu wamekataliwa na.mwanamke...

Yaani wangejua ndio wakati mwafaka wa kuitoa CCM hakika wangepiga kura za hasira ccm watoke, kutopiga kwao kura kutaendeleza kile kile wanachopata sasa
 
Ni wakati sasa kwa wagombea wa Ukawa wa maeneo hayo kujaribu kuwafikia haraka hao watu na kuwashawishi hizo kura wazihamishie upinzani...

Yaani wangejua ndio wakati mwafaka wa kuitoa CCM hakika wangepiga kura za hasira ccm watoke, kutopiga kwao kura kutaendeleza kile kile wanachopata sasa
 
Si wamchague Lowasa



Hapana! Nimependa namna walivyowakilisha tatizo Lao! Hivi unadhani wangewaita ITV nakusema watampigia Kura Lowassa coz Serikali ya ccm imeshindwa kuwajengea nyumba Kama ilivyoahidi hao ITV wangeirusha hiyo habari? Hivi ndo ujumbe umefika Na ukweli Ni kuwa watampigia Lowassa!
 
Back
Top Bottom