Watu wengi wanamuabudu Mungu wa uongo hapa duniani

Ukweli wa hizi imani bado ni kitendawili, siku za usoni itatokea imani ambayo iko nje, kabisa na mfumo wa Uislamu na ukristo. Na hii imani itakuwa na nguvu. Dini zote zitapotea za siku hizi. Na itabaki historia tu . Na mimi kunasiku nitatoa uzi hapa kwa kifafanua:?
 
Biblia na quraani ndio uongo kwa sababu zinagaiwa bure ila hayo maarifa hapo juu nimelipia.
akili ndogo bhaaana hayaa, ukilipia wakati mwingine ujue kutofautisha vitabu au machapisho yaliyoandikwa kwa ajili ya simulizi za kusisimua na machapisho yaliyoandikwa kwa ajili ya simulizi za kweli.
 
Well, mpaka sasa nakiri ukuu wake,amenitendea mambo makuu, ameniinulia uso wake na kunifadhili,amenisamehe dhambi zangu ingali zilikua mbaya. Nitamuhimidi na kumsifu siku zote za maisha yangu.
how sure umesamehewa dhambi zako?
amekwambia kuwa kakusamehe, ama ubongo wako umehic kuwa umesamehewa....??
 
Kwanini Mungu apige story na shetani ili wamtese mwanadamu... Wakati huo huo Mungu anatuambia tumchukie shetani ni mtu mbaya... Wao wanapiga story ni marafiki wanashirikiana kwenye mambo flani flani

Alafu ugomvi wao sie unatuhusu nini kwanini watuingize kwenye ugomvi wao ambao sisi hatukuwepo

Pia anao muda na uwezo wa kumuuwa shetani ili mabaya yasiwepo zaidi wanapiga story tuu na kunywa kahawa pamoja.. kwanini hii
aisee nimecheka kifala sana...
itakuwa walikuwa wanapiga story za kumshughulikia ayubu pale karume huku wanakula kashata na gahawa....
 
Simple sana, kuna ile furaha na amani unayoipata moyoni (rohoni) ailezeki. Ni zaidi ya ile ya kupendwa na pisi kali.
mbona kama ni ideology ileile ya mungu mkuu ni moyo wako plus mind yako...
Ni vile maybe hujui namna nyingine ya kukupa furaha na aman moyon mwako,so mind yako ikakuambia pita hivi utajisikia amani...
 
Mkuu, una uhuru wa kufanya uamuzi, ndiyo maana binadamu amepewa utashi wa kutambua lililo jema na baya. Haijalishi nini ambacho unakiamini, lakini kinachojalisha ni uhakika wa kile ulichokipokea kama imani.

Uhakika wa chanzo cha uhakika cha habari ni jambo la msingi sana. Kwa hicho ndicho humfanya mtu akajengeka kiimani.

Toka awali Mungu ni roho, na hakuna mtu aliyewahi kumuona kwa macho ya kawaida ya kibinadamu. Ili siri za ufalme wake na uhakika wa uwepo wake ndiyo sababu kuu ya kuzaliwa hapa duniani kwa Yesu Kristo.

Na Yesu huyu aliyezaliwa kama mwanadamu, alikuwa ni chapa halisi ya nafsi ya Mungu mwenyewe (rejea Waebrania 1:1-4). Na hapo basi ndipo haswa ulipo msingi yule anayemuamini.

Lakini, nukuu hapa chini ya kile ulichokiandika kinanipa usumbufu akilini mwangu, yaani ulipoandika;

"Mimi ni black sheep kwenye familia yangu, nina miaka zaidi ya kumi sijawahi kuwa na mawasiliano na baba na mama yangu tumekata undugu kwa sababu imani yao"

Mkuu, kama ikikupendeza jaribu kutafuta maarifa ya upendo kutoka katika maandiko matakatifu, ijapokuwa inaonyesha wazi huoni thamani yoyote ile juu yake. Lakini japo kwa mfupi tafakari vifungu vifuatavyo;

1) KUTOKA 20

12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

2) 1 WAKORINTHO 13

1Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.

Kwa hiyo mkuu, upendo wa kweli hujengeka katika imani ya kweli na yenye kuthibitika. Kinyume cha hapo itakuwa ni mapokeo ya uongo.
so sie wengine wote tunaenda motoni enhh couz sio follower wa yesu enhh....
 
Mungu wa Israel, Mungu muumbaji wa Nchi na Ardhi, uliyeviumba hata visivyoonekana kwa macho,

Mzee wa Zamani, Uliyekuwepo, Uliyepo na utakayekuwepo .


Msamehe huyu Kiumbe kiazi, aliyetumia muda wake mwingi KUSOMA mavitabu ya wanadamu ili aje na mautumbo kama haya !!.
mungu wa israel enhhh....
atakuwa mbaguzi sana huyu...
 
Kwanini utumie maneno ya "Mungu wa kweli" na usiseme tu Mungu unayemuamini wewe? Kwanini isiwe kila mtu/watu wanaamini mungu wao na hakuna mungu wa uongo?

Kwa sababu anachoamini mwenzako(mungu) ni tofauti na unachoamini wewe(mungu) hivyo sioni sababu ya kumwambia mwenzako anaamini mungu wa uongo hali ya kuwa wote mnaamini tu kila mtu kashawishika kivyake kuamini hicho anachoamini na wote hamuwezi kuthibitisha zaidi ya imani tu.
pure logic...
 
The best in this world are free. Hata oxygen unayo vuta ni free. Even the life that u have borrowed was given unto you for free u never paid a dime. So Kwa hoja yako hii Biblia Na Qur'aan ndio VITABU Bora kuliko hivyo ulivyo soma.

Unless otherwise useme hata oxygen haina maana Kwa Sababu u get it for free
hakuna cha bure broooo....
hiyo oxygen unailipia kwa kufanya yale aliyokupa hiyo oxgen kakauelekeza...
utachomwa moto buloo we haya tu na haya ndiyo malipo ya ile oxgen uliyoiita free...
life pia sio free couz umepewa time without contract na kuamrishwa kufanya mambo kadhaa,time ikiisha usipofanya malipo ya huo mda ni motoni milele...
 
Vitu vya maana kwa binadamu kwa Mungu ni sawa na mavi na kinyume chake..!

Sikia wewe mtoto mpotevu maarifa ya Mungu hayauzwi maana Mungu hajaumba hicho kinaitwa pesa maana angeumba pesa wote tungekuwa nazo. Zingatia maarifa ya Mungu huyatoa bure kwa wanaostahiri au kwa makusudi maalumu mfano manabii wanapewa ufunuo (revelation) purposeful au Mungu anaweza mjalia mtu yeyote maarifa yake kwa kazi maalum.

Kiufupi sisi MUNGU WA KWELI kwanza achunguziki kama unavyojinasibu kumjua maana yeye anajua ata tuyawazo si kama unavyomwelezea kana kwamba ni sawa na binadam hao unaosema wana UUNGU.
ndo maana yanakuwa editable mara kwa mara couz hayana hakimiliki...
 
Mimi kama chawa wa Mungu, naleta maswali yapatikanayo kwenye kitabu cha Ayubu 33 : 1 - 2, wafia shetani msaidie kujibu baadhi ya maswali hayo, mkishindwa kawaulizeni chawa wa shetani waliowaandikia huo utafiti wenu.

1 Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
2 Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa?
3 Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie.
4 Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.
5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?
6 Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
7 Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
8 Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni.
9 Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,
10 Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango,
11 Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa?
12 Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?
Unapompa maandiko ni ya nini ilihali anachomaanisha yeye ni sawa na haya maandiko yaliwekwa kwa sababu ya manufaa ya watu na si huyo MUNGU.
 
You sound like Joel Osteen.

Mungu yupo na jehanamu ipo, Acha kupotosha watu kwa nadharia ulizozitoa vitabuni.

Acha nimwamini Mungu nikamkose.
Lete ushahidi acha porojo ulizo mezeshwa na watu, mwenzio katoa mada yenye viashiria vinavyo fikirisha kibinadamu ili ujiulize na Kuna kitu unakiona, wewe unakuja na maneno mepesi, toa ushahidi wa unachokiamini, japo kumthibitisha MUNGU uone kama hutashindwa, ili umthibitishe Kwa kitu kinachoonekana na kufikirisha,tutakuta MUNGU ni wazazi wako
 
Lete ushahidi acha porojo ulizo mezeshwa na watu, mwenzio katoa mada yenye viashiria vinavyo fikirisha kibinadamu ili ujiulize na Kuna kitu unakiona, wewe unakuja na maneno mepesi, toa ushahidi wa unachokiamini, japo kumthibitisha MUNGU uone kama hutashindwa, ili umthibitishe Kwa kitu kinachoonekana na kufikirisha,tutakuta MUNGU ni wazazi wako
Bro nikishindwa kukuthibitia haimaanishi Mungu hayupo
 
Bro nikishindwa kukuthibitia haimaanishi Mungu hayupo
Huna la msingi man...
Mimi ni muumini wa unacho amini, lakini nikionaga mtu anayejifanya anajua jambo na kumbe hajui namdharau sana, ni bora kunyamaza
 
Back
Top Bottom