Mkuu Mnyinda,unachokisema ni sahihi saana,mfano mzuri angalia kinachotokea Mtwara sasa.Kuna post moja nimetoka kuisoma sasa hv kwenye uzi mmoja anasema" mtu mjinga akigundua kua unamuibia halafu akacharuka,hua ni hatari kuliko mkorofi"
Tatizo Polisi wanawazuia...wachome na hospitali basi
[FONT=courier
new]Kwani Dr. Slaa amesemaje mpaka sasa....mwenye kujua
atujuze. Namshauri pia awatulize wananchi wake wa
Mtwara[/FONT]
kuna taarifa katika fb kuwa nyumba ya mwandishi wa TBC mikongoro inachomwa moto muda huu!
Duuh, wamakonde ni nouma aisee? Kumbe muungwana akigundua una muonea kwa sababu ya uungwana wake ni hatari kuliko mkorofi!
kuna gari ya wanajeshi kutoka nachingwea kuja mtwara kusaidia imepata ajali mbaya njia yaani wameumia hata kabla haijafika
Nchi hii inapoelekea kitanuka balaaaa
Tamko la serikali lipo wazi kwamba Bomba la Gesi Ntwara hadi dar linajengwa kwa gharama yoyote: no changes; ila tu watapeleka askari wengi kudhibiti mgomo wa wana mtwara wakidhani hilo ndilo suruhisho..
Nimeeleza kwa ufasaha sana ni kwanini kuna uharaka wa kusafirisha gesi sasa. "Eti tusubiri miaka kumi hadi tutakapopata uwezo wa kujenga PowerPlant Mtwara, ilihali uwezo wa kusafirisha sasa hiyo gesi tunao. Kwanini tusiokoe uchumi unaodidimia kutokana na ukosefu wa umeme, kwa kuamua kusafirisha hiyo gesi ili iokoe hali ya mambo iliyopo nchini hivi sasa?
Kuhusu swali lako la pili, kama tatizo ni mikataba, basi iwekwe wazi kwamba kinachogomewa ni mkataba. Ni ukweli ulio dhahiri ambao pia umedhihirisha na Dr F. Ndugulile kwamba gharama za ujenzi wa hili bomba ni mara nne ya gharama halisi.
Tatizo tulilonalo ni la hawa wabunge wa CCM kama akina Ndugulile, wanajua matatizo yaliyopo, lakini mbunge wa upinzani akisimama kutoa hoja kama hiyo.
Sasa we una tofauti gani na CCM, Ukweli wote unaujua, halaf unapinga wanachofanya Wanamtwara.
nchi hii ina mengi ya kutufunza,na huko tuendako ni kubaya zaidi,wewe jiulize kama serikali hii inavyo jiita kila siku ni serikali sikivu,kwanini wanafanya mambo yao kwa uficho,usiri mkubwa tatizo hapo ni nini?wamakonde bwana ogopa,ata vita vya MAJIMAJI VILIANZIA HUKOHUKO MTWARA,kazi wanayo magamba