Watu wa mikoani wakifika Dar ni wasumbufu sana wanataka kufika kila sehemu

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,667
Wanadsm tulivyo bize unapokea wageni wanataka kufika kila eneo la Dar es Salaam hii inakera sana.

Nina jamaa zangu wametoka mikoani wanataka kufika kila sehemu wanazozisikia kwenye media juzi walikomaa niwapeleke Uwanja wa Taifa wanaone match ya watani nikoana sio ishu nikawapelea japo mimi na miaka yote hapa mjini nilikwenda mitaa hiyo kikazi hasa kipindi cha sikuu za kitaifa.

Hapa wanataka kufika Daraja la Tanzanite, Daraja la Mkapa, Serena, Kawe kwa Mwamposa, Jangwani Sea Breeze, Karume, Kkoo, Kigamboni, Chamazi Complex, Mlimani City, UDSM, Kitambaa Cheupe yaani wamekuja na list utadhani mimi sina majukumu.

Nimejaribu kuwaambia wasubiri nikiwa off ila wanamunkari balaa, kumbe huwa wanaona tunafaidi wakati sisi Wanadsm hizo sehemu huwa tunakwenda kwa mambo ya msingi sio kuzurura ovyo.

Uliwahi kukumbana na mgeni kutoka mkoani anaona Dar es Salaam ni kimtaa kimoja hivi, uchome mafuta tu.

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_20230417_180907.jpg
 
Back
Top Bottom