WATU Sita Wamepandishwa Kizimbani Mjini Singida, Kujibu Shitaka La Mauaji

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7


Mwita Waita (wa kwanza kushoto), akifurahi na wafuasi wa CHADEMA mahakamani mjini Singida, baada ya kupata dhamana ktk kesi ya mauaji.
Na: Elisante John.


Julai 16,2012.
WATU sita wamepandishwa kizimbani Mjini Singida, kujibu shitaka la mauaji ya Mwenyekiti UV-CCM Kata ya Ndago Wilaya Iramba,Yohana Mpinga, katika vurugu zilizohusisha wafuasi wa CHADEMA na CCM.
Wamesomewa shitaka hilo na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Neema Mwanda mbele ya hakimu mfawidhi mahakama ya Mkoa Singida, RuthMassam.
Walioshitakiwa ni Manase Daudi (40), Williamu Elia (33), Frank Stanley (20), Charles Leonard (36), Tito Nintwa na Fillipo Edward (30), wakazi wa Ndago, Wilaya Iramba.

Wamedaiwa kufanya kosa hilo Julai 14, 2012 saa kumi alasiri, katika kijiji cha Nguvumali, kwa kutumia mawe na fimbo.

Hawakutakiwa kujibu lolote, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo na itatajwa tena Julai 30, 2012.

Pia kesi nyingine iliyosomwa na mwanasheria wa Serikali Seif Ahmad, imemhusisha afisa sera na utafiti wa CHADEMA makao makuu Waitara Mwita (37) mkazi wa jijini Dar-es-salaam, akidaiwa kutoa lugha ya matusi mkutanoni.

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA http://moses-ayoub.blogspot.com/2012/07/watu-sita-wamepandishwa-kizimbani-mjini_16.html
 
Mambo haya yasingekuwa yanatokea iwapo watu wote tungekuwa na ustaarabu wa kuheshimu mikutano ya wenzetu. Tunapojenga utamaduni wa kufanya fujo katika mikutano ya wenzetu ndipo tunatengeza mazingira ya kudhuriana, na hilo ni jambo baya sana kwa amani tunayojidai kuwa nayo. Waliofanya fujo kwenye mkutano halali wa chama cha wapinzania wao nao wanatakiwa wahojiwe, na huenda pia washitakiwa kwa kuhatarisha maisha yao wenywe na maisha ya marehemu. yaani kesi hii iwahusishe pande zote mbili za ugomvi.
 
Si nilisoma jana hapa wanasema mnyika na dr mkumbo wangepandishwa nao kizimbani...hahaaa wajaribu waone kama ingekiwa rahisi...jk iliambiwa nchi haitatawalika ndo hivi sasa..pole mwanakwetu miaka mitatu iliyobaki ni kama karne hivi....
 
Back
Top Bottom