Watu Muhimu katika Historia ya Nchi yetu

Hivi kwa nini watu mnakuwa wasaahulifu hivi na hata hamna logic!! nimesikia hotuba mbili tofauti ambazo Mwl JKNyerere anamtaja Mzee Tambaza na watu wengine, lakini kama hiyo haitoshi pana shule inaitwa Tambaza kwa kumbukumbu ya huyu mzee,na pia pana uwanja wa sheik Amani ambao unasema siyo kwaheshima ya Karume bali ni Amani mwingine, DSM kuna mtaa wa Kibasila, Migeyo, Shaban robert, Shekilango jamani haya yote ni majina yalipewa miaka hiyo ili iwe kumbukumbu kwetu, Nyerere mlitaka aanza kuandika maisha ya hawa watu kama yeye!!! kama aliruhusu mitaa na monument zingine zikaitwa kwa mjina ya hawa watu ebu nasi tufanye homework kidogo tujue who was who na kwa nini and then publish hicho kitabu na uone kama kuna mtu atakushitaki!! lakini katika hili wacha kumsema vibaya mzee wa watu, angetaka ajulikane peke yake angekwiba na kujitengenezea utajiri wa ajabu, lakini kaishi kwa uadilifu mkubwa akirinda mali za watanzania wote tena wakati hule hata wakuzijua mali alikuwa wapi!! ebu acheni hizo mpe heshima yake!!
Mungu ibariki Tanzania.
 
Mimi labda niulize, kwa nini nyerere asingeanza harakati za kugombea uhuru akiwa kule kule kwao hadi akaja kuutafutia huku pwani? Je alipokuja huku alikuta harakati za kutafuta uhuru zilianza au yeye ndio alizianzisha?
 
Halafu historia ya african association nayo imefutwa,pamoja na historia ya taa,yeye nyerere alijiunga na taa akiwa tabora school,lakini watoto wanafundishwa kuwa alikuja kuuanzisha tanu,wakati tanu ndio taa.


mmmh
 
Mimi labda niulize, kwa nini nyerere asingeanza harakati za kugombea uhuru akiwa kule kule kwao hadi akaja kuutafutia huku pwani? Je alipokuja huku alikuta harakati za kutafuta uhuru zilianza au yeye ndio alizianzisha?

labda huko mkwao kulikuwa hakuna mwamko ndo maana aliamua kuondoka kwao na kutafuta suport ya watu wengi ..kidole kimoja hakiuwi chawa
 
Kwa kweli kama historia ilibadilishwa kwa nia ya kuwafunika baadhi wa washiriki wa harakati za uhuru na mapinduzi.. basi kuna haja ya historia hiyo kuangaliwa upya.. otherwise ni batili especially pale tunapomkubali mtu mmoja ambaye bila the rest asingefanya kitu..
 
Historia ya Tanzania haitamsahau
1. Seif Shariff Hamad na CUF kwa kuleta mapinduzi pemba (CCMchini) na kupigania demokrasia nchini hasa zenj
2. Prof. Kighoma Malima kwa introduce mtindo wa kutumia number kwenye mtihani wa darasa la saba mwaka 1987 alipokuwa waziri elimu badala ya kutumia majina..matokeo yake vijana wengi wa kiislamu walifaulu ikawa noma kwa wenye chuki (wakatoliki)
3. Baba yangu kwa kupinga siasa ya ujamaa vijijini mahakamani alishinda baada ya miaka 30 (thanks to muungwana mwinyi)
4. Ally Hassan Mwinyi kwa kutuletea TV, shule binafsi, sijui maisha yangekuwaje bila wewe Mwinyi tungebaki na wenye chuki na wachoyo
 
Historia ya Tanzania haitamsahau
1. Seif Shariff Hamad na CUF kwa kuleta mapinduzi pemba (CCMchini) na kupigania demokrasia nchini hasa zenj
2. Prof. Kighoma Malima kwa introduce mtindo wa kutumia number kwenye mtihani wa darasa la saba mwaka 1987 alipokuwa waziri elimu badala ya kutumia majina..matokeo yake vijana wengi wa kiislamu walifaulu ikawa noma kwa wenye chuki (wakatoliki)
3. Baba yangu kwa kupinga siasa ya ujamaa vijijini mahakamani alishinda baada ya miaka 30 (thanks to muungwana mwinyi)
4. Ally Hassan Mwinyi kwa kutuletea TV, shule binafsi, sijui maisha yangekuwaje bila wewe Mwinyi tungebaki na wenye chuki na wachoyo

baba yako ni nani mkuu?
 
very interesting thrend..
safi sana Mkandara,
umenikumbusha wazee wa Mbeya, Mzee Ambukege Joab Kakuyu, Mwambije, Mwaisoloka, Mwakitalima, Mwangoka,Nachirwa,na wengine wengi waliofight enzi hizo kwa ajili ya uhuru wetu leo ambao watu wachahche wamekuwa wakiutumia vibaya kwa kugawa bure mabenki yetu, maliasili zetu na utajiri wetu wote kwa wakoloni wanaojiita wawekezaji.
Tanzania imekuwa nchi ya asali na maziwa kwa wageni, wazawa tunaishi bado utumwani Misri
 
Nakumbuka kuna makaburi ya mashujaa pale Upanga... Hivi ni viongozi/mashujaa gani waliozikwa hapo?
 
Mkandara said:
Nakumbuka kuna makaburi ya mashujaa pale Upanga... Hivi ni viongozi/mashujaa gani waliozikwa hapo?

Mkandara,

..inawezekana unazungumzia makaburi ya askari wa Uingereza waliopigana vitaa kuu ya kwanza.
 
very interesting thrend..
safi sana Mkandara,
umenikumbusha wazee wa Mbeya, Mzee Ambukege Joab Kakuyu, Mwambije, Mwaisoloka, Mwakitalima, Mwangoka,Nachirwa,na wengine wengi waliofight enzi hizo kwa ajili ya uhuru wetu leo ambao watu wachahche wamekuwa wakiutumia vibaya kwa kugawa bure mabenki yetu, maliasili zetu na utajiri wetu wote kwa wakoloni wanaojiita wawekezaji.
Tanzania imekuwa nchi ya asali na maziwa kwa wageni, wazawa tunaishi bado utumwani Misri

Wageni wana matatizo yao, lakini bila ya ujio wa wageni wengi situngekuwa bado tunavaa magome ya miti?

Wageni wanatuibia na kutupa ujanja.
 
watu muhimu walikuwa waswahili waliomvalisha Nyerere kaptula na siku uhuru waliachwa chini huku kule juu aliwachukua akina Kambona na wagala wenzie the rest is history

sasa mnaona woga gani kulisema hilo?

Tatizo lako GT unawaona waswahili wenzio tu wengine huwaoni!!Umewahi kumsikia Mzee Edward Mwangosi na mchango wake wa kugombea UHURU toka enzi za TAA kule Dodoma; Mzee John Rupia unamuweka kwenye genge la waswahili?. Haya mambo hayakuanzia Dar kudai uhuru kijana; soma historia.
 
Imeandikwa na Na Kanaeli Kaale; Tarehe: 10th October 2009 Habari Leo


mail


"MIMI ndiye Mwalimu wa Mwalimu Nyerere….bado ni ngali hai…na ninaweza kueleza kwa kifupi niliyojifunza kutoka kwa Mwalimu Nyerere," ndivyo anavyoanza kujibu maswali kuhusu maisha nyake Mwalimu James Irenge.

Irenge ambaye umri wake unakisiwa kuwa ni zaidi ya miaka 100, ni miongoni mwa walimu tisa wa Shule ya Msingi Mwisenge aliyosoma hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Shule hiyo ilikuwa ya bweni mahsusi kwa watoto wa machifu na watemi. Irenge anasema kuwa Nyerere alianza darasa la kwanza katika shule hiyo 1934.

Kwa kuwa alikuwa na upeo wa juu alifanikiwa kusoma madarasa manne kwa miaka mitatu na hivyo mwaka 1937, alihamia shule nyingine ya watoto wa machifu na watemi iliyopo Tabora na kuendelea darasa la tano au maarufu kwa jina la middle school kwa wakati huo.

Irenge ambaye anapenda kujiita "Mwalimu wa Mwalimu" anasema wakati Nyerere akiwa mwanafunzi wa darasa la tatu, alikuwa na busara na upeo wa hali ya juu na alipenda kuuliza maswali mengi yaliyohitaji majibu ya kina.

Ingawa alimfundisha Nyerere takribani miaka 75 iliyopita, anasema bado anamkumbuka vizuri kwa sababu alikuwa mwanafunzi mwenye busara na kipaji cha pekee.

Anasema kuwa Nyerere alikuwa tayari kupokea maoni ya watu wengine na kukubali ushauri wa walimu wake juu ya harakati za kuwania ukombozi wa nchi ya Tanganyika kutoka mikononi mwa wakoloni.

Irenge alijifunza kuwa Nyerere alikuwa kijana mwenye uwezo wa kufikiri kwa makini kabla ya kutenda lolote, mwenye kusema ukweli mtupu bila wasiwasi wala kutishika na lolote.

Pia katika maisha yake aligundua kuwa Nyerere alikuwa kijana mwenye kusikiliza mafundisho ya darasani au kutoka kwa mtu mwenye akili pia alikuwa na akili za kuzaliwa toka tumboni mwa mama yake mzazi.

Irenge anaishi katika Kijiji cha Mwisenge, mita chache kutoka ilipo Shule ya Msingi ya Mwisenge hata hivyo kutokana na hali ya uzee, hawezi kutoka nje ya nyumba yake bila msaada. Hivi sasa hasumbuliwi na maradhi lakini hali ya uzee imesababisha atumie muda mwingi akiwa amejilaza kitandani.

"Mimi siumwi ila nimechoka kutokana na hali yangu ya uzee. Nimezeeka kweli kweli …Nyerere alikuwa mwanafunzi wangu wa darasa la tatu…. akashika madaraka na kulitumikia Taifa kwa muda. "Alifariki akiwa mzee na sasa tunazungumzia miaka 10 baada ya kifo chake lakini mimi Mwalimu wake bado ningali hai," anasema Irenge.

Anaendelea kusema, "hivyo naomba Watanzania na wasamaria wema waelewe kuwa mimi Mwalimu wa Mwalimu Nyerere bado ningali hai na kama ikiwezekana basi wanisaidie maana ninaishi katika hali ya mateso sina fedha za kujikimu."

Hivi sasa Irenge ni mzee asiyejiweza kwani hawezi kujihudumia mwenyewe. Anasaidiwa na mke wake, Josephine Irenge mwenye umri wa miaka 70.

Maisha ya Irenge ni changamoto kwa wanaharakati wanaotetea haki na maslahi ya wazee. Alistaafu kazi mwaka 1969 na anadai kuwa amelipwa pensheni ya Sh 400 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka 40.

"Mimi nilikuwa mtumishi wa umma. Nilistaafu mwaka 1969 na kulipwa pensheni ya Sh 400 tu kwa mwaka. Nasikia wamebadilisha mwezi wa sita mwaka huu na sasa watanilipa Sh 20,000 kila baada ya miezi sita yaani 40,000 kwa mwaka," anasema kwa huzuni. Anasema kwa maisha ya sasa ni vigumu kuishi kwa kutegemea Sh 20,000 kila baada ya miezi sita.

Anaiomba serikali imlipe malipo yanayoendana na gharama halisi za maisha kwa kuzingatia kuwa wazee wanahitaji lishe bora na matibabu ya uhakika. Malipo ya pensheni yamekuwa kero kubwa kwa mzee huyo. Gharama ya kutoka Musoma hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia malipo hayo ya pensheni ni kubwa ikilinganishwa na malipo hayo.

Mmoja wa watoto wa mzee huyo, Musa Irenge anasema baadhi ya watumishi waliopewa dhamana ya kutoa malipo ya pensheni wanatumia lugha mbaya na kuwatukana wazee pasipo sababu ya msingi.

Anasema, baada ya baba yake kulalamikia malipo hayo kwa muda mrefu, yeye aliamua kufunga safari kwenda Dar es Salaam kuelezea hali halisi.

Anasema alikutana na ofisa mmoja na kumpa faili na alipoliangalia, alihamaki na kusema kwa lugha ya Kiingereza, " he supposed to be died!" "Yaani alimaanisha kuwa baba yangu hakupaswa kuwa duniani….hivi kisheria Mtanzania anapaswa kuishi miaka mingapi? Watendaji wanaokerwa na umri mkubwa wa wazee wanafanya nini huko Hazina?" Musa analalamika.

Mzee Irenge anawaasa watumishi wa Hazina wanaotukana wazee kuacha tabia hiyo kwa kuwa hakuna mtu mwenye uwezo wa kujipangia umri wa kuishi. Anaiomba serikali kuwafundisha watumishi wa kitengo kinachoshughulikia pensheni umuhimu wa huduma bora kwa wateja ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha watumishi wazembe na wanaotukana wazee kwa lengo la kukwepa majukumu yao.

Ingawa Irenge ni mzee, bado anakabiliwa na majukumu ya kuitunza familia yake kama mkuu wa kaya. Baadhi ya watoto na wajukuu wanamtegemea kutokana na ukosefu wa ajira hususani kwa vijana.

Hata hivyo hana uwezo wa kufanya kazi na anasema malipo finyu yanamlazimu kuwa ombaomba. Kero yake ya pili ni kuhusu viongozi wanaompa zawadi za mablanketi wakati shida yake ni chakula na fedha za kujikimu.

"Wakiniita kunipongeza wananipa mablanketi, wenzangu wanapewa fedha. Jamani naomba wanifikirie, hivi njaa inaweza kusitiriwa na blanketi?...nipeni chakula jamani," anasihi.

Mzee Irenge anaelezea hofu yake kuhusu sera za utandawazi na ubinafsishaji. Anasema viongozi wasipokuwa makini katika masuala ya utandawazi na ubinafsishaji wanaweza kulirudisha Taifa kwenye hali ya kutawaliwa na wageni.

Anasema kuwa baada ya Uhuru baadhi ya Wazungu walitaka kuendelea kujichumia mali kwa kutumia rasilimali za Taifa lakini Nyerere aliwadhibiti kwa kutumia Azimio la Arusha.

"Naomba viongozi wawe makini na wageni wenye urafiki wa mashaka….waepuke kuuza kiholela rasilimali za nchi kwa sababu hata wakoloni walianza kwa kushika rasilimali muhimu kisha wakatawala," anasema.

"Linalotoka kinywani mwangu ni moja…kuweni macho na marafiki wa kigeni kwani wana hila, watajifanya wanatoa misaada kumbe wanachota mali na rasilimali za nchi na kuwaacha na umasikini wenu…naomba mzingatie neno hili," anasisitiza.

Akizungumzia juu ya maisha yake, Irenge anasema alifanikiwa kuwa mwalimu kwa kuwa alikuwa mtoto mwenye kipaji cha hali ya juu na baba yake mdogo alikuwa Chifu wa Wazanaki.

Aliingia shule kwa kutumia jina la baba yake mdogo kwa kuwa wakati wa utawala wa mkoloni haikuwa rahisi kwa mtoto wa masikini kupata elimu.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyopo katika rasimu ya kitabu chake cha Maisha na Sifa za Viongozi wa Tanzania Kabla na Baada ya Uhuru, Irenge alijiunga na Shule ya Msingi Mwisenge mwaka 1928.

Akiwa shuleni alizingatia masomo na kuonesha utii kwa wanafunzi na unyenyekevu kwa walimu, wake na watoto wa walimu hali iliyomuwezesha kuchaguliwa kuwa kiongozi wa wanafunzi.

Anasema unyenyekevu huo uliwafanya walimu wamfananishe na baba mzazi anavyopokea kondoo wake aliyepotea kama ilivyoandikwa katika Bibilia kitabu cha Mathayo 18:10 na Luka 15:3-7.

Irenge alifanikiwa kuhitimu darasa la nne Oktoba mwaka 1931 baada ya kufaulu mtihani mgumu na kushika nafasi ya kwanza miongoni mwa wanafunzi wote wa jimbo la Mwanza. Mtihani huo ulitungwa katika Shule ya Bwiru Mwanza na wanafunzi walisema ulikuwa mgumu sana.

Swali mojawapo la somo la hisabati liliuliza, mashimo 3 kila moja lina panya 3 na kila panya amezaa panya 3. Je, panya wote ni wangapi jumla? Anasema hata baadhi ya walimu walibabaika kwani wengine walisema ni panya 18, wengine 27 pia wapo waliosema jumla ya panya ni 36.

Anasema kwa kuwa watoto walioruhusiwa kusoma ni watoto wa viongozi pekee , alichaguliwa kuendelea na masomo ya ualimu kwa niaba ya baba yake mdogo, Chifu Ihunyo Monge wa Zanakiwa. Mwishoni mwa mwaka 1931 alijiunga na Chuo cha Ualimu Mpwapwa. Aliingia chuoni akiwa anatumia jina la asili la Zangara Irenge.

Mwaka 1933 alibatizwa na Kanisa la Anglikana na kuitwa James. Hivyo kuanzia wakati huo akabadili jina na kuitwa James Irenge. Baada ya kuhitimu chuo mwaka 1934 na kufaulu vizuri, alipewa nafasi ya kuwa mwalimu wa walimu katika Chuo cha Mpwapwa kisha akasajiliwa kuwa mtumishi wa serikali wa Wizara ya Elimu.

Alifanya kazi hiyo kwa mwaka mmoja kisha akahamia katika Shule ya Msingi Mwisenge kwa ajili ya kufundisha watoto wa watemi na watawala wa Serikali ya Halmashauri ya Mitaa Musoma.

Anasema kwa kuwa alikuwa ameajiriwa na Serikali Kuu haikuwa rahisi kupata uhamisho lakini taratibu zilizingatiwa na akahamia kwenye shule hiyo kama mwalimu wa kuazima. Kwa hiyo mwaka 1936 alifanya kazi chini ya mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kufundisha Shule ya Mwisenge lakini akaendelea kulipwa na Serikali Kuu.

Kwa mujibu wa cheti cha Ualimu cha Irenge, alizaliwa mwaka 1915. Hata hivyo mke wake anasema Irenge anakisiwa kuwa na miaka zaidi ya 100 kwa kuwa alichelewa kuanza shule. Inasemekana kuwa wakati wa ujana, Irenge alipendelea kuwa na ndoa ya mke mmoja na alioa mwaka 1927.

Hata hivyo alilazimika kuoa mke wa pili baada ya kukaa na mke wake wa kwanza kwa miaka 30 bila kupata mtoto. Mke wake wa pili alifanikiwa kupata watoto wawili kabla ya kukosana na kurudi kwao.

Hata hivyo Irenge alijizatiti kukabiliana na changamoto za maisha. Mwaka 1952 akaoa mke mwingine ambaye amebahatika kuzaa watoto 10 na wanaishi pamoja hadi sasa.

Hivyo Irenge alipata jumla ya watoto 12 na walio hai ni 11. Mwaka 2002 Irenge na mkewe Josephine waliadhimisha kumbukumbu ya miaka 50 ya ndoa.

Wakati wa ujana wake Irenge alipenda michezo mbalimbali, kuongoza wenzake, kusoma na kuandika vitabu. Ingawa hakufanikiwa kuchapisha vitabu vyake bado ana ndoto ya kuchapisha kitabu chake cha "Maisha na Sifa za Viongozi wa Tanzania Kabla na Baada ya Uhuru."
Irenge ametumia baadhi ya taarifa zilizomo katika kitabu hicho kuwaasa viongozi waliopo madarakani.

Kwa habari zaidi soma toleo maalumu la kumbukumbu za kifo cha Mwalimu Nyerere kwenye HabariLeo Jumatano ijayo.
 
nauliza wana jf kuna makaburi yako mkabala na international school of tanganyika upanga nadhan primary ni barabarani yanatazamana na mjengo mpya mrefu , kwa sasa naona kuna kama pamezungushiwa uzio hivi , je ni makaburi ya watu gani? na pashauzwa nini?
 
nauliza wana jf kuna makaburi yako mkabala na international school of tanganyika upanga nadhan primary ni barabarani yanatazamana na mjengo mpya mrefu , kwa sasa naona kuna kama pamezungushiwa uzio hivi , je ni makaburi ya watu gani? na pashauzwa nini?
As kids i remember even mucking around these graves-me is also so eager to know who these graves were for
 
Marehemu Prof. Justinian Ferdinand Rweyemamu, mchumi

[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Justinian_Rweyemamu[/ame]


Aliwahi kuwa Dean wa Faculty of Science
Katibu mkuu wa wizara ya Uchumi na Mipango
Mshauri mkuu wa Raisi kuhusu masuala ya uchumi
Member of the secretariat, Committee for Development planning, the UN.
etc

PhD thesis yake iliyozaa kitabu cha "Underdevelopment and Industrialization in Tanzania: A Study of Perverse Capitalist Development" (Nairobi: Oxford University Press, 1973) ni maandiko muhimu kuhusu historia ya uchumi wa nchi yetu. Humo anatoa analysis ya uchumi tegemezi tuliokuwa nao kipindi hicho na tulio nao mpaka sasa.


Moja ya insha yake....

Africa's Natural Resources and African Economic Development


Looking to the future

….. the time has come for Africa to act now; to undertake hard-nosed goal setting. The euphoria phase of independence when leaders could get away with rhetorical, simplistic, vague and inane objectives (of freedom, equality, participation), when they could afford to have contempt for hard facts and when they could keep calm confidence in their "revelation" to create a new humanity, that time is now irretrievable. This has brought African countries to disaster. Goal setting must recognize the universality of certain human attributes, the nature and implications of existing key socio-economic variables and the requirements of an economy producing for surplus. In any case objectives should no longer be set on a course aimed to placate externally generated ideologies, whims of fancies. Nor should objectives be made as if the rest of the world did not exist or matter.

The search for the elusive summum bonum might be an attraction which philosophers can ill afford to ignore; but its utility to men of action is limited, indeed. In my view, there is likely to be very little agreement at any one time, in any society as to what constitutes the summum bonum. There is however likely to be less disagreement on the proposition that human beings everywhere do not want life of suffering or misery – at least not for its own sake. I therefore submit that a commitment to minimizing the social causes of human misery may be a promising start to goal formulation. I may also add in passing that for better or for worse, human beings value what they must work for, not that they work for what they value. And so it is that the grievances of man or woman as a consumer appear to be more important than his or her concerns as a producer.

Secondly, African leaders must pay more than lip service to Adam Smith's dictum that wealth of nations depends on "the skill, dexterity and judgment with which its labor is generally applied". This does not mean merely the setting up of more schools, the responsibility that all African governments have not only accepted but carried out with vigor and energy. The school system tends to superimpose forms of knowledge on existing fold knowledge without necessarily deepening the latter. As a consequence little new useful knowledge is produced. There is need to establish mechanisms and institutions that will deepen and expand Africa's stock of knowledge. Peasants, for instance, are inclined to augment their knowledge primarily from the most successful practitioners of their occupation. What must be underscored is that the basic task of education is the transfusion of values, but values cannot help us much to pick our way through life unless they become our own, a part to say of our mental makeup. An educational system has to give the people of a given culture the ability to make the world and their own lives intelligible. It is through the creation of intelligibility that meaningful education spurs the outburst of daring, initiative, invention and constructive activity. Finally, each country must critically appraise the arrangements that exist for allocating and distributing its available assets, property, power, privilege, prestige and participation – among individuals and groups, since these assets largely determine the latter's well-being.

African governments must also realize that there can be no genuine development without basic freedom and personal security. They must appreciate the fact that leadership of a nation state cannot be confined to "political" leadership; it must be extended to include labor, youth, parents, women, church, business, and professionals. Leaders in these entities must be recognized and given proper mandate and power. These changes will help unleash people's freedom to innovate and experiment. Consideration should also be given to the reduction of prevailing economic control in these countries. But to reduce controls is not the same thing as surrendering to market forces. Of course, these forces cannot and should not be wished away, they should be harness and utilized to fulfill the desired objectives. What must be appreciated however is that every restriction benefits some people and hurts others. Equally important is the realization that almost every control mechanism is circumvented in implementation, more often by those who have access to higher echelons of authority.

… The completion of that [decolonization] process requires attainment of economic liberation from the curse of poverty and misery. This will require a new leadership to propel the requisites of change. There will be no substitute for arduous effort, perseverance and for unity, founded at the highest political level, to uproot poverty and economic subordination. The African people have never hesitated to make sacrifices for a worthy cause. Sacrifice, perseverance and unity freed Africa from colonial rule. I believe that the same forces can free her from the misery and economic subordination which also deprive her of her dignity.

(Rweyemamu, 1992, pp 153)


*Third World Options: Power, Security and the Hope for Another Development
Published by Tanzania Publishing House, 1992
Justinian F. Rweyemamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom