Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,666
- 106,828
Watanzania wengi hatuna kumbukumbu na huwa hakuna maandishi mengi kuhusu Tanzania ya miaka ya nyuma na yaliyopo kidogo watu hatusomi. Haya mambo ya kukamata wazururaji yalikuwepo sana. Watu walihamishiwa mpaka kwenye vijiji vya ujamaa kwa nguvu! Na utendaji wa aina ya Magufuli sio mpya. Mrema alikuwa maarufu na anasifiwa kuliko Magufuli. Kwa kifupi Magufuli anaongoza kwa staili ya miaka ya nyumba ambayo mafanikio hayakupatikana. Ngoja niwaache na kibao cha Urafiki Jazz Band cha Gezaulole. Kipindi hicho ndicho ''wazururaji'' wanakamatwa kweli kweli. Polisi wakipita wanakusanya makundi ya vijana wasio na vitambulisho halafu wanawatoa kitu kidogo na kuwaachia.
Sema wewe, tukisema wengine watasema huyo Kiranga tu.
Magufuli hajui hata economic theory moja. Anahangaika tu.
Kibaya zaidi, hana hata utashi wa kujua. Anabaki kutaja boiling point ya silver na kilomita za barabara tu.
Ndiyo maana anarudia ukomunisti ambao ushatupwa kwenye jalala la historia.