Watu 167 wafanyiwa upasuaji wa mabusha Mtwara

Ujinga mtupu

JF-Expert Member
Aug 16, 2017
851
1,887
Wanaume 167 kati ya 200 wamefanyiwa upasuaji wa mabusha Mkoani Mtwara kwenye kampeni ya matende na mabusha iliyofanyika Mkoani humo kuanzia Feb 06,2023 hadi Feb 14,2023 “Mabusha huwapata Wanaume na Wanawake ila safari hii hakuna Mwanamke aliyekutwa na busha”, taarifa imeeleza.

Mratibu wa Kampeni hiyo ambaye pia anaratibu magonjwa yasiyokuwa na kipaumbele Mkoa wa Mtwara Alfonce Pachi, amesema moja ya sababu inayopelekea kuwa na matende na mabusha ni pamoja na kung'atwa na mbu wa aina zote lakini pia Watu kutokumeza dawa ya Kinga dhidi ya matende na mabusha.

“Lengo la kampeni ilikuwa kuchanja Wagonjwa 200 lakini waliofanyiwa upasuaji ni 167, wengine wana changamoto kadhaa zilizowapelekea kutokujitokeza kwenye zoezi ikiwa ni pamoja kuhofia huenda watashindwa kuendesha shaghuli zao za kiuchumi”

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula Dokta Zawadi Bwanali ametoa wito kwa Wananchi Mkoa wa Mtwara wenye tatizo la mabusha kujitokeza Hospitali ili waweze kupata huduma ya upasuaji na kwamba mabusha yanawapata Wanaume na Wanawake.
 
Ugonjwa maarufu sana huu maeneo ya Pwani.

Mhh! Hapo mwishoni mbona sijaelewa! Mabusha yanawapata wanaume na wanawake, kivipi?

Mwanamke na busha, wapi na wapi!! 🤔
 
Back
Top Bottom