Watoto wa Rais wa zamani wa Gabon (Omar Bongo) wafunguliwa mashitaka Ufaransa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Watoto wanne wa Rais wa zamani wa Gabon, Omar Bongo wamefunguliwa mashitaka Nchini Ufaransa kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma, matumizi mabaya ya mali za makampuni na rushwa.

Watoto hao Grace, Betty, Arthur na Hermine Bongo, wote wakiwa na zaidi ya miaka 50 walifunguliwa mashitaka hayo baada ya uchunguzi.

Wapelelezi wanaamini familia na jamaa wa hayati Bongo akiwemo Omar, Ali ambaye ndiye Rais wa Gabon, na Pascaline walinufaika kwa kujua kutokana kumiliki mali isiyohamishika iliyopatikana kwa njia ya udanganyifu yenye thamani ya Dola milioni 93.

Watoto wanne waliofunguliwa mashitaka wameka kuhusika na ulaghai unaotajwa dhidi yao.

Wamesema kuwa walipokea mali hizo zilizopo Jijini Paris kama zawadi kutoka kwa baba yao kati ya mwaka 1995 na 2004.

Omar Bongo alitawala Gabon kuanzia mwaka 1967 hadi alipofariki 2009 alipofariki na nafasi yake kuchukuliwa na mwakane, Ali.

Inadaiwa Omar Bongo alikuwa na watoto 54 ambao nao wengi wao wanaweza kukabiliwa na makosa mbalimbali.

Alipotafutwa Msemaji wa Ikulu ya Gabon, Jessye Ella Ekogha alikataa kutoa neno lolote kuhusu suala hilo.


Source: AFP

==========================


France files graft charges against Gabon ex-president's children

Four children of Gabon's late president Omar Bongo have been charged in France with embezzlement and corruption, a source familiar with the case told AFP Thursday.

The siblings -- Grace, Betty, Arthur and Hermine Bongo, all in their 50s -- were charged between March 25 and April 5 by financial investigators.

Charges include concealing embezzlement of public funds, corruption and misuse of company assets, documents seen by AFP showed.

Investigators believe members of the Bongo dynasty -- including Omar, his son Ali, 64, who is now president of Gabon, and his daughter Pascaline, 66 -- knowingly benefited from a fraudulently-acquired real estate empire worth at least 85 million euros ($93 million).

All four of Omar Bongo's children who have now been charged denied any knowledge of the allegedly fraudulent origins of the assets, the source said.

They told investigators they had received the properties -- apartments in the well-heeled 15th and 16th districts of Paris -- as gifts from their father between 1995 and 2004.

Grace Bongo's lawyer Elise Arfi said that it was "scandalous" that her client had been charged 25 years after acquiring the properties in question.

France's 15-year-old probe into "ill-gotten gains" originating from its former African colonies saw major bank BNP Paribas charged last year.

A further 14 people are under investigation, including relatives of President Denis Sassou Nguesso of Congo as well as several French individuals, among them a lawyer, a notary and a manager of a real-estate holding company.
"This process is now showing the extent to which French properties could only be fraudulently obtained with the help of accounting and legal engineers" in France, said William Bourdon, a lawyer for Transparency International France, which is a co-plaintiff in the case.

Omar Bongo, a close French ally, ruled the oil-rich state from 1967 until his death in 2009, when he was succeeded by his son Ali.

He had 54 children, more of whom may also face charges, the source said.

Gabonese presidential spokesman Jessye Ella Ekogha declined to comment on the charges when contacted by AFP.
 
Kama hii kesi kesi itawanufaisha raia wa Gabon, ninawaombea Wafaransa mafanikio yote 🙏🏾
 
Na hapo bado waafrika watalaumu tu wazungu kwa madhila yao. Hakuna watu bure kama waafrika na ndio maana sisi hatutakaa tuone uzuri wa hii dunia.
 
Fitina na wivu wa wazungu,mm nipewe uridhi na wazazi wangu halafu leo mje muanze kuniambia oo alipataje hizo mali,upuuz na wivu tu.kwann hawakumuuliza kipindi bongo yupo hai hayo maswari!!??, Waachwe jamaaa wale jasho la baba yao!!!shut...simama kabisa!!
 
Fitina na wivu wa wazungu,mm nipewe uridhi na wazazi wangu halafu leo mje muanze kuniambia oo alipataje hizo mali,upuuz na wivu tu.kwann hawakumuuliza kipindi bongo yupo hai hayo maswari!!??, Waachwe jamaaa wale jasho la baba yao!!!shut...simama kabisa!!
Wazungu wana unafki mwingi sana.
Wakati fedha zinaingia Ufaransa na uwekezaji unafanyika walikua wanajua kila kitu ila wakauchuna,
Sasa hivi inawezeka kuna tofauti za kisiasa baina yao ndio wanajifanya kua wakali.
Huyu Mfaransa ndio anaongoza kwa kashfa za kuhusika na mauaji ya halaiki na wizi wa rasilimali za kutosha katika mataifa yaliokua ni koloni lake barani Africa.
 
Hao Ufaransa wenyewe Wezi tu,Waneziibia Nchi za Africa toka miaka ya 1920 na bado wanaendelea kuiba na hakuna wa Kuwashtaki
hii ni dunia ya utanda wazi. je unaweza sema waliiba nini Africa? au na wewe unasema tuu ili azaliwae kesho nae aseme mpaka inakuwa ngonjera bila kufafanua nini walichoiba na wapi?
 
hii ni dunia ya utanda wazi. je unaweza sema waliiba nini Africa? au na wewe unasema tuu ili azaliwae kesho nae aseme mpaka inakuwa ngonjera bila kufafanua nini walichoiba na wapi?
Kama haulieliwi hilo Kalaga Baho
 
Back
Top Bottom