aise
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 4,124
- 11,992
Kuna hii kasumba sijui tuseme ulimbukeni limeenea sana kwa wafanya biashara na watoa huduma.
Mfano unaenda dukani kununua shati, muuzaji anakwambia bei ya shati ni 40,000.
Wakati shati kama hilo kwa kawaida huwa bei yake ni 15,000, Sasa unamuuliza mbona bei sana? Anajibu "ulikuwa na sh ngapi?"
Unamjibu, basi bwana, (huku unaondoka) umeanzia juu sana, mimi nilidhani labda itakuwa 12,000.
Unaondoka zako anakuita "boss rudi ongeza buku basi nikuachie"
Hivi kwanini usimwambie mteja wako bei inayoeleweka?
Kwangu mimi nikiona mtoa huduma ana hiyo kasumba huwa namdharau sana na hatawahi tena kuniona narudi kwake.
Badilikeni aise, wengine kukaa unalialia na muuzaji eti apunguze bei hatuwezi.
Taja bei ya kueleweka siyo unataja bei za kidalali.