Watizie mnaboaaa..... Mnafanya hivi !!!!????

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,504
12,829
nyumbani ni nyumbani....
Mdharau kwao hana asili................
Dah... Watanzania wenzangu? Tunayoendekeza ni kinyume na uzalendo!

Kiongozi akifuata sheria........ Mnonko huyo/ mlokole huyo!!!. (samaki wa magufuri, tume ya mwakyembe, barua ya shelukindo n.k) hii kitu inawakatisha tamaa wapiganaji
tunapenda udalali kupindukiaaa jamani!!!
Tunapenda kukumbatia uharifu na waharifu kwa kisingizio cha ukarimu..... Wangapi wanalea wahamiaji haramu? Wangapi wanalea majambazi, na sasa al- shabaab na kuwafadhili?
Tunapenda kupapatikia raia wa kigeni na kuwaeleza siri zetu zote, na historia yetu yote hata kabla ya kuwajua vizuri.
Tunapenda kukimbilia maeneo yenye ajali ama rapsha yoyote bila kujali hatari ya mlipuko au maafa yatakayotokea na lengo hasa la watu hawa ni kuondoka na chochote.
Mnaofanya kazi maofisini lazima uondoke na kitu kutoka ofisini na kukipeleka kwako mfano. Bahasha, karatasi, karamu, fedha, kutoa kazi kwa upendeleo, kufanya kazi kwa kumwangalia mtu....
Mwisho... Mtu asiyeiba eneo lake la kazi tunamwita mjinga.... Ohh mara hajengi, hana gari, hana kile hana hiki wakati anafanya tra or bot or polisi. Wizi mtupu
uozo tunaujenga sisi wenyewe ngoja tunyonyolewe na tutabaki watupu.
Nawatua bwaaaaa!!!!!!!!!!!!!!

 
Back
Top Bottom