Wateule wa Rais Magufuli tuondoleeni aibu hii

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Ninapoandika uzi huu sisemi kwamba ni WATEULE wote wa rais wana tabia hii ambayo nitaielelza hapa chini. Ila ni BAADHI yao hawajui kabisa ETHICS za KIUTUMISHI.Na wanafanya kama vile mwalimu na mwanafunzi wa shule ya msingi.

.Sina maana ya kudharau Walimu wa Msingi bali ni mfano tu kuwa wanafunzi hao huwa wangali ni wadogo chini ya miaka 18 na wakati mwingine hukemewa na walaim iili baadaye maishani wawe watu responsible.

Kumekuwa sasa ni kama kawaida MTEULE na MTEULE wakijibizana ama KUFOKEANA mbele ya vyombo vya habari. Hili HALIKUBALIKI kabisa na ni kuvunja MAADILI ya kiutumishi.

Juzi juzi mwingine KAMZABA makofi mtumishi mwenzake.
Mwingine naye kamjibu mteule mwenzake kupitia vyombo vya habari kwamba HAKUBALIANI naye.

DC mwingine Arumeru naye kamfokea DED, tena mbele ya RC.Na badala RCkumchuliahuyo DC hatua za kinidhamu yeye anabaki akishangaa na kutabasamu!!
Sasa jamani mchezokama huu ukiruhusiwa uendelee tunaelekea wapi??

This is unacceptable in a modern society more so kwa watumishi SERIKALI waliopewa DHAMANA ya kuwatumikia wananchi.
Na zaidi ya hayo yote WOTE WANAITUMIKIA
serikali moja na Rais mmoja aliyewateua hivyo ni kusemea. "WOTE ni WATEULIWA" Regardlelss of the pecking order.

Kama kuna KOSA limetokea basi MECHANISMS ZA KIUTAWALA zitumike ndani ya PAZIA pasipo sisi raia kujua chochote kinachoendelea..
KUTATUA kwa KUMFOKEA ama KUMLAUMU mtumishi mwenzako HADHARANI mbele ya WANANCHI hilo si nzuri na Iinatutia AIBU kama Watanzania na serikali kwa ujumla
Tafadhali tuondoleeni AIBU hii!!!.

Sisi kama raia basi tunabaki tukinashangaa. Kwani neno collective responsibility liko wapi AMA KUNA MGAWANYIKO?
 
Huu hauwezi kuitwa uwajibikaji wa pamoja.
Ni dalili za kinachoitwa kijiwe kinachoitwa serikali.
Mkuu wa Mkoa anaagiza makontena.
Waziri wa Fedha anasema alipe kodi.
Rais anaunga Mkono.
Waziri wa Sheria anamkosoa hadharani Mkuu wa Mkoa.
Katibu Mkuu wa Chama Tawala anamkosoa Mkuu wa Mkoa kwa "kuumiliki Mkoa na watu wake".
Halafu Mkuu wa Mkoa anajibu "watasubiri sana".
Hii ni zaidi ya hatari
 
Na mimi nazungumzia hiko hiko hujanielewa tu.soma tena comment
Ni hivi kwa kifupi,usitegemee wateule hao wawe na hekma au heshima au watende mazuri kama tu aliyewateua kalidhalilisha taifa juzi
Hapo umenielewa ?
Mkuu nimekuelewa. Hata hivyo unaweza kunukuu ni WAPI alipolizalilisha taifa ili tuanzie hapo?
 
Mkuu nimekuelewa. Hata hivyo unaweza kunukuu ni WAPI alipolizalilisha taifa ili tuanzie hapo?
Mkuu, rais kusema yeye ni chizi hukuona hizo nyuzi na video clip humu siku chache zilizopita ?jaribu kufatilia kama ulikua hujaziona
Pia kiongozi mkuu wa nchi anaposema ana tatizo la kiakili (chizi,kichaa) means anaongoza watu vichaa pia na ni aibu kwa taifa kuongozwa na mtu mwenye tatizo la akili
(Japo watu walitetea ile kauli. Lakini ni wazi alikubali ana tatizo kichwani)
 
Back
Top Bottom