Watendaji wa Kata Kulipwa Posho

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,977
958
MBUNGE JANEJELLY NTATE AHOJI KULIPWA POSHO ZA WATENDAJI WA KATA

Mbunge wa Viti Maalum Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janejelly James Ntate amehoji Bungeni kuhusu watendaji wa Kata wanaolipwa na wasiolipwa posho ambapo swali lilijibiwa na Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Deo Ndejembi

"Serikali katika bajeti yake ilipitisha posho ya watendaji wa Kata ya kila mwezi lakini posho hii imeonekana ni hisani baadhi ya Halmashauri zinalipa na zingine hazilipi. Je, Serikali ina tamko gani kuhusu posho hizi?" - Mhe. Janejelly James Ntate(Mb)

"Posho zilipitishwa kwenye bajeti na Bunge. Tutaenda kuhakikisha linatekelezwa kwa sababu tayari zikitengwa ili watendaji waweze kupata posho hizi za madaraka" - Mhe. Deo Ndejembi
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-05-12 at 18.47.03.mp4
    9.2 MB
Back
Top Bottom