Watendaji wa ardhi kukaa kituo kimoja zaidi ya miaka 10 ni chanzo kikubwa cha migogoro

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,271
2,024
Leo nilikuwa kwenye Kliniki ya Ardhi Manispaa ya Ubungo pale Stop Over.Kuna Bibi kizee alikuwa ameleta mgogoro wake pale ili upatiwe ufumbuzi.Bibi huyu amesema mgogoro huo ambao amekuwa nao toka akiwa Manispaa ya Kinondoni kabla ya kuigawanya Manispaa ya Kinondoni na kuzaliwa Manispaa ya Ubungo kuwa Umetengenezwa na Watendaji wa Ardhi Manispaa ya Kinondoni, Mgogoro ambao ulikuwa wa kudhulumiwa kiwanja chake na Watendaji wa Ardhi Kinondoni miaka ya 2008.

Katika Simulizi ya Bibi alizungumzia jinsi Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Ndg Wiliam Lukuvi alivyowahi kuzifunga Ofisi zote za ardhi Mkoa wa Dar es salaam kutokana na Kukithiri kwa Migogoro na Malalamiko Makubwa ya Wananchi.

Mkuu wa Mkoa aliagiza Ofisi zote za Ardhi kulindwa na Polisi na Watendaji wote wa Ardhi kufika ofisini bila kuingia ndani mpaka hapo Uchunguzi dhidi yao utakapokamilika. Baada ya Uchunguzi kukamilika wapo Watendaji waliofukuzwa kazi na wapo waliohamishiwa mikoa na wilaya mbalimbali za nchi na kuwaleta Watendaji wapya kutoka Mikoa na Wilaya mbalimbali.

Kitendo hicho kilileta Utendaji Mpya na Wenye Tija wa Ardhi na kupunguza Migogoro Mingi sana ya Ardhi.Kutokana na Watendaji hao kukaa Miaka ya Miaka 10 sasa hali imerudi tena ya Migogoro ya Ardhi ktk Jiji la Dar es salaam.Watendaji wamekuwa Wenyeji sana wamejijengea ukaribu sana na Matapeli na Madalali wa ardhi ambao huwatumia kuuza Ardhi za watu.

Ushauri kwa Waziri wa Ardhi.
Ili kupunguza kwa kiasi kikubwa cha Migogoro nakushauri Fuata njia aliyotumia Bw Wiliam Lukuvi ya Kuwahamisha Watendaji wote wa Ardhi kwa maana ya Maafisa Mipango Miji, Wapima Ardhi Wathamini na Maafisa Ardhi wote walikaa ktk Manispaa zote za Mkoa wa Dar es salaam kwa Miaka 10 na kuendelea na kuleta Watendaji wengine kutoka Sehemu mbalimbali za Nchi.

Kufanya hivyo kutasaidia Kuvunja Mtandao wa hao watendaji na Matapeli na Madalali wa Ardhi ambao wamezoeana kwa zaidi ya Miaka 10.Najua uhamisho ni gharama ila huo Uhamisho utapunguza Migogoro mingi ya ardhi Kama ilivyopungua wakati wa Utawala wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.Wiliam Lukuvi.
 
Hawa maafisa wanamtandao mkubwa Tena hatari Sana

Huyo Lukuvi ni Babayao anawajuwa vijana wake wote!!
 
Back
Top Bottom