Watawala wetu mmerogwa?

Unajua wakati mwingine nafikiri we "a selfish bunch of self-proclaimed non-governmental watchdog"... Yawezekana tumezidi kutafuta mabaya, labda tujiulize mazuri ya ATCL ni yapi na tumpe Mattaka Udaktari wa Falsafa...

At least waliweza kubadilisha ATCL rangi zake!!! that is something to be proud of!

Je hilo ndilo jukumu alilopewa ATCL? Sijaona zuri lolote zaidi ya kuipeleka ATCL to hell!
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Naomba niandikie kutoka kwenye hisia kidogo; Naomba niandike toka kwenye vionjo vyangu vilivyojeruhiwa; Naomba niandikie kutoka kwenye moyo uliojawa na hasira, kero na ambao unajihisi kinyaa!; Naomba niandike kama mtu ambaye akili zake hazijakaa sawasawa na ambaye anaweza kuitwa "fyatu"! Naomba niandike kuhusu haya ya Shirika letu la ndege la ATCL ambalo limekuwa kituko cha taifa na aibu ya nchi yetu!

Watawala wetu mmerogwa? Tumefikaje hapa, je hili limefika kama kwa ghafla na kwamba hakukuwa na dalili zozote? Kwamba leo bila haya mnaitisha vikao vya dharura na kutoa "siku saba" za kupata maelezo toka kwa wazembe na waliofuja mali za shirika hili kana kwamba hamkuliona hili? Ati leo mnathubutu kuelezea kilichofanyika ATCL kuwa ni uzembe wakati kwa mwaka mzima vumbi lake mlishaliona toka mbali? Mmerogwa nyinyi?

Nauliza kama mmerogwa kwa sababu hakuna maelezo yoyote ya kiakili ambayo yana ushawishi wa kimantiki na yenye uzito wa ushahidi wa kisayansi yanaweza kuelezea ubutu wa matendo yenu na ukimya wa maneno yenu kwa mwaka mzima tangu king'ora cha tahadhari tulipokipuliza mwezi Disemba mwaka jana! Ni watu waliopumbazwa na dawa za mitishamba au waliorogwa 'kisayansi' ndio pekee wanaweza kufafanua ni kitu gani kiliwakumba. Mmepitiwa na jini gani lililowafanya mduwae na kuangusha midomo yenu ya chini na denda zikidondoka kama wale wasemwao "washangaao feri"?

Tuliimba na kupaza sauti, makoo yetu yakakauka. Tukawaambia tena bila kuuma uma maneno kuwa ATCL kuna uozo; tena uozo mkubwa wa kiuongozi. Tukaweza mipango yao ya kukodisha dege lenye matatizo ya kiufundi zaidi ya 100 tena kwa bei mbaya; tukawawekea na mikataba yao waliyoingia kuhusu dege hilo hilo, lakini muda wote huo nyinyi mkaendelea kukaa kimya na kuacha ATCL ijiendeshe kama kikaragosi kinachoenda kwa kupiga ufunguo!

Tukawawekea na ushahidi jinsi gani watendaji wa ATCL wamefuja mali zetu huku wakikinga mikono yao kuyupa zaidi; tukawaonesha jinsi mikakati yao ilivyokuwa mibaya na mibovu; tukawaonesha ni jinsi gani David Mattaka na genge lake la makuwadi wa ufisadi wameshindwa kuliongoza shirika hilo. Kwa mwaka mzima tumefanya hivyo pasipo mafanikio.

Tumefanya kama kile tulichokifanya kwenye suala la Ukraine miaka miwili iliyopita ambapo tulionesha upungufu na uozo wa bodi ya mikopo. Mkasimama mkatubeza, mkatucheka kwa sababu ati tunawaonea wivu; kwamba hatupendi maendeleo yenu; kwamba tunajifanya tunajua sana; kwamba ati kama tuna uchungu basi turudi nyumbani kusaidia nchi yetu; kwamba tukae kimya kwa sababu sisi ni wakimbizi! Hivi nyinyi mmerogwa?

.........................!!!!!!!!!!!!!!

Badala ya kuamua kuchukua hatua za kushughulikia tatizo hili mnafanya kile ambacho ni kitendo cha woga kabisa; kwamba mnataka wachina waingie mkataba wa kuliendesha! kwamba ya Afrika ya Kusini hayakuwa funzo, ya Tanesco hayakuwa funzo, mnataka na ATCL mjaribu tena! Hivi katika taifa letu hakuna watu wenye uwezo kweli wa kuliendesha shirika hilo? Kweli mmekuwa waoga kushughulikia matatizo hadi tatizo likija mnakimbilia kwa "mjomba" Uchina, mmerogwa nyinyi?

Mnataka kutuambia kuwa mmeshindwa kukaa chini na kugonganisha vichwa vyenu kutafuta suluhisho la kitanzania kwenye tatizo la kitanzania? Hivi mnaogopa nini kufanya maamuzi magumu na kutoa nafasi kwa WAtanzania wazalendo wa kweli kuliendesha? NI ninyi wenyewe mlimrudisha David Mattaka licha ya kuwekwa nje ya utumishi, mlikuwa mnafikiria nini? Kwamba ATCL ni mahali pa mafunzo?

................................!!!!!!!!

Mkuu pole sana kwa kuongea kwa hisia kali na ambazo zinawaelemea waTanzania wengi.
Hawajalogwa mzee.Hawajalogwa hao tatizo ni moja tu.
Watu hatujifunzi kutokana na matatizo.
ATCL kimsingi ni chombo cha Serikali kinachofanya biashara ya usafiri, biashara inayohitaji mtaji mkubwa sana , ikiwa ni pamoja na mtaji mkubwa wa uendeshaji.

Tatizo la ATCL si la mtu mmoja na kwa vyovyote haliwezi kutatuliwa na uongozi uliopo.Mwenye mali ,Serikali amewekeza kiduchu.Matatizo hayatatuliwi katika muda unaostahili, na matatizo hayo hayaondoki yasipotatuliwa ila yanalundikana na kuzaa matatizo mengine mapya.

Tatizo kubwa zaidi la ATCL ni muundo wake wa kibiashara.Biashara ya usafiri wa anga ni very competative, na very technical.
Unapokuwa na Bodi ya watu kadhaa, hawana "stake "yoyote mle ndani ya shirika, sana sana waangalizi tu.
Una Management kubwa tu inayobugia gharama kubwa za uendeshaji.
Gharama nyingi tu za uendeshaji na operations za ndege.Hapo unapata picha kamili kuwa ATCL is "top heavy".Gharama za uendeshaji zinailemea ATCL.
Mbona hawawezi hata kuiga wenzao wa ndege binafsi ya PRECISION.
Jaribuni kulinganisha hawa watoto wawili-wote wa kiTanzania.
Kitu cha kujifunza hapa ni kuwa kama yalivyokufa mashirika ya TRC,RTC KAMATA,RETCOs na mengine mengi, ATCL is doomed.
Kingine cha kujifunza ni kuwa Serikali si rahisi kufanya biashara kwa kupitia mashirika.
Cha tatu kujifunza ni kuwa si rahisi kuendesha biashara kama uwekezaji katika biashara hiyo ni hafifu.
Kitu cha nne ni kwamba kama uongozi wa biashara yoyote hauna "stake"yoyote katika biashara hiyo, basi uongozi huo si rahisi kuwa na uchungu na biashara hiyo.
 
Waliohusika kuifilisi ATCL wasakwe- Waziri

2008-12-19 11:30:02
Na Mashaka Mgeta

Serikali imeitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ndege Nchini (ATCL), kuwabaini wahusika katika kadhia ya kulifilisi Shirika la Ndege Nchini (ATCL), ili wawajibishwe.

Hatua hiyo, ilitangazwa jana na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, alipozungumza katika mkutano wa majumuisho, baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa barabara za jijini Dar es Salaam.

``Niliwapa Bodi siku saba kunipa maelezo yenye kueleza sababu zilizofanya shirika hilo kufika hapo lililopo...watakaobainika kulifikisha katika hatua hiyo, watawajibishwa,`` alisema.

Dk. Kawambwa alisema katika mapendekezo yake, Bodi ya ATCL inapaswa kuainisha njia bora zitakazotumika kuwalipa mishahara wafanyakazi wake, katika kipindi ambacho haifanyi biashara.

Hivi karibuni, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), iliinyang`anya ATCL cheti cha uendeshaji wa safari za anga, kutokana na kutokidhi masharti yanayobainishwa katika sekta hiyo.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, David Mattaka, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, sehemu kubwa ya mapungufu 482 yaliyobainika katika ATCL, yalisharekebishwa, bila kuwekwa katika kumbukumbu rasmi za maandishi.

Kwa mujibu wa Mattaka, licha ya kutokuwepo kwa kumbukumbu hiyo, ATCL ilikuwa inajiendesha kwa kufuata sheria za anga zinazotambulika kimataifa.

Lakini, akizungumza jana, Dk. Kawambwa, alisema kasoro zilizobainika katika ukaguzi uliofanywa dhidi ya ATCL, zinapaswa kufanyiwa kazi, ili kuliepusha shirika hilo na kadhia kama iliyotokea.

``Hatuwezi kuendeleza hulka ya kuwaone aibu watu wanaolitia Taifa hasara kubwa na kusababisha walio wengi kuendelea kuteseka,`` alisema.

Alitoa mfano wa kasoro hizo kuwa ni pamoja na mafunzo ya marubani yanayopaswa kufanyika mara kwa mara na matengenezo ya ndege za shirika hilo.

Hata hivyo, alisema serikali imelazimika kuingilia kati mchakato wa kurekebisha kasoro hizo, ili kuifanya ATCL irejee katika utoaji wa huduma zake kama ilivyokuwa awali.

``Hili ni shirika letu wenyewe, ni mali yetu sisi hivyo tutahakikisha kasoro zinafanyiwa kazi, na kurejeshwa kwa cheti chake mapema iwezekanavyo`` alisema.

Alisema katika kufuatilia suala hilo, wizara yake imeshafanya mazungumzo na ATCL na TCAA, ambapo imebainika kuwa mchakato wa kushughulikia kasoro zilizojitokeza unaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, ATCL inahitaji kiasi cha Dola 273,000 za Marekani ili kushughulikia matatizo yanayoikabili na kufikia hatua ya kujiendesha kibiashara.

Awali, Ofisa Uhusiano wa Umma wa TCAA, Abel Ngapemba, alisema hatua ya Umoja wa Mashirika a Ndege Duniani (IATA), kuizuia ATCL kufanya biashara, haitakuwa na athari kubwa kwa shirika hilo.

Aliliambia gazeti hili jana kuwa tamko la IATA lililokaririwa jana na baadhi ya vyombo vya habari, halihusu washirika wa kibiashara wasiokuwa wanachama wake.

Kuhusu hatua iliyofikiwa katika ukaguzi wa marekebisho yaliyowasilishwa na ATCL ili kupata cheti cha kutoa huduma ya usafiri wa anga, Ngapemba alisema suala hilo linashughulikiwa kwa umakini.

Hata hivyo, hakuwa tayari kusema ikiwa TCAA itafanikiwa kukamilisha zoezi hilo ndani ya siku kumi za kazi, ikiwa ni kuanzia Desemba 11, mwaka huu kama alivyobainisha Mattaka.

Ngapenda alisisitiza kuwa njia pekee kwa ATCL ni kufanikisha utunzaji wa kumbukumbu za kimaandishi kuhusu utekelezaji wa masharti ya usafiri wa anga.

My Take:
Hii inanikumbusha hadithi mojawapo ya Sungura. Sijui alijibadili namna gani na kumshawishi mtoto ampikie lile jogoo kubwa badala ya yeye mwenyewe kugeuzwa kitoweo kama alivyoagiza baba! Ati Waziri amewaagiza bodi watafute waliohusika na kulifikisha ATCL hapa.... Unawauliza wezi nani kaiba!?
 
Kudadeki walahi! Yaani hakuna chembe hata kidogo ya common sense. Inahuzunisha lakini nimecheka kweli.....
 
sasa kuna mtu yeyote anayeweza kukisia sababu itakayotolewa baada ya siku saba..

Sababu ziko nyingi sana:-
Wakoloni, ukame, Mafuriko, Wahindi, Wazungu, Utumwa, Waarabu, MWANAMKE, Nduli Idd Amini, Nzige, Rwanda Genocide (Wakimbizi), Wasomali, (Kwa Wazenji -- Muungano na Wabara), kuongezeka kwa joto duniani, barafu ya Mlima Kilimanjaro kuisha, Ukimwi, .........

Kwa ufupi ni kila SABABU unayoweza kuweka KASORO SISI MIPINGO.
 
Unaweza kupata nakala ya hoja hii kwenye pdf ikiwa na mabadiliko kidogo...
 
Attachments

  • WATAWALA WETU MMEROGWA.pdf
    76.3 KB · Views: 104
Kwanza aliyemteua mtu aliyefukuzwa kazi kwa matumizi mabaya ya ofisi( Mataka) ana matatizo ya akili.
 
Mkuu pole sana kwa kuongea kwa hisia kali na ambazo zinawaelemea waTanzania wengi.
Hawajalogwa mzee.Hawajalogwa hao tatizo ni moja tu.
Watu hatujifunzi kutokana na matatizo.
ATCL kimsingi ni chombo cha Serikali kinachofanya biashara ya usafiri, biashara inayohitaji mtaji mkubwa sana , ikiwa ni pamoja na mtaji mkubwa wa uendeshaji.

Tatizo la ATCL si la mtu mmoja na kwa vyovyote haliwezi kutatuliwa na uongozi uliopo.Mwenye mali ,Serikali amewekeza kiduchu.Matatizo hayatatuliwi katika muda unaostahili, na matatizo hayo hayaondoki yasipotatuliwa ila yanalundikana na kuzaa matatizo mengine mapya.

Tatizo kubwa zaidi la ATCL ni muundo wake wa kibiashara.Biashara ya usafiri wa anga ni very competative, na very technical.
Unapokuwa na Bodi ya watu kadhaa, hawana "stake "yoyote mle ndani ya shirika, sana sana waangalizi tu.
Una Management kubwa tu inayobugia gharama kubwa za uendeshaji.
Gharama nyingi tu za uendeshaji na operations za ndege.Hapo unapata picha kamili kuwa ATCL is "top heavy".Gharama za uendeshaji zinailemea ATCL.
Mbona hawawezi hata kuiga wenzao wa ndege binafsi ya PRECISION.
Jaribuni kulinganisha hawa watoto wawili-wote wa kiTanzania.
Kitu cha kujifunza hapa ni kuwa kama yalivyokufa mashirika ya TRC,RTC KAMATA,RETCOs na mengine mengi, ATCL is doomed.
Kingine cha kujifunza ni kuwa Serikali si rahisi kufanya biashara kwa kupitia mashirika.
Cha tatu kujifunza ni kuwa si rahisi kuendesha biashara kama uwekezaji katika biashara hiyo ni hafifu.
Kitu cha nne ni kwamba kama uongozi wa biashara yoyote hauna "stake"yoyote katika biashara hiyo, basi uongozi huo si rahisi kuwa na uchungu na biashara hiyo.

kuhusu uchungu, mbona Kimei wa crdb amefanikiwa wakati yeye mwenyewe hajawekeza bali ni mwajiriwa.? au hata kama anakata cha juu, sio kwenye mbegu, bali kwenye cream.
Kuhusu mtaji mdogo wa ATC, ni kweli lakini hicho kidogo walicho kuwa nacho wange kitumia kwa uadilifu, wasinge fika hapo, hii ina nikumbusha enzi zile mtu ananzisha kampuni binafsi, na kuwekeza kwenye ofisi na office equipment na business card with wording impo-expo, badala ya kuwekeza kwenye malighafi. sasa ndugu zetu hawa from day one wanaanza kuzikata kabla ya kuzalisha.
 
August, ni kweli kabisa kuwa Kimei hajawekeza katika Benki yake na ni mwajiriwa.Biashara ya ndege kwa upande mwingine ni very sensitive to cost ukilinganisha na Benki.Kuwekeza kidogo ni tatizo kubwa, tatizo kubwa zaidi ni mtaji wa uendeshaji.Ile biashara inaenda kwa masaa ,kipuri kikiisha hata kama bado kizima ,masaa yake yakiisha lazima kibadilishwe, fwedha ya kigeni hyo.
Mashirika mengi tu ya kigeni yamesalimu amri, SAS na hata SwISSAIR ni kati ya mashirika yenye matatizo makubwa.
Siwatetei hawa watu lakini biashara hii imewazidi kete, hawaiwezi.Tumshukuru Mungu kwamba zingeweza kutokea ajali zisizo za lazima kutokana na uendeshaji wa ATCL usiokidhi matakwa ya usafiri wa anga.
 
Mkuu gwakisa, japo nia yako ni nzuri lakini nakuomba usifanye falacy of generalization. SAS na SWISSAIR zinakumbana na matatizo mengine siyo kama haya ya ATCL. Matatizo ya SAS na SWISSAIR naweza kuyaelezea kwa wakati wake muafaka. Hapa tunaongelea juu ya ATCL. ATCL imekumbwa na ujambazi wa makusudi wa chukua chako mapema bila aibu, uchungu wala uzalendo. Kuna kuiba huku ukiwajibika ili kufunika majeraha ya wizi wako na shirika liendelee kuchechemea. Lakini ATCL si hivyo, pale kilichotokea ni kukata mguu kabisa!!!!!!! sasa utachechemea kivipi na mguu haupo? Mfano mmoja tu, fedha zilizowekezwa zimetumika kukodisha (kununua) madege mabovu kwa bei ya juu sana (sawa na ndege nzima zenye hadhi !!). Wahusika waliofanya hivyo tunawajua na wamezawadiwa VX, na magari mengine kama 10 percent yao!!! Unatarajia nini? Kuna shida ya sifa (qualifications) za mtu anayefaa kuongoza airline. Chunguza management iliyopo madarakani sasa utaghundua haikupaswa kuwepo hapo, nk. nk. nk. nk. TZ bwana!!! - mpaka lini mambo haya?!?.
 
Mkuu gwakisa, japo nia yako ni nzuri lakini nakuomba usifanye falacy of generalization. SAS na SWISSAIR zinakumbana na matatizo mengine siyo kama haya ya ATCL. Matatizo ya SAS na SWISSAIR naweza kuyaelezea kwa wakati wake muafaka. Hapa tunaongelea juu ya ATCL. ATCL imekumbwa na ujambazi wa makusudi wa chukua chako mapema bila aibu, uchungu wala uzalendo. Kuna kuiba huku ukiwajibika ili kufunika majeraha ya wizi wako na shirika liendelee kuchechemea. Lakini ATCL si hivyo, pale kilichotokea ni kukata mguu kabisa!!!!!!!
..................................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wahusika waliofanya hivyo tunawajua na wamezawadiwa VX, na magari mengine kama 10 percent yao!!! Unatarajia nini? Kuna shida ya sifa (qualifications) za mtu anayefaa kuongoza airline.
.......................!!!!!!
Chunguza management iliyopo madarakani sasa utaghundua haikupaswa kuwepo hapo

Mkuu SHARE, toboa tu baba, simfagilii mtu mie, ila kama nilivyosema awali duka ambalo wewe mwenyewe hujaweka bidhaa zako ndani yake ili ziuzwe, utalifilisi kwa kuliibia bidhaa.
Hakuna uchungu pale ATCL.
Na hii ni licha ya ukweli kuwa biashara hii ikiwekezwa vizuri inalipa.Na uwekezaji wenyewe ni ule strategic, mbona PRECISION wanaelekea kuweza, business model yao ikoje? , tujiulize wakuu.
 
Unaweza kupata nakala ya hoja hii kwenye pdf ikiwa na mabadiliko kidogo...

Nadhani kusema "wamerogwa" kunaashiria kuwa wao hawana makosa ila kuna mchawi aliyewaroga ndiye wa kualumiwa. Ni afadhali ungejiuliza kuwa "Watawala wetu hawana akili timamu?"
 
Wasulubishwe, Wasulubishwe, wauawe, wauawe, wachunwe ngozi, tuchemshe ubongo wao na kumwagia salifyuriki esidi ili akil kama zao zisirudi tena maishani mwetu na jamii yetu!
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Naomba niandikie kutoka kwenye hisia kidogo; Naomba niandike toka kwenye vionjo vyangu vilivyojeruhiwa; Naomba niandikie kutoka kwenye moyo uliojawa na hasira, kero na ambao unajihisi kinyaa!; Naomba niandike kama mtu ambaye akili zake hazijakaa sawasawa na ambaye anaweza kuitwa "fyatu"! Naomba niandike kuhusu haya ya Shirika letu la ndege la ATCL ambalo limekuwa kituko cha taifa na aibu ya nchi yetu!

Watawala wetu mmerogwa? Tumefikaje hapa, je hili limefika kama kwa ghafla na kwamba hakukuwa na dalili zozote? Kwamba leo bila haya mnaitisha vikao vya dharura na kutoa "siku saba" za kupata maelezo toka kwa wazembe na waliofuja mali za shirika hili kana kwamba hamkuliona hili? Ati leo mnathubutu kuelezea kilichofanyika ATCL kuwa ni uzembe wakati kwa mwaka mzima vumbi lake mlishaliona toka mbali? Mmerogwa nyinyi?

Nauliza kama mmerogwa kwa sababu hakuna maelezo yoyote ya kiakili ambayo yana ushawishi wa kimantiki na yenye uzito wa ushahidi wa kisayansi yanaweza kuelezea ubutu wa matendo yenu na ukimya wa maneno yenu kwa mwaka mzima tangu king'ora cha tahadhari tulipokipuliza mwezi Disemba mwaka jana! Ni watu waliopumbazwa na dawa za mitishamba au waliorogwa 'kisayansi' ndio pekee wanaweza kufafanua ni kitu gani kiliwakumba. Mmepitiwa na jini gani lililowafanya mduwae na kuangusha midomo yenu ya chini na denda zikidondoka kama wale wasemwao "washangaao feri"?

Tuliimba na kupaza sauti, makoo yetu yakakauka. Tukawaambia tena bila kuuma uma maneno kuwa ATCL kuna uozo; tena uozo mkubwa wa kiuongozi. Tukaweza mipango yao ya kukodisha dege lenye matatizo ya kiufundi zaidi ya 100 tena kwa bei mbaya; tukawawekea na mikataba yao waliyoingia kuhusu dege hilo hilo, lakini muda wote huo nyinyi mkaendelea kukaa kimya na kuacha ATCL ijiendeshe kama kikaragosi kinachoenda kwa kupiga ufunguo!

Tukawawekea na ushahidi jinsi gani watendaji wa ATCL wamefuja mali zetu huku wakikinga mikono yao kuyupa zaidi; tukawaonesha jinsi mikakati yao ilivyokuwa mibaya na mibovu; tukawaonesha ni jinsi gani David Mattaka na genge lake la makuwadi wa ufisadi wameshindwa kuliongoza shirika hilo. Kwa mwaka mzima tumefanya hivyo pasipo mafanikio.

Tumefanya kama kile tulichokifanya kwenye suala la Ukraine miaka miwili iliyopita ambapo tulionesha upungufu na uozo wa bodi ya mikopo. Mkasimama mkatubeza, mkatucheka kwa sababu ati tunawaonea wivu; kwamba hatupendi maendeleo yenu; kwamba tunajifanya tunajua sana; kwamba ati kama tuna uchungu basi turudi nyumbani kusaidia nchi yetu; kwamba tukae kimya kwa sababu sisi ni wakimbizi! Hivi nyinyi mmerogwa?

Mkadharau sauti za tahadhari zilizopigwa kama kengele kwenye Jamiiforums; mkanyamaza tulipoandika kwenye magazeti yetu; mkawa mnatafuta kujua ni nani anavujisha "siri za serikali". Mkawatimua watu kazi ATCL mkidhania kuwa mmeziba uozo wenu! Sasa leo mnashtuka kana kwamba mmegutushwa na mpiga mbiu!? Mnabeba shuka kupeleka hospitali wakati mgonjwa keshakufa? Mmerogwa nyinyi?

Leo ati kwa ujasiri mnasimama; macho meupe tena makavu, mnasema ati mnataka maelezo ya kina kuwa nini kimetokea ATCL! Ati mnaomba maelezo kutoka kwa watu wale wale ambao wanatakiwa wawe Keko wakiwa na pingu katika miguu na mikono yao. Leo mnakaa meza moja na mafisadi mliowaweka hapo, mkitumaini watawaambia kitu kingine zaidi ya kutaka fedha zaidi! Ati mmewapa siku saba za kujieleza! Maelezo gani zaidi ya kuangalia ndege zenu zisizoruka kama tai aliyekatwa mbawa!

Kama vile wasio na akili timamu wanakuja mbele yenu na suti zao za bei mbaya na kuomba fedha zaidi kuwa kinachohitajika ni fedha zaidi! Katika hali yenu ya kurogwa (bewitched state) mnakaa na kufikiria kuwapa fedha zaidi ili kulinasua shirika. Tutawapeleka hospitali gani nyinyi maana hata walioko Mirembe wanaweza wakawakimbia baada ya kuwauliza "ukichaa wenu umeanza lini"?

Badala ya kuamua kuchukua hatua za kushughulikia tatizo hili mnafanya kile ambacho ni kitendo cha woga kabisa; kwamba mnataka wachina waingie mkataba wa kuliendesha! kwamba ya Afrika ya Kusini hayakuwa funzo, ya Tanesco hayakuwa funzo, mnataka na ATCL mjaribu tena! Hivi katika taifa letu hakuna watu wenye uwezo kweli wa kuliendesha shirika hilo? Kweli mmekuwa waoga kushughulikia matatizo hadi tatizo likija mnakimbilia kwa "mjomba" Uchina, mmerogwa nyinyi?

Mnataka kutuambia kuwa mmeshindwa kukaa chini na kugonganisha vichwa vyenu kutafuta suluhisho la kitanzania kwenye tatizo la kitanzania? Hivi mnaogopa nini kufanya maamuzi magumu na kutoa nafasi kwa WAtanzania wazalendo wa kweli kuliendesha? NI ninyi wenyewe mlimrudisha David Mattaka licha ya kuwekwa nje ya utumishi, mlikuwa mnafikiria nini? Kwamba ATCL ni mahali pa mafunzo?

Katika wazimu wangu, nina uhakika tukitafuta watu wawili wa watatu wenye akili za biashara wanaweza kulitengeneza shirika hili na wenyewe wakatengeneza pesa vile vile. Tumeshindwa kuwaita wafanyabiashara wa Kitanzania, wasomi, na watalaamu wa mambo ya anga na kusema "tunaomba msaada tufanye nini"?

Kama mlivyokuwa goigoi kwenye wizi wa Benki Kuu, kama mlivyo goi goi kwenye suala la Elimu ya Juu (mmeunda kamati kuchunguza matatizo ya vyuo vikuu wakati mwaka mmoja mliopita mliunda kamati kama hiyo hiyo au hamkumbuki mlifanya hivyo?), kama mlivyo goi goi kwenye Jeshi la Polisi; kama mlivyo goi goi kwenye Usalama wa Taifa, mmekaa na kusubiri hadi vinuke kabisa ndiyo mnyanyuke! Mmerogwa na nani? Na ni kitu gani tunaweza kuwapa kikawazimua toka katika hali yenu ya bumbuwazi la ulozi?

Mnataka tuombe Bunge liunde Kamati Teule ichunguze ATCL? Msituambie kuwa sasa nchi yetu ianze kuongozwa na Kamati za Bunge maana hata la Dowans nusura mliingize Taifa mkenge licha ya kuwaambia tangu mwaka jana kuwa Dowans haikustahili kuchukua mkataba wa Richmond lakini katika kiburi chenu mkafanya hivyo.

Sasa hili la ATCL limedhihirisha tatizo liliopo. Mmezoea kubebana sana, mmezoea kuoneana haya sana, mmezoea kukenuliana meno kama fisi wanapoona mifupa!! Mmebakia kupigiana makofi!

Zindukeni katika usingizi wenu! Amkeni kutoka katika dimbwi la mshangao wenu, kwani hakuna hirizi itakayowazindua, hakuna ramli itakayowaamsha, hakuna mganga atakayeinua zindiko mlilojipigia wenyewe katika ufisadi wa matendo yenu. Na msitegemee kuchanjwa chale za kinga ya pingu zilizopo mbele zenu!

ATCL haihitaji kubinafsishwa, ATCL haina sababu ya kuitiwa wajomba zetu wachina kuja kuiokoa; ATCL haitaji wataalamu kutoka mbinguni na mabingwa wa utawala kutoka mbingu ya saba. Wamarekani wana msemo "you messed it up, you clean it up" kwamba "mmechafua wenyewe, safisheni wenyewe!". Hili mmelivundisha wenyewe, sasa linanuka mnauliza "kwanini linanuka"?

Labda mnahitaji kuombewa nyinyi; mnahitaji kupepewa; au kufukizwa kwa harufu ya maji yaliyochemshwa ya mwarobaini! au tumwombe Kakobe awawekee mikono! au Shehe aliyebobea katika mambo ya roho awasomee!

Au mwataka tuite mashehe waje wawasomee dua ya kuondoa majini mliyoyakumbatia, na tukawaombe wachungaji waje wakemee mapepo yenu ya ufisadi yaliyowapanda katika vichwa vyenu, labda...... labda... mtarudi kwenye akili timamu!

au mnatuonaje sisi Watanzania, tumerogwa?

labda nyinyi na sisi sote tumerogwa na hakuna wa kutusaidia!

Mwanakijiji, jitahidi upeleke huu mchango wako kwenye magazeti ya Tanzania, ni mchango mzuri sana ambao unaonekana kama ni wa kiwendawazimu lakini kwa Watawala "wendawazimu" wanaweza kuelewa na kusaidika.
 
Hongera Mwana kijiji kwa hoja hizi nzito,zimeikonga roho yangu,Mungu akubariki sana.
 
Hongera Mwana kijiji kwa hoja hizi nzito.Zimeukonga moyo wangu,Mungu akubariki sana.

Kwa maneno hayo ya Mchungaji naona anastahili kupata adhabu kama wanazopata wengine! Au Mods nimekosea?
 
Hii ni tabia ya uongozi kuona kila kitu kinachosemwa ni upinzani. Viongozi wanasahau kuwa hii nchi ni yetu sote iwe CCM, CHADEMA, CUF auwasio wanachama wa siasa. Inatia aibu kuona namna tunavyojilabu mbele ya dunia wakati serikali ikiendesha mambo kwa mtindo wa miaka 47. Si watendaji wa ATCL peke yao bali uongozi mzima wa Wizara ya Miundo Mbinu iende na Maji kama ilivyokuwa kwa wahusika wa Richmond. WALLAHI KWA HILI INAUMA SANA>
 
Back
Top Bottom