hivi kwa wale wanaokatwa deni, huwa wanakata bei gani kwenye kipato chao/chenu!! mimi nami ni mnufaika na mkopo na ninadaiwa LOL
Asilimia 8% ya kipato chako cha kila mwezi
kipatao!!!! okay kabla au baada ya Kodi mkuu!!
Nafikiri HELSB ina watu wasiojua kazi. Haitoshi kuweka majina tu wanatakiwa kuweka na kiasi. Halfu kila siku katika mkataba wa mkopo kunatakiwa kuwa na makubaliano ya mkopo. Ukiangalia kuanzia 2005 kurudi chini sheria inayounda HELSB haikuwepo. Nina hakika kabisa kuwa kama watawafanyia vurugu watu wote waliomaliza chini ya 2005, basi wanasheria wanaweza kuwabuluza mahakamani na kujikuta wanashindwa.
1. Huwezi kuweka sheria ikaanza kutumika restrospectively, ni lazima itumike pale inapoanzia
2. HELSB haina mamlaka ya kuwadai waliokopeshwa kabla ya 2005, hiyo ni dhamana ya wizara ya elimu ya juu wakati
3. wanatakiwa kuwakilisha form ya mkataba mahakamani kati ya HELSB na mwanafunzi. hivyo watakuwa hawana.
HELSB inatakiwa kutumia busara sana kuwadai wanafunzi wote wa chini ya 2005. Wakitumia vitisho wanakaribisha legal challenges.
Kabla ya kodi
Kweli mzee, nafikiri ingekuwa vizuri kama wangeandika na kiasi pia. Mimi nilikuwa ile intake ya kwanza ya mwaka 1994/95. Sincerely sikujua kama nadiwa mpaka about two years ago walipo publish majina gazetini. Nilijaribu kutuma e-mail kuwaulizia lakini hakuna mtu anajibu pale.
Kama wanataka kuwashtaki watu wote hao basi gharama za kesi zitakuwa ni kubwa kuliko hata wanazodai. Vilevile inawezekana kesi zikawabadilikia ikabidi wao ndiyo walipe fidia mwishoni, maana miaka ile ya 94/95 sidhani kama kulikuwa na sheria hiyo ya mikopo na wala bodi haikuwepo!!
mtoa maada, ile list imeandikwa tu, wala haijachujwa, wengi tunalipa na majina bado yamo!