Watanzania wawili wakamatwa na madawa ya kulevya Hong Kong

Wala usiwe na shaka, kuwataja tu haitoshi na hatua zinazostahiki zitachukuliwa. Subiri, ujuwe watu wa unga ni watu hatari sana, kuna nchi mpaka wameingia mwituni wanapigana na Serikali zao, inatakiwa uwe na akili kuyajuwa hayo. Vita na wauza unga ina hasara zake na faida zake ni lazima utumie mbinu za hali ya juu na si kukurupuka tu, utadondokea pua.

Na kama nilivyoeleza hapo juu, Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete si mtu wa kukurupuka, ni mtu ambae yupo "organized" anafanya mambo yake kwa kupanga na kwa umakini mkubwa sana. Hilo usiwe na shaka nalo.

Nimenote point muhimu: Madawa ya kulevya yana faida na hasara zake....ndio maana Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete anashughulikia mambo haya kwa umakini mkubwa. Umesomeka Faiza Foxy
 
Mimi naona nao hao wachina ni corrupt tu unakamata watu hutaji majina manake nini,waweke majina ya hao wahalifu hadharani ili tuwajue si kama hivi wanavyojenga mazingira ya sintofahamu zaidi na nia ovu ya kumalizana kimyakimya kwa style ya prince Rz1,huu ni ushenzi mwingine wamwage vitu hadharani kama wasouth walivyofanya kwa kina masogange.Hizi ni dalili kwamba hao wabongo walibebeshwa mizigo ya madrug lords wa huko ambao wana nguvu kubwa kwenye serikali yao.
 
wadau embu tembeleeni hapa muone haya majanga juu ya vijana wetu2013

Hii kitu imenishtua sana kaka kumbe hali ni mbaya saaana. Ni kwa nini serikali isiwe na vipindi maalum vinavyoelezea madhara ya kutumia na kusafirisha madawa kwa kutumia mifano halisi ili vijana wengine wasijaribu kufanya hivyo?
 
Matola mambo ya madude unayajulia wapi? wewe ni mtu wa kutumiwa na umezoea kubebeshwa mikoba angalia sana; utabebeshwa madude mjini hapo!
cc Ritz
 
Last edited by a moderator:
Utajuaje kama hao unaotarajia waendeshe vipindi hivyo ndio hao hao wadau ya maafa haya? Very complicated
 
Nimenote point muhimu: Madawa ya kulevya yana faida na hasara zake....ndio maana Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete anashughulikia mambo haya kwa umakini mkubwa. Umesomeka Faiza Foxy

Umesoma lakini unaonesha ni finyu mu kichwa, hujaelewa au unajifanya hayawani.
 
Hii pia inawezekana ila kumbuka pia huu mchezo haujaanzwa sasa na vijana wa Tanzania. Toka mwishoni wa miaka ya 80 katika utawala wa Mwinyi huu mchezo ndiyo ulishamiri sana na kuna vijana wengi tu wa Kitanzania waliofungwa Italy, Uturuki, Ugiriki, Japan, China, na nchi za Scandinavian, na pia kuna walionyongwa huko Pakistan il ndugu na jamaa hapa Tanzania hawajuwi. Serikali inafahamu ila kwa makusudi hawataki kuonya watu kwa sababu kuna vigogo ndani ya huu mchezo. NI kitu kinachofahamika kwani huwezi kamwe kusafiri na unga kiasi kile bila kukamatwa. Serikali fanyeni uungwana, mnaua vijana wetu bila huruma.

Mi nakubaliana nawe 100%. Tuzungushe tukatae, lakini Watz hasa vigogo wametufikisha mahali ni aibu. Serikali iliyoko madarakani ndio wahusika, halafu sisi wananchi tulivyo mambulula tunaitaka serikali iwataje wahusika na uuzaji hayo madawa, inawezekana kweli? Ila Tuisihi serikali iachane na zahama hii ya aibu, iwaonee huruma vijana tuondokane na AIBU hii
 
Matola mambo ya madude unayajulia wapi? wewe ni mtu wa kutumiwa na umezoea kubebeshwa mikoba angalia sana; utabebeshwa madude mjini hapo!
cc Ritz
Mkuu chama,

Type kama kina Matola, wengi wameisha Guangzhou, Qian Daohu, Macao, kwa kubebeshwa sembe.

Wanadanganywa sana hawa.

Huyu anaweza kubebeshwa sembe bila hata kujijua.
 
Last edited by a moderator:
Wala usiwe na shaka, kuwataja tu haitoshi na hatua zinazostahiki zitachukuliwa. Subiri, ujuwe watu wa unga ni watu hatari sana, kuna nchi mpaka wameingia mwituni wanapigana na Serikali zao, inatakiwa uwe na akili kuyajuwa hayo. Vita na wauza unga ina hasara zake na faida zake ni lazima utumie mbinu za hali ya juu na si kukurupuka tu, utadondokea pua.

Na kama nilivyoeleza hapo juu, Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete si mtu wa kukurupuka, ni mtu ambae yupo "organized" anafanya mambo yake kwa kupanga na kwa umakini mkubwa sana. Hilo usiwe na shaka nalo.

Maajabu haya,Radhia Sweety katoweka ghafla JF bila kuaga mara umeibuka FaizaFoxy?Ni ajabu kuona mawazo yenu yanafanana hivyo.Is it a coincidence?
 
Kuna watawala ndani ya utawala wa Kikwete watakuja kupelekwa mahakamani aidha kwa machela ama kwa kujikongoja wenyewe kwa kutingwa na maradhi ama uzee. Sasa hivi wanaimba na kufurahi kwa maovu wanayotenda lakini siku yaja watajikuta wakiwa na waliosongwa na dhiki kuu.
 
Kweli hii ni aibu, tunayoisifia kwa utulivu na amani kumbe ni maharamia wa kununua na kuuza unga wa kulevya.
Sasa hivi biashara imeshika kasi na nguvu mpya, maana nchi za wenzetu hawana masihara wanapigana vita vya ukweli na kupinga ununuaji na uuzaji wa madawa ya kulevya. Serikali yetu imeyanyamazia matukio haya ya aibu inaelekea wanahusika kwa namna moja au nyingine kulinda biasharaa hii kwa manufaa ya wachache waliko madarakani. Chonde chonde waheshimiwa taifa linaangamia!!!.....
 
Kuna umuhimu sheria ikaingizwa kwenye katiba kabisa juu ya hili suala la madawa ya kulevya.
Kitu kimoja sijaona majina katika hii taarifa. Pronoun tu ndo zimetumika. Kulikoni? Kaka ataenda Hong Kong mda si mrefu litaisha na hili.


Watanzania wawili wamekamatwa na madawa ya kulevya yenye thaman ya Dola za marekani million 3.34.

Mtu mmoja jana alisema sasa hivi wasafiri watokao Tanzania wanakaguliwa kwa makini zaidi ya ilivyokuwa hapo awali kutokana na matukio ya kukamatwa na dawa za kulevya! Hii ni sifa mbaya mno kwa raia na Taifa zima!

Iliyopachikwa hapo chini ni taarifa kutoka kwenye tovuti ya Serikali ya Hong Kong ya Julai 26, 2013


499076.jpg


6220121.jpg


4733281.jpg



5643847_orig.png


Hong Kong Customs yesterday (July 25) detected three drug trafficking cases, with seizures totally valued at $4.78 million, in the department's escalated anti-narcotics efforts to combat drugs.

Customs officers at the Hong Kong International Airport (HKIA) intercepted a 26-year-old incoming male passenger arriving from Tanzania for clearance yesterday afternoon and seized 1.6 kilogrammes of heroin concealed in two false compartments of his hand carry briefcase. The drugs would fetch a value of about $1.28 million.

Later in the evening, Customs officers at the HKIA intercepted another 45-year-old man from Tanzania for clearance. On suspicion of concealment of drugs inside his body, the suspect was escorted to hospital where he discharged 204 grammes of heroin after staying for one day. The value of the drugs was about $0.16 million. The suspect is still in the hospital.

In the same evening, Customs officers intercepted a 28-year-old man at a carpark in Tai Kok Tsui. Approximately 2.03 kg of cocaine camouflaged as snacks were found inside a plastic bag carried by him.

Customs officers later escorted the suspect to a domestic flat nearby for a search and seized 1 kg of cocaine and 290 grammes of crack cocaine there. The total value of the seizure was about $3.34 million.

A Customs spokesperson said today (July 26) that all three suspects in the three cases were arrested for drug trafficking. The cases are still under investigation.

Under the Dangerous Drugs Ordinance, drug trafficking is a serious offence. The maximum penalty is life imprisonment and a fine of $5 million.


Ends/Friday, July 26, 2013
Issued at HKT 23:43

NNNN
[/COLOR]



[h=2]ISEMAVYO SHERIA YA HONG KONG UKIKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA[/h]


598618_orig.png



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Pamoja na madudu wayafanyayo wa-tz ila nahisi kuna kamchezo mchafu unachezwa..!!
Nahisi kama kuna watu wana passport za Tanzania, ilihali wao si watanzania. Hii sio bure...

Kwa maana hiyo mkuu Masongange & Co ni wanyarwanda na si watz?
 
Hili tatizo la madawa ya kulevya ni la kimataifa. Dawa zinatengenzwa sehemu mbali mbali za dunia, Tanzania ni soko na njia kama ilivyo nchi zingine. Mara nyingi inakuwa ni network ya hali ya juu, ikhusisha watu wakubwa wa serikali za nchi zetu. Kigugumizi cha viongozi wetu kina sura nyingi na tafsiri nyingi.
 
Huu Mtandao ni mkubwa wa ajabu.....End of the day muathirika zaidi ni wazazi na yule innocent mbebaji !! (kama atapona)
 
Back
Top Bottom