Watanzania Watakiwa Kujiongeza

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
Wahimizwa kufanya kazi kwa kasi ya Dk Magufuli

WAHITIMU wa kozi mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Tumaini, Makumira tawi la Mbeya, wametakiwa kuendana na kasi ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa wabunifu na wenye kutekeleza majukumu yao kwa tija zaidi.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Profesa Esther Mwaikambo alisema hayo kwenye mahafali ya kwanza kwa tawi hilo na mahafali ya 13 kwa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira.

Alisema watu wengi wamekuwa wakizungumzia falsafa ya ‘Hapa Kazi Tu’ ya Rais John Magufuli, lakini ni wachache wanaoitekeleza falsafa hiyo kwa kuendana na kasi ya mwenye nayo.

Alisema ni wakati kwa wasomo wakiwemo wahitimu hao kuiishi falsafa ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa kutokuwa watu wazembe, wenye kutanguliza lawama, bali wenye kuonesha utofauti kiutendaji.

“Mnapaswa mdhihirishe ubora wa kuhitimu kwenu kwa kuboresha maisha yenu ya ya jamii inayowazunguka kupitia utendaji kazi wenu mzuri. Hii itasaidia pia kuonesha utofauti wa vyuo kati ya mlichohitimu ninyi na wanavyohitimu wengine.

“Mkawe mwanga wa jamii mkijiheshimu na kuwaheshimu wengine. Mkifanya hivyo na wao watawaheshimu kwa kuwa mtaonekana sawa na mshumaa uliowashwa na kusaidia wengine kuona gizani,” alisema Profesa Mwaikambo.

Mwenyekiti huyo pia aliwasihi wahitimu hao, kupenda kujiendeleza kimasomo akisema hiyo ni njia pekee ya kuboresha utendaji kazi wao badala ya kuishia katika hatua waliyofikia na kuona huo ndiyo mwisho wa elimu.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Tumaini Makumira, Mchungaji Profesa Joseph Parsalaw aliwataka wasomi nchini kuzichangamkia fursa zitokanazo na utandawazi na uwepo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Chanzo; Habarileo Wahimizwa kufanya kazi kwa kasi ya Dk Magufuli
 
Back
Top Bottom