Watanzania wana uelewa mdogo kuhusu Pension Fund, 25% ni maamuzi sahihi

Maelezo mengi hayasaidii. Ksa kuwz fedha zinazohifadhiwa kwenye mifuko hii ni za wanachama zilizokatwa kutoka kwenye mishahara yao, mtumishi akistasfu apewe fedha zake zote na serikali isijibebeshe jukumu la kulea wazee wastaafu kupitia mafao yao.

Kingine ni kwamba, serikali imekuwa ikizitumia fedha za mifuko hii ipendavyo ikiwemo kukopa na wakati mwingine fedha hizi kutumika kwenye uwekezaji wa kujenga miradi ya kiuchumi mfano majengo ya kupangisha, na sasa inajenga viwanda vya sukari wakati wanachama wrnye fedha zao hawanufaiki na fauda inayotokana na uwekezaji huo wala mifuko haiingii makubaliano yoyote ya kugawana gawio na walioweka fedha zao. Huu ni wizi na hili halikubaliki.

Tunataka mwanachama awe na sauti na fedha zake na siyo serikali ndiyo iwe na sauti na fedha za mtu halafu impangie inampa kissi gani au atumieje.
 
Huo utaratibu upo toka zamani hapa Tanzania Mtu akifarika wale warithi au beneficiary wanalipwa kwa mkupuo lumpsum, Halafu kidogo kidogo kwa miaka mitatu mwisho, ndio maana nimesema Tanzania uelewa ni mdogo Sana Mkuu, Huu utaratibu upo kitambo sana
unajua we ndio hujielewi na hata hujui unacho kitetea? hebu fanya kurudi ukasome vizuri watu wanacho kilalamikia ndio uje na utetezi wako, sio unalazimisha Watanzania wote hatuna uelewa wakati wewe ndio hauna uelewa na hujielewi.
 
Wewe huna ulijualo.
Ivi ukipewa milioni 100 ndo unajua umefika.
Waulize Maprofesa kwanini wamekubali kuingeozewa miaka ya kustaafu.
Miaka yote ya nyuma hao wafanyakazi wastaafu walikuwa wanachukua pesa yao yote, je umewafuatilia maisha yao japo miaka mitatu tu baada ya kustaafu ?
Mimi nina uhakika nitaishi miaka mingi baada ya kustaafu.
Kama wewe unaugonjwa usiokuwa na tiba shauri yako.
Wewe nakuona fala tu, kama huna mipango ya maisha ndiyo ukipewa 100m itakuzuzua.Hao maprofesa kama wamekubali kuongezewa miaka basi hawajajipanga kuishi nje ya ajira. Hela yangu mwenyewe unipangie jinsi ya kutumia, huo ni uzwazwa, na wewe unatetea kitu usichokijua, sisi tunajua kanuni hii imewekwa kuihami Serikali kwani ndiyo imekausha mifuko hiyo kiasi inakosa uwezo wa kuwalipa wastaafu stahiki zao.
 
Mwandishi wa hii mada wewe si mwakilishi wa Wastaafu hata kidogo na umetoa sentensi ya mkumbo mno wa UELEWA wa Watanzania wote milioni 55-plus - sijui umeupimaje! Mbona hukuja kunipangia matumizi ya mshahara wangu aliokuwa unabaki baada ya kukatwa mchango wa mfuko niliokuwa ninachangia kwa nguvu ya sheria? WEWE siyo mwathirika wa maamuzi yaliyofanywa, tafadhali achana na hili suala. Sisi wastaafu ambao kwa miezi zaidi ya 10 tangu tusataafu na hatujalipwa CHOCHOTE utatuambia maneno gani tukuelewe hata kama una PhD ya mafao ya Mifuko ya Pensheni? Kumbuka, "An Empty Stomach Has No Wisdom". Sisi tunataka haki yetu. Sisi ni kundi dogo lisilo na mahali pa kugomea, pa kuandamania nk. tunateseka KWELI wakati fedha zetu zilikatwa kwenye mishahara - TAFADHALI ACHA MASIHARA, unagusa maisha ya watu wenye DHIKI, wanaoishi kwa kujificha kwa sababu ya madeni na hawakopesheki tena!
 
Tundu lisu ameelezea kuwa mifuko haina pesa, Hajaongea uhalisia Mfano PPF iliambiwa ianze kulipa wastaafu Wa zamani wa serikali ambao wengi hawakuchangia ,

PPf ilirithi Deni ambalo sio lake, na Hata baadhi wanaoliopwa hawakuchangia kwani mfumo haukuwaruhusu, wengi wastaafu Wa miaka ya 1994 kurudi Nyuma walikuwa hawachangii lakini Sasa wanalipwa kupitia PPf imerith deni

Tundu lisu amelisema Hilo?

Mwambie aliyekutuma tumekustukia. Mlaaniwe milele na milele.
 
Wana JF, Mambo ya 25 percent ya Pension yameongelewa sana humu ndani na kundi Fulani likilaumu serikali. Je watu wanauelewa na elimu ya Mafao (Pension)?

Je watu wanafahamu misingi ya uendeshaji mifuko ya pension jinsi inavyopata faida na hasara?

Kuna aina ngapi za pension? na ni vihatarishi gani hii mifuko inakumbana nayo ili iendelee kulipa wastaafu?

Majibu ya hayo maswali yataondoa utata na watu hawatailaumu serikali bali wataipongeza sana sana

Mosi, Serikali imepitisha sheria kuwa Mtu atalipwa 25 percent kwa mkupuo yaani ( lump sum). Halafu baadae Mtu ataanza kulipwa kidogo kidogo yaani periodical payment kwa 75 percent tunaita (Annuities)

Mode of Operations
Katika Pension funds kulipa annuities au periodical payments yaani kulipa kidogo kidogo hiyo 75 percent ni hasara kubwa sana endapo hao wastaafu wataishi miaka mingi zaidi ya makadirio, Mara nyingi mtu akistaafu hukadiriwa ataishi chini ya miaka 15 na atafariki. Commitment ya mifuko hii wamekadiria hivyo

"Longevity situation "Hii ni hali ya mabadiliko ya kimaisha ambayo imeonyesha maisha ya wanadamu yanazidi kuboreka zaidi hasa Katika kupambana na Magonjwa, Hivyo watu wengi wataishi maisha marefu sana kwa utafiti uliofanyika ( long life). Mifuko hii hapa tayari imejiiingiza kwenye hasara mpya itokanayo na longevity risk, kitendo cha kukubali kulipa 75 percent kwa kidogo kidogo wanaweza mlipa Mtu kwa Muda mrefu zaidi hivyo hasara

Moral harzad situation, Tafiti nyingi hapa Tanzania zimeonyesha watu wanatumia vibaya uwepo wa hizi faida zitokanazo na Pension fund, Wanaishi maisha hatarishi ya kuvuta sigara, kutofanya mazoezi na kutumia pesa hovyo wakitegemea Pension watapata kwa mkupuo ,Moral hazard situation ni hali ya Mtu kuishi visivyo au hovyo akitegemea pension ipo, kungekuwa hakuna pension asingeishi maisha ya hatari.

Kudhibiti hali hii ya Moral hazard ni bora ukampa mpatia Mtu 25 percent ili ajidhibiti mapema Kama mkupuo, Kumpa 75 percent kwa mkupuo kuna weza mtokea puani akidhani maisha ameyapatia kumbe ndio kifo chake mapema

MUUNDO WA UWEKEZAJI

Mifuko ya Pension uwekezaji wao mkubwa ni kwenye amana za serikali yaani "long term treasury bond na short term treasury bills, Inategemea ipate faida toka uwekezaji huu wa serikali ambayo wengi mnafahamu riba yake ni ndogo sana sana

mifuko hii kuna muda inaamua kuwekeza kwenye riba za mabenki za biashara hapa namaanisha fixed deposit, Lakini uwekezaji kwenye mabenki bado wanatakiwa kulipa kodi (withholding tax) kwenye riba wanayopata hivyo kipato kinapungua tofauti na makadirio

UELEWA MDOGO KWA WATANZANIA
Africa ya kusini Mtu anachagua mwenyewe fedha yake ya pension iwekezwe Sehemu gani, Africa ya kusini Mtu anaweza tumia pesa yake ya pension Kuweka dhamana ya mkopo au kununua nyumba dhamana ikiwa ni michango yake ya pension

Hapa Tanzania elimu ya Pension fund ni ndogo sana sana, Serikali inachofanya siyo kibaya tatizo hawajatoa elimu kwa watu

Aina za kuchangia zipo nyingi sana, Serikali yetu inaamua kutumia mfumo wa pamoja unaoitwa "Defined Benefit Plan "Huu mfumo ni mzuri kuwa watu tunachangia kwenye pool moja Mfano Nssf au Psssf, halafu toka kwenye Pool ndio maamuzi yanafanywa hii huleta usawa kidogo kwani kunakuwa na mfumo mmoja wa kupiga hesabu wa pension

Hasara za mfumo wa "Defined Benefit plan "hujui michango yako inawekezwa wapi na faida gani imepatikana, Hapa ndipo serikali ilibidi itoe elimu kwa Raia

Mfumo wa pili ambao Afrika ya kusini wamewapa Raia wao unaitwa "Defined contribution Plan "Huu mfumo unachangia kwenye pool moja lakini Kila Mtu anakuwa na akaunti yake inafunguliwa, na Raia Kila wakati anajua kiasi gani kimewekezwa na faida yake kiasi gani, Raia anaweza toa maelezo kwa mfuko pesa yake itumike vipi?

Mwisho, Kuna mabadiliko makubwa Sana Duniani kuanzia kwenye udhibiti wa Pesa mpaka mifuko ya Pension, Wataalamu wetu lazima wajifunze na kukubali mabadiliko, kuna mambo ya virtue currency BItcoins n. k, Wataalamu wajifunze wasikae kuzuia tu

Naipongeza Serikali kwa maamuzi haya ya 25 percent na 75 percent tatizo hawajatoa elimu ya kutosha

Je? Kipi muhimu wazee wetu kulipwa pesa kwa mkupuo nyingi kwa Mara moja au Walipwe kidogo kwa mkupuo halafu Kila mwezi Walipwe pension nyingi

Lengo la sheria kwa Sasa ni kuwafanya wastaafu waishi Kama wapo kazini Kila mwezi wapokee pension kubwa kuliko wanavyoishi Sasa wengi walipata kwa mkupuo halafu Kila mwezi wanaumia

JE WATOA SERA NA WATUNGA SERA WETU WANA UELEWA MPANA KUHUSU MAMBO YA PENSION?

JE UTAFITI WA KUWA WATANZANIA WANAISHI MUDA MREFU BAADA YA KUSTAAFU NI SAHIHI ?

Tutazidi kuelimishana zaidi na zaidi kwenye ishu ya Pension na Bima zote lengo ni kutoa Cover au Kinga kwa wachangiaji,Pia Serikali itoe elimu zaidi kwa wachangiaji
life span yetu ni ndogo
 
Tatizo hamjaelewa lengo la serikali

Mabadiliko ya hii sheria imeanza mchakato toka kipindi cha kikwete,

Maoni na Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu maisha ya wazee baada ya kustaafu

Asilimia kubwa ya wazee walipokea pension ya mkupuo Mara moja zinaisha haraka wanaishia kutanga tanga wakisubiri pension ya Kila mwezi ambayo ni kidogo sana

Sasa serikali imeona bora Mzee apokee pension kubwa ya Kila mwezi halafu ya mkupuo iwe kidogo

Wanataka Mzee aishi maisha ya Kila mwezi Kama yupo kazini ndio lengo la sheria hii

Watu wengi wanafikiri imekuja ghafla hii sheria, Sheria ya awali wazee wengi wa zamani imewaumiza ukiwaona Leo Hata kula na kuvaa shida, Angekuwa anapokea Kila mwezi let say laki nane au 800,000 kidogo nafuu kuliko Kumpa laki 250,000
unaweza kudhani una akili kumbe ni mbumbumbu mzungu wa reli !
 
Pesa yangu mwenyewe,naichangia kwa jasho langu miaka takribani 30+ bado tena unipangie namna ya kuitumia??Pumba****vu!Najua hili litawaathiri wastaafu katika utawala huu dhalimu ,lakini nina imani Mungu atasaidia hii sheria itakuja kubadilika tu!Huu ni unyonyaji wa waziwazi kabisa!!

Sent from my HUAWEI VNS-L21 using JamiiForums mobile app
 
Wana JF, Mambo ya 25 percent ya Pension yameongelewa sana humu ndani na kundi Fulani likilaumu serikali. Je watu wanauelewa na elimu ya Mafao (Pension)?

Je watu wanafahamu misingi ya uendeshaji mifuko ya pension jinsi inavyopata faida na hasara?

Kuna aina ngapi za pension? na ni vihatarishi gani hii mifuko inakumbana nayo ili iendelee kulipa wastaafu?

Majibu ya hayo maswali yataondoa utata na watu hawatailaumu serikali bali wataipongeza sana sana

Mosi, Serikali imepitisha sheria kuwa Mtu atalipwa 25 percent kwa mkupuo yaani ( lump sum). Halafu baadae Mtu ataanza kulipwa kidogo kidogo yaani periodical payment kwa 75 percent tunaita (Annuities)

Mode of Operations
Katika Pension funds kulipa annuities au periodical payments yaani kulipa kidogo kidogo hiyo 75 percent ni hasara kubwa sana endapo hao wastaafu wataishi miaka mingi zaidi ya makadirio, Mara nyingi mtu akistaafu hukadiriwa ataishi chini ya miaka 15 na atafariki. Commitment ya mifuko hii wamekadiria hivyo

"Longevity situation "Hii ni hali ya mabadiliko ya kimaisha ambayo imeonyesha maisha ya wanadamu yanazidi kuboreka zaidi hasa Katika kupambana na Magonjwa, Hivyo watu wengi wataishi maisha marefu sana kwa utafiti uliofanyika ( long life). Mifuko hii hapa tayari imejiiingiza kwenye hasara mpya itokanayo na longevity risk, kitendo cha kukubali kulipa 75 percent kwa kidogo kidogo wanaweza mlipa Mtu kwa Muda mrefu zaidi hivyo hasara

Moral harzad situation, Tafiti nyingi hapa Tanzania zimeonyesha watu wanatumia vibaya uwepo wa hizi faida zitokanazo na Pension fund, Wanaishi maisha hatarishi ya kuvuta sigara, kutofanya mazoezi na kutumia pesa hovyo wakitegemea Pension watapata kwa mkupuo ,Moral hazard situation ni hali ya Mtu kuishi visivyo au hovyo akitegemea pension ipo, kungekuwa hakuna pension asingeishi maisha ya hatari.

Kudhibiti hali hii ya Moral hazard ni bora ukampa mpatia Mtu 25 percent ili ajidhibiti mapema Kama mkupuo, Kumpa 75 percent kwa mkupuo kuna weza mtokea puani akidhani maisha ameyapatia kumbe ndio kifo chake mapema

MUUNDO WA UWEKEZAJI

Mifuko ya Pension uwekezaji wao mkubwa ni kwenye amana za serikali yaani "long term treasury bond na short term treasury bills, Inategemea ipate faida toka uwekezaji huu wa serikali ambayo wengi mnafahamu riba yake ni ndogo sana sana

mifuko hii kuna muda inaamua kuwekeza kwenye riba za mabenki za biashara hapa namaanisha fixed deposit, Lakini uwekezaji kwenye mabenki bado wanatakiwa kulipa kodi (withholding tax) kwenye riba wanayopata hivyo kipato kinapungua tofauti na makadirio

UELEWA MDOGO KWA WATANZANIA
Africa ya kusini Mtu anachagua mwenyewe fedha yake ya pension iwekezwe Sehemu gani, Africa ya kusini Mtu anaweza tumia pesa yake ya pension Kuweka dhamana ya mkopo au kununua nyumba dhamana ikiwa ni michango yake ya pension

Hapa Tanzania elimu ya Pension fund ni ndogo sana sana, Serikali inachofanya siyo kibaya tatizo hawajatoa elimu kwa watu

Aina za kuchangia zipo nyingi sana, Serikali yetu inaamua kutumia mfumo wa pamoja unaoitwa "Defined Benefit Plan "Huu mfumo ni mzuri kuwa watu tunachangia kwenye pool moja Mfano Nssf au Psssf, halafu toka kwenye Pool ndio maamuzi yanafanywa hii huleta usawa kidogo kwani kunakuwa na mfumo mmoja wa kupiga hesabu wa pension

Hasara za mfumo wa "Defined Benefit plan "hujui michango yako inawekezwa wapi na faida gani imepatikana, Hapa ndipo serikali ilibidi itoe elimu kwa Raia

Mfumo wa pili ambao Afrika ya kusini wamewapa Raia wao unaitwa "Defined contribution Plan "Huu mfumo unachangia kwenye pool moja lakini Kila Mtu anakuwa na akaunti yake inafunguliwa, na Raia Kila wakati anajua kiasi gani kimewekezwa na faida yake kiasi gani, Raia anaweza toa maelezo kwa mfuko pesa yake itumike vipi?

Mwisho, Kuna mabadiliko makubwa Sana Duniani kuanzia kwenye udhibiti wa Pesa mpaka mifuko ya Pension, Wataalamu wetu lazima wajifunze na kukubali mabadiliko, kuna mambo ya virtue currency BItcoins n. k, Wataalamu wajifunze wasikae kuzuia tu

Naipongeza Serikali kwa maamuzi haya ya 25 percent na 75 percent tatizo hawajatoa elimu ya kutosha

Je? Kipi muhimu wazee wetu kulipwa pesa kwa mkupuo nyingi kwa Mara moja au Walipwe kidogo kwa mkupuo halafu Kila mwezi Walipwe pension nyingi

Lengo la sheria kwa Sasa ni kuwafanya wastaafu waishi Kama wapo kazini Kila mwezi wapokee pension kubwa kuliko wanavyoishi Sasa wengi walipata kwa mkupuo halafu Kila mwezi wanaumia

JE WATOA SERA NA WATUNGA SERA WETU WANA UELEWA MPANA KUHUSU MAMBO YA PENSION?

JE UTAFITI WA KUWA WATANZANIA WANAISHI MUDA MREFU BAADA YA KUSTAAFU NI SAHIHI ?

Tutazidi kuelimishana zaidi na zaidi kwenye ishu ya Pension na Bima zote lengo ni kutoa Cover au Kinga kwa wachangiaji,Pia Serikali itoe elimu zaidi kwa wachangiaji
Hata wewe hauna unachokijua kuhusu dhuluma iliyopo kwenye so called sheria ya hifadhi ya jamii.
 
.kuu umeona hatuna akili uandike upumbavu wako?
Wewe ni mbunge waziri au kaitbu wa wizara??
Ila Mungu yupo na anaona haya yote mnayofanya
 
Fedha nyingi za wastaafu zimeelekezwa kwenye uwekezaji usio na tija. mfano zile nyumba za NSSF za kigamboni zina tija gani mbali na hasara kubwa Shirika limeingia. Ki utaratibu kila mtumishi angeulizwa ni utaratibu gani angeupenda katika mafao yake kama walivyo watumishi uliowasema wa Afrika Kuusini. Huu ni udikteta uliotumika katika uamuzi huo.
 
Wewe nakuona fala tu, kama huna mipango ya maisha ndiyo ukipewa 100m itakuzuzua.Hao maprofesa kama wamekubali kuongezewa miaka basi hawajajipanga kuishi nje ya ajira. Hela yangu mwenyewe unipangie jinsi ya kutumia, huo ni uzwazwa, na wewe unatetea kitu usichokijua, sisi tunajua kanuni hii imewekwa kuihami Serikali kwani ndiyo imekausha mifuko hiyo kiasi inakosa uwezo wa kuwalipa wastaafu stahiki zao.
Sawa
Ila mimi napenda nilipwe asilimia 25 ya mafao yangu, halafu niendelee kulipwa asilimia 75 ya mshahala wangu kwa miaka yote ya maisha yangu.
Kama ningestaafu leo ningekuwa navuta zaidi ya m 1 kwa mwezi hadi nitakapo aga dunia.
Katu nisingekuwa ombaomba
 
Back
Top Bottom