Watanzania tunaingizwa kwenye mkenge mwingine wa eac!!

BRO EDDY

Member
Dec 6, 2010
22
3
Ndugu zangu wanajf,

Shirika la ndege Tanzania (ATC) lipo jamani au lah mbona liko kimya? Hii nchi imelogwa au? Wenzetu Kenya wanachangamkia jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) sisi vipi mbona serikali imelala haitoi hata muongozo kwa wananchi wake inabaki kuimba tu wimbo wa jumuiya hiyo kwenye vikao?

Wenzetu nchi jirani ya Kenya tayari wameleta mashirika yao mawili ya ndege JETLINK na FLY 540 ambayo imeanzisha route mpya za hapa nchini achilia mbali route zao za Nairobi to dar es salaam, Mwanza and Zanzibar.

Mashirika yetu yameshindikana hapa nchini ATC nayo ndio hoi, nayo itawekeza Kenya au?

Hatari ninayoiona Tanzania itamezwa na Kenya na hata nchi zingine zilizopo kwenye jumuiya hii, hali itakayopelekea tusifaidike kwa lolote bali nchi hizo zikawa zinafaidi na sisi tukawa wateja wao wakubwa kwenye bidhaa na huduma mbalimbali wanazozalisha.

Naomba kuwakilisha:nono:
 
JK+malawi+arrive+1.jpg
 
yan hata muongozo ukiletwa na hawa mafisadi wetu, utaletwa ambao ushachakachuliwa kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe! Yan hichi kikundi kidogo kinachotuongoza hapa Tz, kama hakitashikishwa adhabu hatutatoka kwenye mfumo huu wa CHUKUA CHAKO MAPEMA (a.k.a CCM)
 
Back
Top Bottom