Watanzania tulikanye bunge

Aug 31, 2011
35
27
WATANZANIA TULIKANYE BUNGE

WABUNGE ISHINI BEYOND YOUR POLITICAL PARTIES IDEOLOGIES. UTANZANIA KWANZA ITIKADI ZA VYAMA VYENU BAADAE. KWANI USHABIKI WA KIITIKADI UMELIGHARIMU TAIFA KWA MDA MREFU.SASA IMETOSHA.WAVUJAJASHO KARIBU WATAAMUA 2015.


TATHMINI NILIZO NAZO NA AMBAZO NAAMINI WATANZANIA WENGI TUNAZO.

KITI CHA SPIKA HAKIJATENDA HAKI KWA MDA MREFU NA KIMESHINDWA MAJUKUMU YAKE.

WABUNGE WAMESHINDWA KULITENDEA HAKI TAIFA HILI KWA SABABU YA MVUTANO WA KIITIKADI.


HOJA ZENYE MASLAHI NA TAIFA HAZIPITI KWA SABABU YA USHABIKI NDAKI NDAKI WA ITIKADI ZA VYAMA VYETU.


CCM- UWINGI WENU BUNGENI ILIBIDI IWE FARAJA YA WAVUJAJASHO WA TAIFA HILI. LAKINI KWA MDA MREFU UWINGI WENU UMEKUWA KARAHA KWA WAVUJAJASHO WA TAIFA HILI. FUMBUENI MACHO ACHENI KUWA WATETEZI WA DHULUMA. MAMBO MANGAPI WAVUJAJASHO TUNAONA HAYAPITI KWA SABABU YA UWINGI WENU.


NISEME TU KWAMBA NI ULIMBUKENI KUTUNISHIANA MISULI NDANI YA BUNGE NA KUJIONA WEWE NI ABOVE SHERIA ZA BUNGE, NI ABOVE SHERIA ZA NCHI. KWA SABABU WAHUNI WACHACHE WANAKULINDA NA WAMEKUHAKIKISHIA MAISHA BORA KINYUME NA MAISHA YA WALALAHOI WA TAIFA HILI.WEWE UNAYETETEWA NA KITI, KWA UPUUZI NDANI YA BUNGE. "TIME WILL TELL"

NA NISEME TU NI UJINGA KWA MBUNGE YEYOTE YULE KATIKA CHAMA CHOCHOTE KILE KUTOUNGA MKONO HOJA YA MBUNGE YEYOTE ALIYETOKA CHAMA CHOCHOTE ETI KWA SABABU YA UTOFAUTI WA ITIKADI WA VYAMA VYENU. YANAYOTOKEA BUNGENI TUNAYAONA LAKINI SISI NDIO TUTAKAO HUKUMU.


Kwa niaba ya watanzania ambao wala hawafahamu kuwa kuna mitandao ya kijamii, ni vema wabunge wote mlioko katika mitandao hii muisome taarifa hii na muwe mawakili kwa wabunge wa vyama vyote yani CCM,CDM,TLP,CUF, n.k


msingi mkuu wa hoja yangu, ni kwamba si sahihi kutowasaidia watanzania waliowengi kwa kutounga mkono hoja ambayo imetolewa na mbunge wa wa chama Fulani kwa sababu ya itikadi yake.


sisi kama watanzania haswa vijana. umefika wakati wa kuishi beyond our political part ideologies. tusiwe washabiki ndaki ndaki wa itikadi za vyama vyetu hata kama vyama vyetu havilitendei haki taifa letu. bunge letu limeshatafunwa na ushabiki ndakindaki wa kiitikadi. TUMEONA masuala mazuri yenye maslahi na wavujajasho wa taifa letu hayapiti bungeni sababu ya mvutano wa kiitikadi. baadhi ya wabunge wa vyama vyetu hawajawa liberal. endapo hoja imetolewa na mbunge wa chama fulani, wabunge wa vyama vingine wanashindwa kumuunga mkono kwa sababu tu eti ya kuona watampa umaarufu.

huu ni upumbavu ambao hautakiwi kuvumiliwa. mtu analeta hoja inayogusa uchumi wa watanzania. wabunge ulimbukeni wanaanza kujihami nani katoa hoja, kwa nini tusiwe chama chetu. wanashindwa kuunga mkono hoja kwa sababu ya upumbavu wa ushabiki ndaki ndaki wa itikadi. binafsi nachoshwa sana na muenendo wa bunge.


Niseme tu yangekuwa ni mamlaka yangu. Spika na naibu spika ningependa wajiuzulu kwa maslahi mema ya muenendo mwema wa bunge, na kama watanisikia au kuisoma taarifa hii naomba waitendee haki, hata kama hawataipata usalama wapelekeeni taarifa hii kwa maslahi mema ya taifa letu.


Lakini pia wabunge wote wa vyama vyote. Bungeni si mahala pa itikadi za vyama vyetu. Si mahala pa ukada wa vyama vyetu. Bungeni tuna itikadi moja kuu utanzania. Wabunge wa vyama vyote bebeni itikadi ya utanzania kwanza, ITIKADI ZA VYAMA VYENU BAADAE. Wabunge wote fanyeni kazi ya kibunge na si wabunge mfanye kazi ya kuitetea serikali.


Msipoisikia sauti hii kwa niaba ya wavujajasho ambao wako nyuma yangu kwa hoja hii. Subirini danger zone, wakati wa wavujajasho kuamua hatma ya nchi yao umefika.

UTANZANIA KWANZA, ITIKADI ZA VYAMA VYETU BAADAE.
Your young boy.
EMEKHA.
W.TOGETHER@YAHOO.COM
 
Back
Top Bottom