Elections 2010 Watanzania tujiandaeje kwa uchaguzi mkuu mwaka kesho?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Ninapokumbuka kwamba uchaguzi mkuu wa rais na wabunge utafanyika mwaka kesho,
naona ni vema tukashauriane mambo muhimu ya kujiandaa ili uchaguzi huo uwe wa mafanikio makubwa.Tena uwe huru na wa haki ya kweli.
 
Kwa uchaguzi kuwa huru na wa haki tunahitaji kwanza kabisa tume itakayokuwa huru na isiyo ya ki-CCM CCM. Pili UWT usiwe na jukumu lolote katika shughuli za kuhesabu kura.
 
Kushauriana labda kwenye strategy za kupata wabunge.

Rais mbona anajulikana tayari kwamba ni Kikwete tena! Labda kifo kiingilie kati, lakini nadhani hata kampeni ya urais hapo mwakani hazina maana; Zikifanyika itakuwa ni ufujaji wa pesa ambazo tunazihitaji kwenye shughuli nyingine nyeti kama kuboresha maabara kwenye mashule na mahospitali yetu.
 
Heshima mbele mkulu,kwa vile uchaguzi mkuu ndo huooo unakaribia mi nadhani ni vema vyama(hasa vyama vya upinzani) vikatumia muda uliobaki kwa ajili ya kufanya maandalizi ya uchaguzi wa mwakani(mikakati ya ushindi) badala ya kusubiri mwaka 2010 ufike na kufanya maandalizi ya zimamoto...Huu ni wakati wa kuanza kuangalia ni nani atagombea na kushinda kihalali(kukubalika kwa wananchi) na si wakati wa kuanza kukusanya hela za kutoa rushwa ili ushinde katika uchaguzi huo mkuu...Huu ni wakati wa vyama vyote vyenye nia ya kushiriki katika uchaguzi huo mkuu kufanyia kazi/kusahihisha makosa yote yaliyopelekea vishindwe katika chaguzi zilizopita...Vilevile huu ni wakati kwa CHADEMA kujiimarisha katika ngazi za mikoa,wilaya,tarafa,kata,vijiji na shina(kama ilivyo katika chama tawala CCM) ili kuleta upinzani na ushindani wenye uwiano tofauti na ilivyo sasa(Hii ni pamoja na kuandaa bajeti ambayo kipaumbele chake kitakuwa ni kuimarisha kama sio kuanzisha matawi ya wilayani na vijijini ambako ndiko wapiga kura wengi wapo) ,Pia ni wakati wa CUF kujiimarisha zaidi Tanzania bara kama ilivyojiimarsha PEMBA,lengo kama nilivyosema hapo awali ni kuwa na upinzani wa kisiasa wenye uwiano hasa bungeni na katika halmashauri za wilaya,miji,manispaa na majiji(maendeleo yatakuja kwa kasi ya ajabu mno)...Aidha ni wakati wa chama tawala CCM kukaa na kujisafisha ili kiwe safi(japo kiasi) kinapoingia katika uchaguzi mkuu wa mwakani,hapa nina maana kwamba CCM kiandae wagombea walio wasafi,wanaokubalika kwa wananchi na si wanaoingia madarakani kwa kutoa rushwa ama wale ambao wanasifika kwa kuwa na sifa maarufu ya UFISADI...Mwisho ni wakati kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi(NEC) na pia Bunge kukaa chini na kuifanyia marekebisho sheria ya uchaguzi ili kuepukana na malalamiko ya mara kwa mara ambayo ni matokeo ya mapungufu ya sheria hiyo(kama ilivyotokea katika uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini).Ni ushauri tu....Naomba kuwasilisha wakulu..Mbarikiwe sana
 
Umeongea busara tupu.Hata hivyo dalili ya chama chochote kushinda ni uchaguzi wa serikali za vijiji ambao utafanyika mwaka huu nadhani miezi ya octoba au november
 
Jamani samahani kwa kutofautiana na wachangiaji wa mada waliopita.
Ukweli ni kwamba hakutakuwa na uchaguzi wa haki na huru kama hatujabadilisha katiba. Katiba iliyopo sasa inaipa CCM nafasi kubwa sana ya kuendelea kutawala kimabavu kama inavyotawala sasa.

Uhuru wa kweli wa Mtanzania wa leo utapatikana tu kwa kubadilisha katiba, vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu.

Ndugu Makyao bila shaka aanza kuwaelimisha wachaga huko Moshi waanze kudai mabadiliko ya katiba ili wapate uhuru wao.
 
Tujiandae kuipokea CCM madrakani tena maana JK lazima atapita tena kwa kishindo kama kawaida yao.
kama ni mikakati vijijini ndo mkazo uwekwe angalau kupata viti vingi vya ubunge.

Ila ni mtihani mkubwa kwa mpinzani kuukwaa urais na sijui itakuwaje siku hili likitokea Tanzania!
 
Amani iwe nanyi.

Niafurahishwa sana na hoja hii iliyoanzishwwa na Makyao.

Kupata mabadiliko ya siasa kunahitaji sana watu waliandaliwa kiakili, kiroho na kimtizamo. Watanzania kiakili wanachoka haraka sana kufikiria na kjupamga mambo kimkakati

Kiroho wanaamini kabisa kuwa ikulu imeandaliwa kwa ajili ya CCM tu na ya kwamba chama kingine kikiingia ikulu yatatokea mauzauza ya kutisha sana. Na pengine huo wanauona kama mwisho wa Tanzania.

Kimtizamo: Watanzania wameandaliwa wawe watumwa. Mtumwa hajitawali, hatawali mali yake, hamtawali mtu mwingini wala hawezi kuishi bila kutawaliwa. Sidhani kama watanzania watathubutu maisha ya kutotawaliwa, kuibiwa, kunyonywa na kudnganywa kila siku na CCM. Hayo ndo maisha wanayapenda. Ili kuondoa hilo ni lazima mfumo wa elimu ubadilishwa kwanza na elimu inayomwandaa mtu kujiamini na kujitawala itolewe kwa wingi.
 
Kwa uchaguzi kuwa huru na wa haki tunahitaji kwanza kabisa tume itakayokuwa huru na isiyo ya ki-CCM CCM. Pili UWT usiwe na jukumu lolote katika shughuli za kuhesabu kura.

JASUSI,
Inaonekana kuwa unapendekeza upatikanaji wa tume ya uchaguzi ufanywe huru.
Nani achague tume sasa?
Ipo kazi.
 
Kushauriana labda kwenye strategy za kupata wabunge.

Rais mbona anajulikana tayari kwamba ni Kikwete tena! Labda kifo kiingilie kati, lakini nadhani hata kampeni ya urais hapo mwakani hazina maana; Zikifanyika itakuwa ni ufujaji wa pesa ambazo tunazihitaji kwenye shughuli nyingine nyeti kama kuboresha maabara kwenye mashule na mahospitali yetu.

Nadhani hakuna haja ya kumpiga muhuri wa ndio Rais Kikwete kwani wapiga kura ndo waamuzi.
 
Jamani samahani kwa kutofautiana na wachangiaji wa mada waliopita.
Ukweli ni kwamba hakutakuwa na uchaguzi wa haki na huru kama hatujabadilisha katiba. Katiba iliyopo sasa inaipa CCM nafasi kubwa sana ya kuendelea kutawala kimabavu kama inavyotawala sasa.

Uhuru wa kweli wa Mtanzania wa leo utapatikana tu kwa kubadilisha katiba, vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu.

Ndugu Makyao bila shaka aanza kuwaelimisha wachaga huko Moshi waanze kudai mabadiliko ya katiba ili wapate uhuru wao.

Suala la kama kuna haja ya kubadili katiba au laa, ni la watanzania wote na siyo la kufanywa kikabila.
 
Tujiandae kuipokea CCM madrakani tena maana JK lazima atapita tena kwa kishindo kama kawaida yao.
kama ni mikakati vijijini ndo mkazo uwekwe angalau kupata viti vingi vya ubunge.

Ila ni mtihani mkubwa kwa mpinzani kuukwaa urais na sijui itakuwaje siku hili likitokea Tanzania!
Kwa huko T/bara au Tanganyika mtapanga mikakati mpaka hewani na kupata wasikilizaji wengi tu ,lakini wananchi wa huko wakishapewa kofia upande wa khanga na bilauri la mvinyo basi yale yote mliokuwa mkiwamwagia katika viwanja vya mikutano na wao wakiserebuka kwa kufurahia sera zenu na kuziona ndio zenyewe wanayaeka upande na kuipigia kura CCM huku wakisema CCM ndo baba,ila naungana na wale wote wanaosema hakuna uchaguzi kama Katiba na tume hazikufanyiwa marekebisho.
 
Suala la tume huru au kubadili katiba ni madai ya upinzani .kama kisingizio chao kwa kushindwa vibaya katika chaguzi mbalimbali.Suala kubwa hapa kwa wapinzani ni kuueleza umma sera zao,matarajio yao na mikakati yao katika kuendeleza watanzania.pili lazima wawe watu wenye uwezo wa kujieleza.Mathalani baada ya kumfukuza akwilombe natambwe hiza CUF hana mzungumzaji wa kujenga hoja.Chadema wanao wazungumzaji wazuri na wanao mikakati mizuri na ni wepesi wa kutumia fursa pale CCM inapoteleza.Mrema amepoteza kabisa kipaji cha kuzungumza kila akihubiri huzungumzia alipokuwa naibu waziri mkuu na kujisifu tuu.Kwa mtaji huu SISIM itadumu
 
\
Alaa?
Wachambuzi wa siasa za TZ mwasemaje kuhusu hoja hizi za SAID?
 
Ninapokumbuka kwamba uchaguzi mkuu wa rais na wabunge utafanyika mwaka kesho,
naona ni vema tukashauriane mambo muhimu ya kujiandaa ili uchaguzi huo uwe wa mafanikio makubwa.Tena uwe huru na wa haki ya kweli.

Kwanini wana JF ambao wako nyumbani wasianze na wao kugombea viti vya ubunge sio kukaa kusema watu wanao jaribu nafasi zao kuleta mabadiliko after all Zitto kaonyesha its possible umri si tatizo sana.

Na nadhani mtu kama FMES hana weza pambana na mbunge yeyote katika hiyo nafasi kama ni hoja tu na ana muda wa kujipanga aende sehemu moja ambayo anaona mbunge ana faida kuliko kukaa nyuma ya migongo ya watu. Kinachoitajika kwa sasa ni challenge kushindwa si vibaya lakini sauti isikike kwamba tupo karibu mno kuliko wanavyofikiria.

CCM hawataleta mabadiliko inabidi ya letwe ata mkishindwa uchaguzi hila waele wazi kwamba kuna challenge za kweli sasa na kama CCM ni damu huu ndio muda wakuanza kupigana kuwe na wagombea binafsi au chama chochote chenye nguvu ya ku-challenge. Safari ya maili millioni moja uanza na atua moja bila kunyanyua mguu amna tunakosogea,vilevile maneno matupu ayavunji mfupa.

action speaks louder than words 'Exhaud Makayo' sijui utajipanga na jimbo gani. Uchaguzi wa Japan chama tawala akikutegemea kama kitashindwa baada ya almost half a century in power lakini wananchi walishachoka na viongozi wale wale ata opinion polls azikutegema mabadiliko especial ndio wenye hela, na watanzania nao wameshaanza kuchoka lakini jibu alitopatikana bila ya kujaribu sidhani watu kama wana-enjoy kulala giza wakati Lowassa kakimbia na hela yao kwa mkataba wa uongo.

Kujaribu si ...........
 
Tanzania hakuna uchaguzi kuna uchafuzi tu. endeleni tu na ngonjera lakini tume ya uchaguzi hata sikumoja hawatamtangaza mpinzani hata hao wabunge wa wapinzani ni ruzuku tu kutoka CCM.
 
Kwanini wana JF ambao wako nyumbani wasianze na wao kugombea viti vya ubunge sio kukaa kusema watu wanao jaribu nafasi zao kuleta mabadiliko after all Zitto kaonyesha its possible umri si tatizo sana.

Na nadhani mtu kama FMES hana weza pambana na mbunge yeyote katika hiyo nafasi kama ni hoja tu na ana muda wa kujipanga aende sehemu moja ambayo anaona mbunge ana faida kuliko kukaa nyuma ya migongo ya watu. Kinachoitajika kwa sasa ni challenge kushindwa si vibaya lakini sauti isikike kwamba tupo karibu mno kuliko wanavyofikiria.

CCM hawataleta mabadiliko inabidi ya letwe ata mkishindwa uchaguzi hila waele wazi kwamba kuna challenge za kweli sasa na kama CCM ni damu huu ndio muda wakuanza kupigana kuwe na wagombea binafsi au chama chochote chenye nguvu ya ku-challenge. Safari ya maili millioni moja uanza na atua moja bila kunyanyua mguu amna tunakosogea,vilevile maneno matupu ayavunji mfupa.

action speaks louder than words 'Exhaud Makayo' sijui utajipanga na jimbo gani. Uchaguzi wa Japan chama tawala akikutegemea kama kitashindwa baada ya almost half a century in power lakini wananchi walishachoka na viongozi wale wale ata opinion polls azikutegema mabadiliko especial ndio wenye hela, na watanzania nao wameshaanza kuchoka lakini jibu alitopatikana bila ya kujaribu sidhani watu kama wana-enjoy kulala giza wakati Lowassa kakimbia na hela yao kwa mkataba wa uongo.

Kujaribu si ...........

Mkuu FMES umeipata hiyo?
 
Amani iwe nanyi.

Niafurahishwa sana na hoja hii iliyoanzishwwa na Makyao.

Kupata mabadiliko ya siasa kunahitaji sana watu waliandaliwa kiakili, kiroho na kimtizamo. Watanzania kiakili wanachoka haraka sana kufikiria na kjupamga mambo kimkakati

Kiroho wanaamini kabisa kuwa ikulu imeandaliwa kwa ajili ya CCM tu na ya kwamba chama kingine kikiingia ikulu yatatokea mauzauza ya kutisha sana. Na pengine huo wanauona kama mwisho wa Tanzania.

Kimtizamo: Watanzania wameandaliwa wawe watumwa. Mtumwa hajitawali, hatawali mali yake, hamtawali mtu mwingini wala hawezi kuishi bila kutawaliwa. Sidhani kama watanzania watathubutu maisha ya kutotawaliwa, kuibiwa, kunyonywa na kudnganywa kila siku na CCM. Hayo ndo maisha wanayapenda. Ili kuondoa hilo ni lazima mfumo wa elimu ubadilishwa kwanza na elimu inayomwandaa mtu kujiamini na kujitawala itolewe kwa wingi.

Hapa kuna hoja ya kujibu.
 
Back
Top Bottom