Watanzania tubadilike

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
Hii tabia ya kuchangia harusi hadi milioni 26 watu wanakula siku moja na kujisifu watu walikunywa sana itaisha lini?
Mtu kaishi na mkewe miaka 20 hadi watoto wamefika vyuo anaamua kubariki ndoa anaomba achangiwe miaka yote alikuwa wapi?

kwani bila sherehe ndoa haifungwi
Tuige tabia ya nchi ya Ghana hawana mila za kuchangia watu kufanya harusi unafanya harusi wewe unaandaa wewe mwenyewe kwa uwezo ulio nao siku ya harusi watu wanakuja na zawadi za kufa mtu.
Wenzetu Kenya kidogo sio kama sisi Watanzania.

Ajabu harusi imechangiwa milioni 26 bwana na bibi harusi wakitoka hapo wanatoka kwenda kuishi maisha ya ukiwa na umasikini.

Kwa siku hiyo ya furaha kwa watu wengine inakuwa siku ya kuharibika kwa mauhusiano ya kindoa au kuvunjika kabisa unakuta mkewe kalewa sana anafanya vituko vya ajabu sana ukumbini.Hata kukojoa mbele ya kadamnasi na mwingine hata kubakwa.

Hili nimelishuhudia kwa macho yangu hiyo ndoa hadi leo haipo na ndio chanzo cha kutoa uzi huu.
Ajabu sasa ukiuguliwa hakuna mtu anakuchangia

Ajabu sasa watanzania tulivyo andaa harusi yako wape watu kadi wao waje kula tu na kunywa wasipate tabu watu hawaji kabisa wanasema nitakwendaje harusi sijachangia huu ni upimbi wa kiwango cha LAMI
 

Attachments

  • drunker woman.PNG
    drunker woman.PNG
    44.3 KB · Views: 2
Kwa kweli kabisa watanzania kuna vitu 2 tunafeli. Hata ukiangalia movie za wenzetu wazungu ndoa ni suala la kifamilia. Hata kama wanauwezo vipi wanaandaa sherehe simple wanaalika marafiki wa karibu mambo kwisha.
Jambo la pili ambalo pia inabidi tubadilike ni suala la kuzaa bila mpangilio. Na ni jambo nalo linazidisha umasikini. Hatukatai watoto ni baraka lkn tuzae wale tunaoweza kuwahudumia kwa kuwapa msingi bora.

Wenzetu wazungu hata kama mtu anauwezo kiasi gani atazaa watoto wawili watatu basi. Hii nayo imekua desturi kila ukipita sehemu watu wanachouliza una watoto wangapi? Ukiwajibu mmoja au wawili aaah utasikia acha uvivu ongeza wengine muda unaenda. Lkn huwezi kuwasikia wakikupa hata ushauri wa kutafuta hela.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fedha nyingi za watanzania zinapotea kwa vitu visivyo na tija.

Gharama kubwa za sherehe
Mahari
N.k

Watu walewale waliokuchangia Milioni 20 ya harusi, hawawezi kukuchangia Milioni 5 ukiugua. Tuelekeze pesa pahali penye uhitaji wa Pesa
 
Back
Top Bottom