Watanzania Tuache unafiki.... Eti leo Kila mtu ni CDM hata wana CCM leo wana

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,770
553
Matokeo ya Arumeru yametufundisha mambo mengi sana kwanza watu wengi kuanzia ile asubuhi wanajitambulisha kama wana CDM..

Siko zote watu hawa walikuwa wanasifia na kukataa kuamini kama CDM itashinda, Kila wakisikia CDM imefunika mkutano fulani utasikia Ahhh.. wengi hapo si wapiaga kura Ohh CCM wana mbinu nyingi sana... Mara ohh labda kama vyama vyote vya upinzani vingeungana.... Mara hili... Lile hadi wanachosha lakini Leo kila moja utasikia Hongera aise tumeshinda!!!!!!!!

Ushindi unaanzia mwanzo wa Kampeni hadi siku ya kutangaza KUra na si kukatishana tamaa hadi mwisho...
 
Waache wana wapotevu...sasa hivi wanafikiria kurudi kwa baba yao!
Mfano mzuri ni Ritz, leo mpole kama kondoo anayepelekwa machinjioni!
 
Unafiki + ujinga = umaskini (tanzania hoyeeee)kidumu chama cha mapinduzi wameshikika ipasavyo
 
Kila siku nimekuwa nikisema mie si CHADEMA wala CCM, sifungamani na chama, nafungamana na masuala.

Na - not to rain on anybody's parade, hongereni CHADEMA- lakini kama hakuna mkakati zaidi ya kushinda chaguzi tunaweza kujikuta tunafanya kama Zambia ilipomuondoa Kaunda na kumuweka Chiluba.

Matatizo ya nchi yetu ni makubwa kuliko chama gani kinaongoza. Ingawa kuna hoja nzuri tu kwamba wanaoshindwa kuleta maendeleo inafaa watolewe.

CHADEMA inabidi kijiandae kushika uongozi ili kikija kupata nafasi ya kuongoza kisijikute kinaumwa ugonjwa wa "opposition syndrome" ambao unakifanya chama kiwe kizuri katika upinzani, kinachojua kupinga kama Kiranga bila kutoa mbadala mujarab.

Kiranga anaweza kusamehewa kwa kuwa hana dhamana ya mtu (first of all he refers to himself in the third person, that ought to be a clue). Lakini CHADEMA ni chama cha "kitaifa".
 
Ukiangalia kwa upande mwingine ni
Kitu kizuri kwa hao CCM kuungana na
kusherehekea na CDM...

Haita chukua muda wataanza Kuon umuhimu
Wa kuwa CDM.. You never know wanaweza hamia CDM.. more votes for CDM in 2015.. :)

Mdogo mdogo tunazidi kuwavuta ..
 
Hapo kwenye RED, nimepapenda sana. Kumbe UNAJIJUA....., hahahahaaa......

Ni ujumbe MZITO sana ambao mtu anaweza kuudharau. CHADEMA waanze kuendesha nchi wakiwa kivulini ili wajifunze mapema ugumu upo wapi. Mwamko wa vijana itakuwa SUMU sana kwao siku wakichukua nchi. Nasubiri kujiunga na CCM itakayofufuka baada ya kuzikwa.
CHADEMA inabidi kijiandae kushika uongozi ili kikija kupata nafasi ya kuongoza kisijikute kinaumwa ugonjwa wa "opposition syndrome" ambao unakifanya chama kiwe kizuri katika upinzani, kinachojua kupinga kama Kiranga bila kutoa mbadala mujarab.

Kiranga anaweza kusamehewa kwa kuwa hana dhamana ya mtu (first of all he refers to himself in the third person, that ought to be a clue). Lakini CHADEMA ni chama cha "kitaifa".
 
Nashukuru sana Message sent and delivered , naona wameanza kujikanyaga... Hawa watu ambao hawaeleweki ni wabaya sana kuliko... Ni bora kuwa wa moto au baridi kuliko kuwa vugu vugu.....

Naona hata humu JF wanajikanyaga tena.
 
Back
Top Bottom