Watanzania na umaskini wa kujitakia

Kiraka Kikuu

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,904
1,976
Kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ni msingi wa maendeleo ya mtu,taasisi na jamii yoyote duniani. Bila kujenga utamaduni wa kujibidiisha,maendeleo kufikiwa ni ndoto za mchana! Watanzania wengi wamekuwa na hulka ya kulaumu serikali kutowaletea maendeleo!

Lakini,ni ukweli ulio mchungu,kwamba mtu binafsi,ana wajibu mkubwa sana wa kusababisha maendeleo yake! Ukipita mijini,utakuta makundi makubwa ya vijana wenye nguvu wakiwa vijiweni,wakilalamika ugumu wa maisha!

Muda wa kazi,utakuta watu wamejaa vilabuni,wanalalamikia ugumu wa maisha! Mashuleni na vyuoni,wanafunzi wengi ni wavivu mno katika kujisomea,nao wanalalamikia ugumu wa maisha!

Mwisho wa siku,tunajenga taifa la walalamishi,wavivu na wasio penda kufanya kazi! Ndugu zangu,ni kweli uongozi wa nchi ni mbovu! Lakini,hata tukipata rais imara,kama Dr.Slaa,kwa utamaduni huu wa kutopenda kujibidiisha,hatuwezi kufika popote!

Watu tufanye kazi,ndipo tuilaumu serikali ili iboreshe mazingira ya kazi zetu! Kukaa vijiweni na baa muda wa kazi na kulaum viongoz wetu wachovu ni ujuha mkubwa!
 
Unastahili pongezi kwa kuelezea hali halisi ya 99% ya watanzania walivyo wavivu kwa jambo lolote lile na kusakizia serikali kwa kila jambo
 
Back
Top Bottom