Watanzania kwanini tunakubali Rais wetu adhalilishwe na media za nje kwa kuitwa "The 'Bulldozer' Tanzanian President"?

Mayalla, siku hizi umekuwa mvivu wa kufukunyua maandiko? Nickname siku zote huendana na matendo au tabia ya mpewa jina hilo la utani! Angalia michezo ya mieleka na majina wanayopewa wacheza mchezo ule utagundua kuwa yanaakisi tabia ya mtu huyo. Na hata jina lako alikuambia lina maana ya njaa kwa lugha yenu na huenda ni nickname aliyopewa babu yako!
By the way, wewe linakusumbuaje hilo jina?
 
Kwani wewe kinakuuma nini,kama wao wenyewe wenye mtu wao walimwita hivyo kipindi cha kampeni,na lilikubalika,..labda mmeshituka sasa baada ya kuona kama linaashilia ukweli hv,mwenye nalo hajapinga
 
mean tinga tinga ... nadhani ni jina ambalo hata yeye hana shida nalo ... otherwise kingereza chake ndio kinaleta ukakasi .
 
Pumbafu kabisa wewe, au umayala wa bin njaa unakusumbua wewe??? Mlimuita wenyewe tingatinga kwenye kampeni mkachora na kwenye matisheti yenu picha ya buldoza ,halafu unakuja kusema vyombo vya nje vinamchafua ??? Pimbi kabisa wewe na sisiemu yako...
Punguza ukali wa maneno Mkuu...
 
Je Mayalla hope najua unajua BULLDOZER / TINGATINGA ni mtambo wa aina gani.

Pili kwa kuwa najua wewe ni mfuatiliaji wa siasa za bongo hasa 2015 basi unajua asili ya jina hili kwa Rais wetu.

Itoshe tu kusema aliitwa kwa maana hiyo ya kutusafishia nyumba yetu sasa hao wa nje kama wana tafsiri yao tofauti tusaidie ili tuijadili na kushauri kama ulivyoona wewe.

Otherwise ni jina zuri kwake kwa kuwa anatenda kama alivyotuahidi.
 
Yote na Yote udikteta huu ndio bays zaidi ya Yote pamoja na raisi wa ajabu hii hapa imekaaje na nchi yetu tunayoinadi nchi ya amani

Mkuu Orenda,

Lazima tufahamu kitu kimoja cha ziada mwelekeo na mtizamo wa uongozi wake hautaweza kufanikiwa ktk nchi hii,

Bado, nasubiri kwa hamu kubwa maelezo na studies za wasomi wetu kuelezea jinsi gani utawala wa kuigwa kama Rwanda, Uganda au hata Kenya, utafeli to implicate and implement hapa Tanzania

Na kuna sababu nyingi sana za kimsingi na kihistoria, we are different, very diverse, progressive, location yetu geographically, resources zetu na la msingi zaidi watu wake.

Sasa siasa za nchi jirani na mielekeo yao ya kikabila, partisan politics haitoweza kufanyika hapa Tz. Mwalimu Nyerere aliyaona hayo akayawekea misingi imara yenye mizizi kuepuka ujirani, na hili la uchama ndani ya jeshi, polisi na vyombo vya usalama ni kitendo cha kupingwa kabisa.

Sasa sijui nani? Anamshauri vyenginevyo, foka foka nyingi majukwaani, vitisho, na kibaya zaidi kujipendekeza na jeshi na vyombo vya usalama, maguvu mengi kwa wanaompinga kisiasa. Siasa za namna hii hazina mafanikio popote pale.

Tumeweza kukaa na jeshi letu kwa amani na utulivu for years, anakuja yeye anaanza kuingiza upartisan ndani ya uongozi wa viongozi wa jeshi na kuwahusisha zaidi kichama.

Jeshi letu liko smart sana kuona mtizamo huu, limeweza kufanikiwa na kuimarika nje ya politics why risking all now? That’s the question.

Ndio anastahili sifa kubwa ya kujaribu kusafisha uzembe ndani ya taasisi za serikali, vita dhidi ya rushwa na madawa ya kulevya ijapokua kuna mapungufu yake, kusimamia ufanyaji kazi bora, lakini cha msingi kabisa bado hajaweka misingi mipya ya kuwezesha hayo anayoyakusudia, ijapokua ameweka wazi zamira yake ya mahakama ya ufisadi as a short term solution, sheria bado ni zile zile and yet to see fisadi in jail. So far ni rusha roho tu. Na swala la msingi what next on his part au ndio amesha run out of gas and ideas, sasa ni shurti na piga piga.

Ameharibu sana biashara za ndani, na Vile vile ameshaharibu uwekezaji, a signature policy on his part, kaipigia debe sana juu ya hili anafeli kuliona hili na mengi tu, amebaki kusifia ujaji wa Bill gate, Rais wa world bank kama sijakosea, Dangote(now nemesis), nk

Yaani kinachofanyika sasa kuchukua bunduki na kuua panya ndani ya nyumba yako, effort kubwa alitakiwa kuweka mazingira bora kuondoa ukaazi wa panya, na sio kuweka matundu ya mtutu kila sehemu, enough of that sasa ziba viraka kabla ya kuziba nyufa.
 
Nakumbuka "Bulldozer" iliyokuwa imepakwa rangi ya kijani pale viwanja vya Furahisha-Mwanza, likiashiria kuwa mgombea wa Chama Chetu atafanya kazi kama TingaTinga. Sasa Mzungu kasema "Bulldozer" imeshakuwa nongwa. Sisi tukimsifia Mkuu Tingatinga; mswano tu! Bulldozer = Tingatinga.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la wito kwa Watanzania wote wenye mapenzi mema na taifa letu, kwa nini tunakubali rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, adhalilishwe na Media za Nje kwa kuitwa The 'Bulldozer' Tanzanian President!, na sisi tunakubali na kunyamaza tuu?! huku Kurugenzi yetu ya Mawasiliano Ikulu ipo?, Idara yetu ya Habari Maelezo ipo?, Waziri wetu wa Habari yupo?.

Soma hii
Dangote accuses 'Bulldozer' Tanzanian president of scaring away ...
What does this statement kuachwa tuu bila kukanushwa, mean to Tanzania investment climate?.
Na hii sio mara ya kwanza kwa rais Magufuli kuitwa hivi, aliwahi kuitwa hivi
John Magufuli - Tanzania's 'Bulldozer' president in profile - BBC News
Tanzania's new president, 'The Bulldozer' Magufuli » Capital News
Tanzania: Tension Between Tanzania's 'Bulldozer' President and ...
Tanzania's bulldozer president takes on London miner - Financial Times
Tanzania's President John Magufuli: The bulldozer crushing ...
Behind Tanzania's President John 'The Bulldozer' Magufuli's mining ...
Tanzania's new president, 'The Bulldozer' Magufuli - Nairobi News


Kwa nini rais wetu, asemwe vibaya na sisi tupo, tunakubali na huku tumenyaza tuu?!. Kurugenzi yetu ya Mawasiliano si ipo?, kwa nini inakubali na kukaa kimya?!,
Idara yetu ya Habari Maelezo si ipo?, kwa nini inakubali na kukaa kimya?!.
Waziri wetu wa Habari si yupo?, kwa nini anakubali na kukaa kimya?!.

Swali msingi ni Jee ni kweli rais Magufuli ni The 'Bulldozer' Tanzanian president?!. Japo kuna wengi watatafsiri Bulldozer kama Tingatinga, lakini kwa wazungu, Bulldozer ni someone who bullies, ambalo sio jina zuri. Jee kweli rasi wetu ni bully?. Kama sii kweli, kwanini tunanyamaza tuu bila kukanusha, maana uongo ukisemwa sana na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wake sio tuu utaonekana kama ni ukweli, bali mwisho wake hugeuka ni ukweli!.

Mimi naomba kujipambanua kuwa ni Mtanzania Mzalendo wa kweli kwenye media, na kwa mujibu wa fani yangu, kazi yangu na uwezo wangu ni kushauri tuu kwa kuandika au kusema au kutangaza.
  1. Rais wetu alipotuhumiwa kuhongwa suti nilipinga na kushauri.Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi ...
  2. Hata kelele kuhusu udikikiteta wa Magufuli ziliposhika kasi nilishauriUdikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
  3. Magufuli aliposemwa vibaya na SABC, nilishauriSerikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
  4. Rais Magufuli aliposemwa vibaya kuhusu Mimba za utotoni, pia nilishauriJe, Huku Sio Kudhalilishwa Kwa Rais Wetu na Media za Nje?. Jee ...
  5. Juzi kati hapa srikali yetu ilipoitwa Sinister na Authoritarian, pia nilishauri
    Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli ...
Na sasa hapa rais wetu anaposemwa vibaya, na kuitwa The 'Bulldozer' Tanzanian president!, nimeandika na kushauri tusikubali, tusikae kimya, tukanushe unless kama yanayosemwa kumhusu rais Magufuli ni kweli kuwa ni The 'Bulldozer' Tanzanian president, vinginevyo tukanushe.

Mungu ibariki Tanzania.

Paskali
Huku kwetu Uzunguni/Ughaibuni maana ya Bulldozer ukiipeleka kwenye tafsiri ya mtu/kufananishwa ina maana >> Mharibifu, mbomoaji, mkurupukaji, mvunjaji, mvamizi, mwonevu, mbinafsi, mvunjifu kwa kila jambo analolifanya mhusika..
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la wito kwa Watanzania wote wenye mapenzi mema na taifa letu, kwa nini tunakubali rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, adhalilishwe na Media za Nje kwa kuitwa The 'Bulldozer' Tanzanian President!, na sisi tunakubali na kunyamaza tuu?! huku Kurugenzi yetu ya Mawasiliano Ikulu ipo?, Idara yetu ya Habari Maelezo ipo?, Waziri wetu wa Habari yupo?.

Soma hii
Dangote accuses 'Bulldozer' Tanzanian president of scaring away ...
What does this statement kuachwa tuu bila kukanushwa, mean to Tanzania investment climate?.
Na hii sio mara ya kwanza kwa rais Magufuli kuitwa hivi, aliwahi kuitwa hivi
..
Swali msingi ni Jee ni kweli rais Magufuli ni The 'Bulldozer' Tanzanian president?!. Japo kuna wengi watatafsiri Bulldozer kama Tingatinga, lakini kwa wazungu, Bulldozer ni someone who bullies, ambalo sio jina zuri. Jee kweli rasi wetu ni bully?. Kama sii kweli, kwanini tunanyamaza tuu bila kukanusha, maana uongo ukisemwa sana na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wake sio tuu utaonekana kama ni ukweli, bali mwisho wake hugeuka ni ukweli!.
...
Mungu ibariki Tanzania.

Paskali



Link JK amfananisha Magufuli na 'tingatinga'
 
Back
Top Bottom