Watanzania hawatapata unafuu wa maisha milele

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,716
36,186
Hello!
Ninaposema Watanzania namaanisha majority ya Watanzania nikiwaondoa watu wachache sana.
Hawa majority walipata taabu sana, wanapata taabu sana na watapata taabu sana.
Babu zao walipata taabu sana kubeba mizigo bandarini na kufanya shughuli zingine ngumu ili wale na wajenge nyumba za kuishi, ile taabu na dhiki ikarithishwa kwa watoto wao na sasa wajukuu wao wanaendelea kupata shida.
•Nilitaraji gesi ingefuta taabu kwa wananchi haikuwezekana.
•Nilitaraji labda barabara za rami zitaleta unafuu, haikuwezekana licha ya mikoa mingi kufikiwa na rami.
•Nilitaraji sekondari za kata zingefuta ujinga, na umaskini, haikuwezekana.
Sasa ni nini kitaweza kutumika kufuta umaskini na kuleta unafuu?
Je, makaa ya mawe?
Dhahabu?
Almasi?
Tanzanite ?
Bahari na maziwa?
Mbuga za wanyama tulizokuwa tukiimbishwa shuleni tangu tupate uhuru?
Hii dhiki ya Watanzania ni ya milele. Walioko kwenye system ambao ni wachache pamoja na wafanyabishara wachache ndio watapata unafuu.
CCM ndio kwanza wanawaandaa chipukizi walijua kuwa miaka 30 mbele ndio watakuwa bungeni na Ikulu.
 
Back
Top Bottom