Watanzania Acheni Ukatili wa Kuwachoma Moto Wenzenu: Video Ikionyesha Mauaji

Geeque

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
936
316
Hivi Serikali iko wapi ili kuweza kuhakikisha mauaji kama haya hayatokei, lini serikali imeweza kuwachukulia hatua washiriki wa mauaji kama haya? Tunajua iliwachukua muda muda mrefu kwa viongozi wetu kukubali kulikuwa natatizo la mauaji ya albino. WARNING: GRAPHIC VIDEO VIEWERS DISCRETION IS STRONGLY ADVISED.

http://www.eastafricantube.com/media/25226/Petty_Thieves_Burned_to_Death_in_Tanzania-_East_Africa/

Hii clip nimeamua kuiweka kwenye siasa ili wengi waione lakini Moderator unaweza kuihamisha hapo baadae.

SAHIHISHO: BAADA YA UTAFITI IMEGUNDULIKA VIDEO HII HAIKUCHUKULIWA NDANI YA TANZANIA BALI KENYA, SAMAHANI KWA USUMBUFU ULITOKEA KUHUSIANA NA RAIS KIKWETE NA VIONGOZI WA TANZANIA KUHUSISHWA NA VIDEO HII.
 
Mpelekeeni Smata. Vipi Geeque ukiona mahali pameandikwa EA lazima ufahamu hao ni Kenya mara nyingi lakini ukiona Kilimanjaro au serengeti ndio wanaandika Kenya lazima uwe mwangalifu kidogo kwa hawa Manyang'au maana wanasaidiwa na Ankal wao kule ulaya.
 
Haipendezi kumsingizia Kikwete kila jambo litakaloonekana kuwa ni baya. Acheni kutafuta laana zisizokuwa na maana. Sasa hata video za Kenya na zenyewe Kikwete, mmeambiwa yeye ni Rais wa East Africa? Mwacheni Rais wetu bwana.
 
Mh, T. usitetee hawa jamaa wana haya mambo ya kuchoma moto sijui vibaka wa vipochi hile piga ua yao. Duuh hii sasa noma OK niko na wao kumuwashia nguki jambazi wa bunguki. Lakini mteja kumchoma moto sijui kisa kaiba nembo ya benzi, au anakimbia na nguo za uwani kule kwetu kariakoo si sawa bwana.
 
Braza,

Hiyo video sio bongo ni Kenya, ni ya siku nyingi kidogo na kama nakumbuka vizuri......hao watu walikuwa wanashutumiwa kwa uchawi au kitu flani!!! Ni Kenya na sio Tanzania.......huyo Kikwete mpeni breki mara moja moja au walau mumpe tuhuma sahihi na sio za kizushi!!! LOL

Isitoshe, nchi zote za 'ulimwengu wa tatu" ambapo rule of law imepindapinda kama bongo, vibaka na washenzi wengine kama wauaji wa albino uaga wanachezia kiberiti, machete, mawe na kadhalika! Kipi kigeni hapo kaka? Hii political correctness saa nyingine hunishangaza sana.....

Jioni njema!

Ahsanteni wote kwa maoni yenu na usahihisho kuhusiana na eneo video hii ilipochukuliwa, ingawa mtu alietuma alisema Tanzania na hivi sasa sina uhakika ni wapi ilipochukuliwa. Wengi wetu tunajua Tanzania kwa muda mrefu sana kumekuwa na tabia ya kuchoma moto watu wanashutumiwa kwa wizi na ujambazi. Hii haiondoi jukumu la serikali kukemea tabia hii ili utawala wa sheria uchukue mkondo wake. Haya madai si kwa ajili ya POLITICAL CORRECTNESS bali ni umuhimu wa Rule of Law na majukumu ya viongozi tunaowachagua na vyombo vya usalama na sheria kutimiza majukumu yao tuliowakabidhi.
 
Haipendezi kumsingizia Kikwete kila jambo litakaloonekana kuwa ni baya. Acheni kutafuta laana zisizokuwa na maana. Sasa hata video za Kenya na zenyewe Kikwete, mmeambiwa yeye ni Rais wa East Africa? Mwacheni Rais wetu bwana.
Ina maana hujui kuwa kuna vibaka wadogo wadogo wanaochomwa moto Tanzania na serikali inabaki kimya bila hata ya kukemea au kuchukulia hatua washiriki wa mauaji kama hayo?
 
........... ingawa mtu alietuma alisema Tanzania na hivi sasa sina uhakika ni wapi ilipochukuliwa. ..........

Mazee.......Heri ya mwaka mpya.........pamoaj na ukweli kuwa watu wanachomwa moto kule nyumbani (walaaniwe wanaofanya kitendo hicho).........pia angalia sana mtu anayekupa taarifa........
 
Mazee.......Heri ya mwaka mpya.........pamoaj na ukweli kuwa watu wanachomwa moto kule nyumbani (walaaniwe wanaofanya kitendo hicho).........pia angalia sana mtu anayekupa taarifa........
Pouwaaa sana Mazee heri ya mwaka mpya na nimekupata kabisa, nadhani nimeshafanya masahihisho hapo juu
 
I am very sad, it real hurt to see human being burned to death, while other people are watching and triumphing!

Kenya you will never join with Tanzania by anyhow, not in this planet;

we are Tanzanian! east africa is just a geographic position! if God will ask me what miracle I want, I will say please move Tanzania far, far, far, far, away from Kenya.
 
Back
Top Bottom