Watangaza nia walikuwemo bungeni tangia 2000 - 2015

Chademakwanza

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
6,346
1,871
Walijua rushwa inakua,kwa kuwa wao ndani ya ccm,hauwezi kupita bila kutoa rushwa

Ccm ilijua,kuwa hakuna maji,

Ccm ilijua,hakuna umeme wa kubabaisha umekuwepo tangu uhuru,

Ccm walikuwepo ( wakiwa na baraza la mawaziri) walipomshauri Rais kama ilivyo ajenda yao ya kutegemea misaada kwenye bajeti yao tangu 2000-2015,

Walikuwemo ndani ya baraza lao,walipokubaliana kuuza viwanda vyetu,

Walikuwepo ndani ya bunge na baraza la mawaziri,walipogundua gape la walionacho na wasionacho likikua,

Walikuwepo wakati fedha nyingi zilizopelekwa Tamisemi kwenye Halmashauri lakini zililiwa na CAG ametumia miaka 15 kutoa maeneo ya wizi wa fedha hizo za miradi ya maendeleo,

Walikuwepo,walipopitisha sera ovu za Elimu,Afya ambapo ahadi ya wakina mama wajawazito,watoto na wazee hawakupaswa kulipa gharama za matibabu,

Walikuwepo wakati walipopitisha na kuacha sheria zivunjwe!

Walikuwepo walipopitisha sheria ya Elimu kuwashirikisha wazazi kuchangia elimu huku wakijua kuwa wanaiba?

Walikuwepo wakati kupanda gharama za msisha kutoka unga tsh 250-2500!,sukari toka tsh 600hadi 2500?
Walikuwepo wakati matatizo ya walimu ya mshahara mdogo,Waajiri 3 ,Tamisemi,Tume ya utumishi,wizara ya Elimu na Mkurugenzi kiasi kwamba matatizo yao yalibaki yakipigwa dabadana!

Walikuwepo madai ya walimu,mishahara,malimbikizo, nauli za likizo ambazo kwa mujibu wa sheria waliyoitunga inapaswa kumlipa mtumishi na mme au mke na msaidizi mmoja,lakini leo wanasema walimu ni wengi mno,mara kama ualimu hauna dili katafute kazi nyingine( Mwantumu Mahiza) ,na pia kukosa kujengewa nyumba,

Walikuwepo walipoona walimu wakishangaa madarasa yakijengwa hayana umeme wala hakuna choo cha walimu ila cha wanafunzi kipo!

Walikuwepo wakati ccm inatangaza KDA kigamboni kwa nguvu,leo inasema imefuta sababu ya uchaguzi,ila ukiisha sheria iko palepale mikataba waliyoingia hakuna mahala walipoivunja!

Walikuwepo wakati 1990-2015 Timu ya Taifa ya riadha na ile ya miguu na michezo mingine ikifa!

Walikuwepo walipofanya maamuzi magumu ya kuiba fedha za Wananchi na kusimama bungeni kuwaita watu tumbili huku Escrow wakiweka mifuko hadi hata wanaoishi nyumba ya watanzania iitwayo takatifu .

Walikuwepo walipokubali mazao kama pamba,ngano,karafuu,nazi kahawa na mengine yalipokosa soko la uhakika na wakulima kuvunjika moyo!

Walikuwepo wakati wakiona,madini,almasi,dhahabu na Tanzanite wazungu wa Afrika kusini wakibeba kwa helkopita na kwenda kusafishia kusini!

Walikuwepo wakati watu takribani ajali zipatazo 2500 zikiua karibu watu laki 40000 tangu 1995-2015 na kuacha mayatima ambao hata Elimu,tiba na chakula imekuwa shida!

Walikuwepo wakati Sheria ya Takrima,Sumaye akiipitisha na wenzake!

Walikuwepo wakati David Mwangosi,Absalom kibanda ,Ulimboka,Mbwambo na pale soweto walipovamiwa kupigwa,kung'olewa meno,kumwagiwa tindikali na wengine kutupiwa bomu la kurushwa na mikono.

Walikuwepo wakati shilingi ya Tanzania ikishuka kisa sisi hatuuzi ila tunaagiza hakukuwa na juhudi ya kukuza uchumi ila kuna juhudi ya kuiba na kuvorwsha maisha ya mtu kiongozi baki!

Walikuwepo wakati machinga,bodaboda ,mama ntilie wakipigwa,kuzolewa na kunyang'anywa mali zao!

Hao ndio watangaza nia ya kuwakomboa watanzania kutoka lindi la umaskini, leo hii kila mmoja anatangaza nia?

Tutakuwa watanzania wa ajabu tukikubali kuwa ndani ya ccm kuna mtu!

Wagombea hawa,ni wote wamewahi kukaa kwenye baraza la mawaziri na baraza la ulinzi na usalama,walifanya nini?

Watanzania,mlakunde anasahau lakini mtupa maganda hawezi kusahau ccm haifai!
Mazoea huzaa tabia umefika muda ambapo chupa yeye kuwekwa mvinyo ileile tuikatae!

Tanzania nchi ya amani ,uchumi imara,maisha ya kati, na usalama inawezekana achaneni na mazoea ukawa ndio umoja wenye tija kwawananchi inawezekana,ni kuwa na kadi yako ya kupigia kura, kuwahi siku ya kupiga,"amua kwa ajili ya watoto na wajukuu wako"
 
Kuwepo Bungeni si hoja!Maana kuwepo hata wabunge wengine ambao hawajatangaza(maana watatamgaza tu, it is just the matter of time) walikuwepo.

Kuwepo Bunfeni si hoja, ila kuwepo Bungeni na kupiga kura ya "Ndiyoooooooooooo" kwa kila jambo ndiyo hoja!
 
ccm kama ina lengo la kupambana vizuri kwenye uchaguzi wa oktoba ihakikishe inapitisha mgombea asiye na kashfa na pia anayekubalika na watanzania walio wengi. pia asiye ambaye alikuwa serikalini. vinginevyo ccm wasitafute mchawi.
 
walikuwepo wakati wagawa viwanda vyetu leo wanajidai tatizo la ajira bomu,walikuwepo wakati wanajipendelea kugawana nyumba zetu leo wanachukia umasikini,elimu inatelekezwa walikuwepo pia
 
Wana jf, nijambo la kushangaza kila mtangaza nia anajinadi atakavyowatumikia wananchi kwa ufanisi na kuonyesha mwongozo na sera atakazo zitumia. Wania hawa jk aliwaami akawachagua waisaidie serikali yake kuvuka malengo ya milenia kwa kuondoa vikwazo vya maendeleo.

Leo hii wameonyesha unafiki wa wazi, kwa kukunjua makucha kuelezea njia walizozificha ili serikal ya jk ikwame. Watwambie walificha haya mawazo kwa faida ya nani? Kumbe tunahitaji kuwepo mdahalo wa kuwachuja hawa, tunataka wawepo wagombea 60 ili tukusanye mawazo yao tuendeleze nchi.

Ona mwigulu mbeba zege mwenye digree, ona huyu lowasa mwenye utajili wa ng'ombe tu,njoo kwa masatu mkulima na mfanyabiashara ya samaki walivyoficha mawazo wakiwa wasaidizi
 
Naskia na bwana Kighoda nae atatangaza nia,sasa jamani huyu bwana alishiriki uuzwaji na uuaji wa Vijiwanda vyetu,leo akiwa rais si ataiuza mpaka tii bii esi
 
ccm kama ina lengo la kupambana vizuri kwenye uchaguzi wa oktoba ihakikishe inapitisha mgombea asiye na kashfa na pia anayekubalika na watanzania walio wengi. pia as
iye ambaye alikuwa serikalini. vinginevyo ccm wasitafute mchawi.
Naomba niku sahihishe Hakuna Msafi ccm anayeweza kuongoza Watanzania
 
walikuwepo wakati wagawa viwanda vyetu leo wanajidai tatizo la ajira bomu,walikuwepo wakati wanajipendelea kugawana nyumba zetu leo wanachukia umasikini,elimu inatelekezwa walikuwepo pia
Ccm wameuza kila kitu na Kugawana Shamba la bibi
 
Na hili ulilolisema Mkuu, nisahihi. Reflection ya rangi halisi ya ccm na seikali yake utaiona kila sehemu sasa kuanzia kwa viongozi wao wa mitaa, mabaraza yote kata na kuendelea.

Mtanzania hapati huduma bila rushwa,
Kupiindishwa kwa haki na ukweli.
Michango isiyotija wala maelezo.
Ubaguzi na uonevu kwa raia.
Umangi meza na kutaka kuabudiwa na kila mtu, asiyefanya hivyo, atatafutiwa zengwe ama atasubiriwa siku ya tatizo akomeshwe zaidi.
Kuweka mbele tamaa ya fedha kwa viongozi hawa badala ya kuwahudumia wananchi.
Dharau kwa raia.
Kulindana, kuteteana na kufichiana makosa.
Kuwaaminisha Watanzania kwamba maisha duni wanayoishi na maumivu yao ndiyo stahihli yao na hakuna uwezo wa kuishi maisha bora zaidi ya hapo.
Kuwafanya Watanzania waamini huduma wanayopata ni msaada na si haki yao.
Kuwafanya watu waone Miradi ya maendeleo ya serikali ni hisani ya ccm na si majukumu ya serikali hivyo hawana haki ya kuhoji.
Kuwajengea watu woga kwamba atakayehoji nyendo za watawala ni adui na hivyo lazima apigwe.(Nidhamu ya woga).
Kukata tamaa kwa wananchi kwamba wanaishi wakingoja kufa, basi.

Ccm kujiona ni watawala na wengine ni vijakazi.

Yote hayo yanayofanywa na ccm taifa ndiyo hayo hayo yameshuka hadi chini ambako yanagusa maisha ya mtu moja mmoja. Huko ndiko kwenye kilio na kusaga meno.

NINAOMBA SERIKALI YA UKAWA, ISISAHAU KABISA SUALA LA UTAWALA BORA, NIDHAMU NA UWAJIBIKAJI KWA WANANCHI KWA VIONGOZI WA VYAMA NA SERIKALI YAKE KATIKA NGAZI ZOTE.

Ccm imejenga uozo mkubwa mno Tanzania.

UKAWA HOYEEEEEEEEEEEE!
 
Kuwepo Bungeni si hoja!Maana kuwepo hata wabunge wengine ambao hawajatangaza(maana watatamgaza tu, it is just the matter of time) walikuwepo.

Kuwepo Bunfeni si hoja, ila kuwepo Bungeni na kupiga kura ya "Ndiyoooooooooooo" kwa kila jambo ndiyo hoja!
Na wale wanaokuwepo Bungeni na kulala?
 
Na hili ulilolisema Mkuu, nisahihi. Reflection ya rangi halisi ya ccm na seikali yake utaiona kila sehemu sasa kuanzia kwa viongozi wao wa mitaa, mabaraza yote kata na kuendelea.

Mtanzania hapati huduma bila rushwa,
Kupiindishwa kwa haki na ukweli.
Michango isiyotija wala maelezo.
Ubaguzi na uonevu kwa raia.
Umangi meza na kutaka kuabudiwa na kila mtu, asiyefanya hivyo, atatafutiwa zengwe ama atasubiriwa siku ya tatizo akomeshwe zaidi.
Kuweka mbele tamaa ya fedha kwa viongozi hawa badala ya kuwahudumia wananchi.
Dharau kwa raia.
Kulindana, kuteteana na kufichiana makosa.
Kuwaaminisha Watanzania kwamba maisha duni wanayoishi na maumivu yao ndiyo stahihli yao na hakuna uwezo wa kuishi maisha bora zaidi ya hapo.
Kuwafanya Watanzania waamini huduma wanayopata ni msaada na si haki yao.
Kuwafanya watu waone Miradi ya maendeleo ya serikali ni hisani ya ccm na si majukumu ya serikali hivyo hawana haki ya kuhoji.
Kuwajengea watu woga kwamba atakayehoji nyendo za watawala ni adui na hivyo lazima apigwe.(Nidhamu ya woga).
Kukata tamaa kwa wananchi kwamba wanaishi wakingoja kufa, basi.

Ccm kujiona ni watawala na wengine ni vijakazi.

Yote hayo yanayofanywa na ccm taifa ndiyo hayo hayo yameshuka hadi chini ambako yanagusa maisha ya mtu moja mmoja. Huko ndiko kwenye kilio na kusaga meno.

NINAOMBA SERIKALI YA UKAWA, ISISAHAU KABISA SUALA LA UTAWALA BORA, NIDHAMU NA UWAJIBIKAJI KWA WANANCHI KWA VIONGOZI WA VYAMA NA SERIKALI YAKE KATIKA NGAZI ZOTE.

Ccm imejenga uozo mkubwa mno Tanzania.

UKAWA HOYEEEEEEEEEEEE!
Fisadi kutangaza nia nikuwadhihaka Watanzania
 
Leo nasikia yule jamaa anataka kuwa rais wawauza juice ataongea na kutangazania awe rais wetu wauza juice!yule ambaye anaamini sisi wauza juice hatuwezi ila wageni ndio wanaweza wakati yeye mwenyewe muuza juice na kuonesha hawezi wauza juice walimpa ile wizara ya moto kwenye lile shirika la moto deni likawa kubwaa hatari!na bei ya moto ikawa kubwa hatari
 
Mungu uwalinde watu hawa wanao jua kuchambua mambo kwakina ccm imelaaniwa ndio maana akuna msafi
 
Back
Top Bottom