Waswahili tunatawaliwa na waarabu ?

kwa maoni yangu mimi ili kiswahili kiweze kujitegemea basi lazima kwanza zitafutwe sarufi za kiswahili kama ilivyowezekana kukitoa kiswahili kwenye serufi za kiarabu na kuzileta hapa tulipo sasa, likiwezekana hilo basi tutaweza kupunguza kuwa wategemezi wa lugha zingine na wala sio kiarabu pekee kichomimeza hii lugha yetu
 
kwa maoni yangu mimi ili kiswahili kiweze kujitegemea basi lazima kwanza zitafutwe sarufi za kiswahili kama ilivyowezekana kukitoa kiswahili kwenye serufi za kiarabu na kuzileta hapa tulipo sasa, likiwezekana hilo basi tutaweza kupunguza kuwa wategemezi wa lugha zingine na wala sio kiarabu pekee kilichoimeza hii lugha yetu
 
Hapo mwanzo ni Kweli Kiswahili kilikuwa na Maneno mengi ya Kiarabu, lakini hivi sass Kadri kinavyokuwa na Kupanuka kwa kasi, Msamiati wake unaongezeka kwa Maneno yasiyo ya Kiarabu. Kukua kwa Teknolojia kumeingiza maneno Mengi ya Kiingereza (km Neno "teknolojia lenyewe ni la Kiingereza "Technology") aidha taasisi zetu za Lugha ya Kiswahili ikiwemo BAKITA wamefanya kazi ya ziada Kuisanifu Lugha hii na kutafiti maneno mbalimbali kutoka lugha za Asili ya Kiafrika ma hasa za Afrika Mashariki. Angalia, utakuta Msamiati katika Kamusi ya Kiswahili unaongezeka kila mara Lakini sio kwa Maneno ya Kiarabu, kwa Hiyo hakuna hofu ya Lugha yetu Adhimu Kumezwa na Lugha nyingine yoyote Kubwa!
 
Hiatatokea waarabu wakasema tusitumie lugha yao maana hata wao kwenye lugha yao kuna maneno wameyatohoa kutoka kwenye lugha nyingine. Pia Duka sio neno la asili ya kiarabu ni neno la Kigujarat cha nchini India.

Chai-Gujarat
 
kwa maoni yangu mimi ili kiswahili kiweze kujitegemea basi lazima kwanza zitafutwe sarufi za kiswahili kama ilivyowezekana kukitoa kiswahili kwenye serufi za kiarabu na kuzileta hapa tulipo sasa, likiwezekana hilo basi tutaweza kupunguza kuwa wategemezi wa lugha zingine na wala sio kiarabu pekee kichomimeza hii lugha yetu

Kaka, sarufi kwa mujibu wa Kamusi ya Isimu na Lugha(TUKI, 2004) ni "taaluma ya lugha inachunguza na kuchanganua kanuni za lugha." Sarufi inahusu kanuni, na kwa mkataa huo, sarufi ya Kiswahili inaoana na sarufi za lugha nyingi za Kibantu. Mf. Muundo wa kiima na kiarifu, mpangilio wa viambishi, uhusiano wa maneno katika sentensi n.k. Ndio maana neno likitoholewa, hurekebishwa ili lioane na mfumo wa lugha husika. Mfano: Basin-beseni, heller-hela, mezr-meza, dukha-duka!
 
Lugha ya kiswahili ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita,Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. zaidi ya theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.kuna maneno machache ya kiajemi,kihindi ,kireno na kingereza.
waswahili bado tumetawaliwa na Waarabu kupitia kwenye lugha.Tanzania ,Kiswahili ni lugha ya Taifa.mfano wa maneno ya kiarabu tunayoyatumia ni suku-soko,dukan-dukani,shai-chai,bahri-bahari,samaku-samaki,rejea-rejea,daftar-daftari,asbuh-asubuhi,........
maneno ni mengi siwezi kuyataja yote hapa.
NINI KITATOKEA ENDAPO WAARABU WATAKAA NA KUTUOMBA TUSITUMIE MANENO YAO ?,KISWAHILI KITAKUFA?.

Kiarabu kimejengwa kutoka Lugha ya Kiajemi ya iliyokuwa Mesopotamia pia Lugha Iliyoongelewa Egypty Enzi za Farao.

Kuchukua maneno kutoka Lugha fulani hakuna maana kwamba wenye Lugha wanakutawala.
Mfano Kijapan chote na Kikorea chote ni Modified Chinese.
Wachina waligundua kuandika wakati Japanese walikuwa bado wanawinda Ndezi.
Si kweli wajapan wanatawaliwa na wachina.

Wajapan ndiyo waliowatawala Wachina na Wakorea japo Wachina walikuwa mbali katika kila kitu kwa miaka Elfu kadhaa.
 
Madela wa Madilu, yaani Hukuona chochote cha Kuwindwa na WaJapani ila NDEZI, ilimradi Uwachokoze Wazigua ili Waseme, Sio?
 
na kwa nini tumefika mahala tunadhani kiswahili kimeiba maneno ya lugha zingine kiarabu n.k kwa nini sio vice versa kwamba wao ndo wameiba kutoka kiswahili??????kwa nini tunapenda kuwa chini..ina maana mababu zetu hawakufanya chochote??
Si zaidi ya 25% ya Kiswahili ni Kiarabu.
INGEKUA 60% YA KISWAHILI NI KIARABU KAMA BAADHI WANAVYODAI BASI WAARABU WASINGEKUA NA HAJA YA KUWA WAKALIMANI KUELEWA KISWAHILI. NA WATANZANIA WASINGEKUA NA HAJA YA MKALIMANI AU KUJIFUNZA KIARABU MAANA WANGEELEWA BILA SHIDA.

NILIWAHI KWENDA UARABUNI, NIKAWA SISIKII CHOCHOTE PUNDE WANAPOANZA KUZUNGUMZA KIARABU. NDIO UNAWEZA BAHATISHA NENO MOJA KATIKA SENTENSI NZIMA LAKINI HII HAIKUWEZESHI KUELEWA SENTENSI ILIKUA INA MAANA GANI.
 
Kiarabu ndio kilichukua maneno ya Kiswahili/Kiafrica na kuingiza kwenye Lugha yao, Kiarabu kilichukua maneno mengi kutoka lugha iliyokuwa inazungumzwa africa (Misri, Nubi, Kushi) na kuingiza kwenye lugha yao

hivyo si Kiswahili kilichokopa maneno ya kiarabu, bali Kiarabu ndicho kilichokopi hayo maneno
 
Lugha ya kiswahili ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita,Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. zaidi ya theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.kuna maneno machache ya kiajemi,kihindi ,kireno na kingereza.
waswahili bado tumetawaliwa na Waarabu kupitia kwenye lugha.Tanzania ,Kiswahili ni lugha ya Taifa.mfano wa maneno ya kiarabu tunayoyatumia ni suku-soko,dukan-dukani,shai-chai,bahri-bahari,samaku-samaki,rejea-rejea,daftar-daftari,asbuh-asubuhi,........
maneno ni mengi siwezi kuyataja yote hapa.
NINI KITATOKEA ENDAPO WAARABU WATAKAA NA KUTUOMBA TUSITUMIE MANENO YAO ?,KISWAHILI KITAKUFA?.

Chai na chapati ni kihindi.

Ukienda India, ingia tu ndani ya mgahawa, kisha sema " Chai, chapati"... Utaletewa hizo hizo chai na chapati.
 
Naomba ubadlishe heading yako..

Mie ni Mswahili.. lakini kutawaliwa na Waarabu? Thubutu..!!! Ni sawa na kujaribu kumtawala simba.
 
Lugha ya kiswahili ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita,Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. zaidi ya theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.kuna maneno machache ya kiajemi,kihindi ,kireno na kingereza.
waswahili bado tumetawaliwa na Waarabu kupitia kwenye lugha.Tanzania ,Kiswahili ni lugha ya Taifa.mfano wa maneno ya kiarabu tunayoyatumia ni suku-soko,dukan-dukani,shai-chai,bahri-bahari,samaku-samaki,rejea-rejea,daftar-daftari,asbuh-asubuhi,........
maneno ni mengi siwezi kuyataja yote hapa.
NINI KITATOKEA ENDAPO WAARABU WATAKAA NA KUTUOMBA TUSITUMIE MANENO YAO ?,KISWAHILI KITAKUFA?.

Zaidi ya theluthi mbili kama si zaidi ya tatu, usijidanganye kuwa Kiarabu ni theluthi moja au zaidi ya moja. Hayo niliyokuwekea rangi kwa uchache, yote yanatokana na kiarabu.
 
Si zaidi ya 25% ya Kiswahili ni Kiarabu.
INGEKUA 60% YA KISWAHILI NI KIARABU KAMA BAADHI WANAVYODAI BASI WAARABU WASINGEKUA NA HAJA YA KUWA WAKALIMANI KUELEWA KISWAHILI. NA WATANZANIA WASINGEKUA NA HAJA YA MKALIMANI AU KUJIFUNZA KIARABU MAANA WANGEELEWA BILA SHIDA.

NILIWAHI KWENDA UARABUNI, NIKAWA SISIKII CHOCHOTE PUNDE WANAPOANZA KUZUNGUMZA KIARABU. NDIO UNAWEZA BAHATISHA NENO MOJA KATIKA SENTENSI NZIMA LAKINI HII HAIKUWEZESHI KUELEWA SENTENSI ILIKUA INA MAANA GANI.

In red, all derived from Arabic.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom