Wastaafu, tatizo lenu sio kikokotoo bali mishahara yenu midogo

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,347
12,682
Wastaafu wanailalamikia kikokotoo Cha mafao yao ya kusataafu wakituhumu kikokotoo kinawapa hela ndogo ya mkupuo. Ukweli kikokotoo Kiko sahihi ila shida yetu kubwa ni mishahara midogo sana inayozalisha makato ya mafao ya hifadhi ya jamii.

Mishahara yetu ni midogo sana kuliko ya nchi nyingi za dunia na Afrika. Tanzania hakuna mishahara Bali tunalipana posho TU.

Kila kitu siasa, kila kitu woga wa kudai maslahi yenu kwa kuogopa siasa.

Kima Cha chini kilipaswa kuwa TZS 3,000,000 kutokana na kupanda kwa dola na maisha. Kule Marekani malipo ya mfanyakazi wa chini ni USD 10 kila saa ya kufanya kazi. Mishahara Mikubwa itazaa makato makubwa ya kwenye mfuko wa hifadhi, hivyo wakati wa kusataafu kama utapewa 33% ya kiasi kilichoko kingekuwa kikubwa sana.

Daini mishahara Mikubwa sio kikokotoo.
 
Sasa mkuu kavulata, Serikali imeleta kikokotoo kwasababu wamekausha hela za mifuko ya hifadhi na leo mama kakimbia uwanja na kakwepa kuongeza mishahara.. Hiyo nyongeza wataitoa wapi ya kuwapa?

Upande wa pili Serikali ikalazimisha kweli, italeta mfumuko wa bei.. milioni 3 wakapewa punde thamani yake inageuka laki tano ya sasa..
 
Hizi porojo watanzania wengi mmeaminishwa na mnaziamini. Nani alikuambia nyongeza ya mishahara ya watumishi wa serikali huleta mfumko wa bei? Unajua idadi ya wafanyakazi wa serikali nchi hii kuwa hawazidi milioni 2?

Ukisoma kwenye uchumi kuna factors zinazopelekea mfumko wa bei, nyongeza ya mishahara wala haimo.
 
Labda wadai vyote viwili,
 
Hoja ni nzuri ila shida ni kwamba nchi haina mapato ya kulipa kima hicho cha chini watumishi wake wote
 
Hizi porojo watanzania wengi mmeaminishwa na mnaziamini. Nani alikuambia nyongeza ya mishahara ya watumishi wa serikali huleta mfumko wa bei? Unajua idadi ya wafanyakazi wa serikali nchi hii kuwa hawazidi milioni 2?

Ukisoma kwenye uchumi kuna factors zinazopelekea mfumko wa bei, nyongeza ya mishahara wala haimo.
Kuongeza pesa kwenye mzunguko ilhali uchumi hauzalishi sawia na pesa zilizoingizwa inasababisha mfumuko wa bei, mathalani ulikuwa unanunua mchele kilo moja kutokana na mfuko wako, ukiongezewa pesa utanunua kilo mbili kama mkulima hajaweza kuzizalisha utapanda dau kupambana na mwenzako mlioongezewa wote mshahara.

Anaemuuzia mkulima pembejeo atapandisha bei ili aweze kuhimili bei ya mchele iliyopandishwa na mfanyakazi na huu mzunguko mwisho unafikia uchumi mzima.
 
Sasa mkuu kavulata, Serikali imeleta kikokotoo kwasababu wamekausha hela za mifuko ya hifadhi na leo mama kakimbia uwanja na kakwepa kuongeza mishahara.. Hiyo nyongeza wataitoa wapi ya kuwapa?

Upande wa pili Serikali ikalazimisha kweli, italeta mfumuko wa bei.. milioni 3 wakapewa punde thamani yake inageuka laki tano ya sasa..
Mishahara hii inazalisha watumishi wala rushwa, wezi wa mali na muda wa mwajili na watu wasiokuwa na morali ya kufanya kazi. Serikali inafahamu kuwa watumishi wote wanaiba mali na muda kama mbinu ya kujiongezea muda, yaani iba lakini usikamatwe wala kulalamikiwa(Iba na kuchukua kwa uangalifu)- kula usawa wa kamba yako usizidishe.

Duniani kote kikokotoo ndio hikihiki ila mishahara (denominator) ni Mikubwa, hivyo wanaipata hela nyingi na pension kubwa. Wasomi wetu hawawezi kudai maslahi Yao.
 
Hata mshahara uwe mkubwa vipi? Lakini kupewa 33% wakati unaaa 67% upewe kidogokidogo bado haijakaa vizuri. Wafanye viceversa watoe 67% kwa mkupuo the rest watoe kidogokidogo
Mishahara Mikubwa itakupa fedha nyingi za mkupuo na na fedha nyingi za kila mwezi. Kima Cha chini ni sh. 370,000 sawa na US dollars 147 TU. Professor analipwa mishahara wa sh.4,000,000 sawa na US dollars 1,600 TU kwa mwezi. Mshahara wa Prof wetu hapa ni sawa na mshahara wa mzibua mitaro ya maji taka kwa nchi nyingine. Hata kikokotoo kikiwa 50% bado tabu kwako itakuwa palepale.
 
Back
Top Bottom