TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,544
- 11,294
Wanajamii kuna habari nimeisoma kuhusu msimamo wa vyuo vikuu dhidi ya waraka waziri Maghembe kuwataka watumie vyeo vya mwenyekiti badala ya rais wa serikali ya wanafunzi na pia juu ya kufutwa kwa serikali za wanafunzi n.k
Kauli yao waliyoitoa juu ya waraka huo ni ya kumtaka waziri aachane na mambo hayo vinginevyo watapambana naye na hata ikibidi wataendesha kampeni dhidi yake kwenye jimbo lake la uchaguzi.
Hoja yangu siyo kujadili upande upi uko sahihi bali kutokana na msimamo wa wasomi hawa nimeshawishika kuamini kuwa tatizo la uongozi mbovu nchi yetu mara nyingine linasababishwa na ubinafsi tulionao watanzania hasa wasomi. Ni mara nyingi sana viongozi wetu wanatoa kauli au kufanya maamuzi ambayo hayana tija kwa jamii lakini sijawahi kusikia kauli ya hawa viongozi wa vyuo. Mpaka maslahi yao yanapoguswa ndiyo wanaibuka na kutaka kuishirikisha jamii.
Nadhani ni wakati sasa kwa wasomi wetu nao angalau kutoa misimamo yao pale wanapoona mambo yanafanyika ndivyo sivyo serikalini. Hii itasaidia angalau kuamsha mori ya wazalendo wengine kwa manufaa ya jamii ya watanzania wote.
Nawasilisha.