Wasomi wanahujumu uchumi.

May 19, 2011
62
5
Napata wakati Mgumu sana,nimeshuhudia wanaharakati wengi sana Wakitoka chuoni na mwisho wa siku wanageuka wanamikakati. Ukiwauliza JIBU 'ofisi zimeharibika' nabaki kuamini kumbe wanaharakati ni wanapo banwa ukipata upenyo wa pesa unageuka mwanamikakati.
Sitaki kumezwa na hii fikra chakavu nataka nibaki nikiamini kuwa mwanaharakati ni kwa ajili ya mabadiliko na ni popote.

Kilio changu ni kwa wasomi wetu, kiukweli kwa sasa kila sehemu ni mbovu, kila huduma imeoza, watu maofisini hawafanyi kazi ipasavyo, kwa ufupi nchi inaenda tuu yenyewe hakuna anayeweza sema baada ya mwaka tutakuwa wapi, ila tutakuwa pale nchi itakapo elekea.

WASOMI wamejawa uroho wa madaraka na FEDHA
,chuoni hakuna wanachowaza zaidi ya MAGARI,NYUMBA na PESA nyingi ,..wachache sana wanawaza maendeleo na mambo ya msingi,..Wengi tunawaza KUIFILISI serikali.

HILI kwangu LINABAKI CHANGAMOTO.WASOMI tubadilike mtu mmoja anaweza kubadili kila kitu ndani ya ofisi WEWE chapa kazi acha wengine waibe lakini wewe simamia HAKI, WAJIBU na UTARATIBU.

Hizi ndio baraka za MWENYEZI Mungu na atakusaidia katika mapambano ya nchi hii kwenda nchi ya AHADI. SITAKI RUSHWA NA SITACHUKUA RUSHWA, sioni sababu ya kuwa na fedha za dhuluma.

NAHITAJI KUONA SURA YA MUNGU, twende kwa staili ya mabadiliko ya mmoja mmoja kwa moyo wa DHATI, mwishowe TANZANIA ITABADILIKA.
 
Wasomi..wasomi...wasomi na nchi hii!!wasomi aina ya akina Chenge..Prf Maghembe...Malchera,wasomi wetu bwana,wana dozi za kozi kibao,ni wataalamu wa kuandika proposal...wasomi vijana,akina Nepi,Ridhiwani,Nyangwine!!
 
Back
Top Bottom