Wasipoifuta kuna hatari kwa Preventive Detention Act kutumika dhidi ya viongozi hawa wa CCM

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wadau:

Kila mara huwa najiuliza: Kwa nini ile sheria ya kuwaweka watu kizuizini bila ya kufunguliwa mashitaka (Preventive Detention Act) bado ipo hadi leo hii?

Hiyo sheria kandamizi haijaondolewa na tangu ujio wa siasa za vyama vingi haijawahi kutumiwa na kiongozi yoyote wa nchi. Kwa maneno mengine sheria hiyo ipo kisheria lakini siyo halali.

Hivi hawa viongozi wa serikali ya CCM wa sasa hivi hawaoni umuhimu wa kuiondoa? Hawaoni kwamba inaweza kuwarudia wao wenyewe.

Nasema hivi kwa sababu hatujui Mwenyezi Mungu ameipangia Tanzania yetu hii kitu gani – katika miaka ijayo huwezi kujua katupangia nini.

Siombei machafuko, lakini kwa madudu viongozi wa CCM wanayowafanyia Watanzania, wanaweza kujikuta wametupwa nje ya uongozi-kama ilivyotokea katika nchi nyingi tu Barani humu, na sikioni kitu chochote kinachoweza kuniridhisha kuwa nchi hii ni ya kipekee yaani unique.

Madudu yanayofanywa na viongozi wetu ni yaleyale waliyokuwa wakiyafanya hao wengine kwa wananchi wao na kujikuta wako nje.

Sasa wapinzani wakishika nchi wanaweza kupata urahisi mkubwa wa kuwashughulikia mafisadi hawa wa CCM walioko katika uongozi sasa kwa sababu sheria hiyo haitahitaji ushahidi thabiti wa ufisadi hao. Serikali mpya inaweza kuwasweka ndani wakaozea huko, na ikawa haijavunja sheria wala Katiba.

Ikitokea hivyo, hivi wafuasi wa CCM (yaani wapinzani) kweli watapata nguvu ya kuilalamikia serikali hiyo mpya?

CCM lazima itumie akili. Kuna kila dalili sheria hii inaweza kuwarudia wao.

Nawasilisha.

Mkuu Zak, kwa nini unawaamsha awalio lala? hasa kama ni mafisadi? We acha tu wabanwe na sheria yao wenyewe, na hapo ndipo patakuwa patamu!
 
Hawa CCM wanajiamini sana! Hawajui la kesho. Wimbo wao huu 'Amani na utulivu" unaanza kuwa kichekesho kutokana na madudu wanayofanya. After all amani haiimbwi kwenye majukwaa, bali hujengwa kwa misingi madhubuti ya haki.
 
Ayaaaa mbona unawashitua wewe? Huoni unaharibu ukichukulia kuwa hiyo sheria haijatumika muda mrefu?!
 
http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/2-1985.pdf

Hapo utapata amendment yake ya 1985. Naona wanaruhusu ku-challenge detention order in court. Na mahakama za sasa ivi haziwezi kuruhusu detention orders zisizokuwa na evidence.
Tatizo hapa ni evidence. The crime committed by the mafisadi ni ngumu ku-pin down kwa mtu mmoja. Sio sawa na wizi wa kuku. Watu wametengeneza shell companies, nk kujificha nyuma yake. Hizi kesi zitakuwa ndefu. Sio rahisi kama mnavyodhani.
http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/2-1985.pdf
 
Zak kwa historia yote ilipo dunia mwisho wa sheria mbovu uishia kwa waliyoitunga, huo ndio ukweli na unachokisema ndiyo historia ya udhalimu maana wanaotunga sheria mbovu ujishau wakidhani kuwa wao watakuwa madarakani milele, bila kujuwa kuwa siku wakitoka hiyo hiyo sheria mbovu itawachapa.

Wadau:

Kila mara huwa najiuliza: Kwa nini ile sheria ya kuwaweka watu kizuizini bila ya kufunguliwa mashitaka (Preventive Detention Act) bado ipo hadi leo hii?

Hiyo sheria kandamizi haijaondolewa na tangu ujio wa siasa za vyama vingi haijawahi kutumiwa na kiongozi yoyote wa nchi. Kwa maneno mengine sheria hiyo ipo kisheria lakini siyo halali.

Hivi hawa viongozi wa serikali ya CCM wa sasa hivi hawaoni umuhimu wa kuiondoa? Hawaoni kwamba inaweza kuwarudia wao wenyewe.

Nasema hivi kwa sababu hatujui Mwenyezi Mungu ameipangia Tanzania yetu hii kitu gani – katika miaka ijayo huwezi kujua katupangia nini.

Siombei machafuko, lakini kwa madudu viongozi wa CCM wanayowafanyia Watanzania, wanaweza kujikuta wametupwa nje ya uongozi—kama ilivyotokea katika nchi nyingi tu Barani humu, na sikioni kitu chochote kinachoweza kuniridhisha kuwa nchi hii ni ya kipekee yaani unique.

Madudu yanayofanywa na viongozi wetu ni yaleyale waliyokuwa wakiyafanya hao wengine kwa wananchi wao na kujikuta wako nje.

Sasa wapinzani wakishika nchi wanaweza kupata urahisi mkubwa wa kuwashughulikia mafisadi hawa wa CCM walioko katika uongozi sasa kwa sababu sheria hiyo haitahitaji ushahidi thabiti wa ufisadi hao. Serikali mpya inaweza kuwasweka ndani wakaozea huko, na ikawa haijavunja sheria wala Katiba.

Ikitokea hivyo, hivi wafuasi wa CCM (yaani wapinzani) kweli watapata nguvu ya kuilalamikia serikali hiyo mpya?

CCM lazima itumie akili. Kuna kila dalili sheria hii inaweza kuwarudia wao.

Nawasilisha.

Huwezi kujiapiza kuwa nikikatwa patachimbika, wewe nani? Ngoja ukome nyau wewe.
 
Back
Top Bottom