tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,859
- 18,277
Sakata la mchele wenye virutubisho kutoka Marekani limeendelea kuchukua sura mpya baada ya waislamu kuukataa bila kumumunya maneno. Wakiongea kupitia redio ya kiislamu ya Imaan FM inayounguruma kutokea mkoa wa Morogoro, wamesema hawautaki mchele huo na wametoa tahadhari kwa mtu yeyote atakayewalisha watoto wao. Wamesema chakula wanacho cha kutosha hapa nchini na kushauri waletewe vitu wasivyokuwa navyo kama vile ndege, magari na ambulance.
Ili kuonyesha kuwa hawatanii katika hili, hata watangazaji waliokuwa wakiendesha kipindi walionekana kushabikia kitendo hicho. Mtu yeyote aliyepiga simu kwenye kipindi akionyesha kwenda kinyume na msimamo wao, walimkatia simu mara moja. Hebu wasikilize wewe mwenyewe kupitia klipu hiyo hapo chini.
MAONI YANGU
Huu mchele sasa naona umeanza kutugawa kiitikadi. Wakristo nao wakitoka hadharani na kuweka msimamo wao, hapatatosha. Ifike mahali ubaguzi wa kijinga kama huu ukemewe kwani unaweza kuligawa taifa na kuhatarisha umoja na mshikamano tulio nao hapa nchini. Tusiruhusu kikundi kidogo cha watu kitugawe kwa sababu yoyote ile.
Nawasilisha.