Washtakiwa watano mauaji ya bilionea Msuya wahukumiwa na Mahakama Kuu adhabu ya kunyongwa hadi kufa

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,101
Washitakiwa watano katika kesi ya kumuua kwa kukusudia mfanyabiashara wa madini, bilionea Erasto Msuya wamehukumiwa na Mahakama Kuu adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

=====

WhatsApp Image 2018-07-23 at 11.25.03.jpeg


Mahakama Kuu ya Tanzania imewahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa watano baada ya kuwatia hatiani kwa kumuua kwa makusudi mfanyabiashara wa Arusha na Mirerani, Erasto Msuya.

Waliohukumiwa adhabu hiyo ni mshitakiwa wa kwanza, Sharifu Mohamed; mshitakiwa wa tatu, Mussa Mangu; wa tano, Karim Kuhundwa; wa sita Sadick Mohamed na wa saba; Ally Mussa Majeshi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Julai 23, 2018 na Jaji Salma Maghimbi aliyesikiliza kesi hiyo.

Pia, Mahakama imemwachia huru mshitakiwa wa pili, Shwaibu Jumanne baada ya kukosekana ushahidi dhidi yake.

Chanzo: Mwananchi

----

Pia soma

VIDEO: Mauaji ya Erasto Msuya, Aneth Msuya na hukumu ya Miriam Mrita

Soma Sakata la Kifo cha Bilionea Msuya


MWENENDO WA KESI MAUAJI YA BILIONEA ERASTO MSUYA

Septemba 17, 2013 watuhumiwa wakiwa kwa mganga wakijizindika wasikamatwe

Soma Waliomua Bilionea Erasto Msuya wakutwa kwa sangoma

Juni 12, 2014, Mahakama yaelezwa jinsi Erasto Msuya alivyouawa
Soma Mahakama yaelezwa bilionea wa madini Erasto Msuya alivyouawa

Oktoba 27, 2017, Shahidi adai kuahidiwa Tsh 17m kutekeleza mauaji
Soma Shahidi aelezea walivyoahidiwa kulipwa Sh 17 milioni kila mmoja kumuua bilionea Msuya

Mei 11, 2018, Shahidi alidai kuwa Mfanyabiasha wa Madini, Chusa ndiye alipanga mauaji
Soma SHAHIDI: Chusa alipanga mauaji ya Bilionea Msuya

Mei 14, 2018 Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu washtakiwa 6
- Kesi ya bilionea Msuya: Sita wana kesi ya kujibu huku mmoja akiachiwa huru

Julai 23, 2018 washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa
soma Washtakiwa watano mauaji ya bilionea Msuya wahukumiwa na Mahakama Kuu adhabu ya kunyongwa hadi kufa

Agosti 18, 2018 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa wakata rufani
Soma Waliohukumiwa kwa mauaji ya Bilionea Msuya wapinga kunyongwa

Jaji aliyetoa hukumu atishiwa kifo
Soma Jaji aliyesikiliza kesi ya mauaji ya Bilionea Msuya na kutoa hukumu ya kifo atishiwa kuuawa

Pia soma Aliyeachiwa kesi ya mauaji ya Bilionea Msuya aeleza mazito


MAUJI YA ANETH MSUYA NA MWENENDO WA KESI YA MAUAJI YAKE

Aneth Msuya aliuawa kinyama akiwa nyumbani kwake Kibada
Soma Aneth Msuya ambaye ni dada wa bilionea Erasto Msuya auawa kinyama Dar

AUG 23, 2016 Mirima Mrita alipandishwa kizimbani kwa tuhuma za mauji ya Aneth Msuya
Soma Mjane wa Erasto Msuya apandishwa Kizimbani Kisutu

SEPT 18, 2023 Mahakama ilimkuta Miriam Mrita na kesi ya kujibu Mauji ya Aneth Msuya
Soma Dar: Mke wa Bilionea Msuya akutwa na Kesi ya Kujibu mauaji ya wifi yake

FEB 23, 2024 Mahakama Kuu ilimuachia huru Miriam Mrita
Soma Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia mauaji ya Aneth Msuya


UGOMVI WA MALI ZILIZOACHA NA ERASTO MSUYA
Familia ilishindwa kuelewana suala la mirathi na kupelekea Serikali kuingilia kati
Soma Mali za Marehemu Bilionea Erasto Msuya, ndugu ngumi mkononi

Mama Mzazi wa Erasto Msuya adai kuwa mjane alikomba mali kabla ya mazishi
Soma Mama wa Bilionea Msuya: Mke alikomba mali kabla ya kumzika mwanangu

Wadau wahoji uhalali wa ndugu wa Miriam Mrita kusimamia mali za Erasto Msuya
Soma Mama wa Bilionea Msuya: Mke alikomba mali kabla ya kumzika mwanangu

Mama Mzazi wa Msuya akubali kuondoa shauri Mahakamani ili kulimaliza kifamilia
soma Mama wa Bilionea Msuya akubali kuondoa kesi kwa Muda Mahakamani

Mahakama yataka pande mbili za familia kukaa meza moja na kuondoa tofauti
Soma Ugomvi wa Mali za Marehemu Bilionea Msuya, Mahakama yanena

2021, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumuondoa Miriam Mrita kuwa msimamizi wa Mali
Soma Mahakama yamuengua mjane wa Bilionea Erasto Msuya kusimamia Mirathi ya Mumewe
 
safi kabisa, kwani Hukumu imeonesha ni kweli walihusika
na ni kwa ajili ya tamaa na wivu
hata km watafia jela wazikwe hukohuko
Mleta mada bado yupo katika chumba cha mahakama kuu simu haziruhusiwi
na najua Hukumu ni ndefu mpaka saa hizi bado inasomwa
yeye mwandishi katuletea Hint tu Hongera sana Papaa Mobimba
 
pole mno kwa ndugu wa marehemu Msuya ninategemea mmepata closure kuhusiana na kifo cha mpendwa wenu na maisha kidogo kidogo yataanza kurudia yalivyokuwa;adhabu waliyopewa haina maana kwenu maana haitarejesha uhai wa mpendwa wenu,adhabu iliyotolewa haimaanishi mlikuwa mnahitaji revenge kwa wahusika ila mlitaka kupata ukweli ilikuwaje na why walimuua mpendwa wenu;hii death sentence ni adhabu ya kinyama na kikatili mno na watu wengi hasa karne hii wanaipiga vita maana sasa tutakuwa tumepoteza watu 6(including waliyemuua)je haya ndio tunayoyataka yatokee?wakati umefika kwa adhabu hii ya kinyama kuondolewa kwenye vitabu vyetu vya sheria
 
Hiyo ni hukumu tu kuna nafasi ya kukata rufaa pia na hata rufaa ikishindikana hawanyongwi leo au kesho
Hilo ni sahihi! Nilishuhudia kesi moja jamaa alihukumiwa kunyongwa lakn baada ya rufaa kusikilizwa ikaja manslaughter na akahukumiwa miaka minne jela...
Jamaa aliposomewa tu akatulia kimyaa kama dk 3 kwenye kizimba kumbe alikuwa haamini akarudia tena kumuuliza wakili wake alipoambiwa minne jamaa alipiga magoti akalia Sana kwa furaha
 
Hebu tukumbushane ile orodha ya wahukumiwa. Maana Tetesi zilipita sana kuwa mke alihusika. Ila mke akakamatwa kwa ile ya mauaji ya dada yake msuya marehemu Anet Msuya kama sikosei. Hivyo vifo viwili vina walakini mkubwa mno maana pia Annet alikuwa mstari wa mbele kuratibu hii kesi ya mauaji ya kaka yake. Hatimaye naye akauawa kinyama sana huko makazi yake Kigamboni.
 
Back
Top Bottom