Washirika wenzangu wa Shindano la Stories of Change 2023 mnafuata vigezo vilivyowekwa kweli? Milioni 20 sio mchezo ujue!

Black Opal

Senior Member
Jan 22, 2023
199
253
vigezo.jpg

Kama tunavyojua mchongo ushaanza na nimeona kuna milioni 20 za kubeba. Watu tunaotaka kuchota hizi milioni 20 tunafata vigezo kweli au mnafikiri ni kazi rahisi kuzipata?

Mtu unaandika tu ovyo ovyo kama uropoka, vigezo hufati halafu unajiwekea asilimia za kushinda!

Kuna baadhi ya Vigezo na Mashari hatufati ambavyo nimeona vitatukosti sana sisi tunaotaka kunyakuwa hizo Milioni 20:

Kigezo cha idadi ya maneno
Katika vitu naona itakula vichwa ni kigezo hiki 🤣 🤣. We unaambiwa andika maneno kati ya 700 hadi 1000 unaandika maneno 1050, au maneno 400, mwingine anajikuta kukamia anaandika maneno 2000+🤣🤣. Mpo humu mnaojikuta Mataikoni wa kuandika, nyie mjue hii milioni 20 haiwahusu, mmetuachia.

Kwa kuwasiadia, kama unaandika moja kwa moja hapa jukwaani, kopi uzi wako na uuweke kwenye Microsoft Word pale itakuonesha idadi ya maneno kwa chini kushoto hivyo utajua kama umezidisha maneno au la.

Idadi ya maneno kwenye kichwa cha habari
Hapa kigezo kimekwambia kweupeee, kwamba kichwa cha andiko lako kisipungue maneno manne, jitu linakwenda kuandika maneno matatu au mawili, wewe jua ushajiondoa kwenye shindano. Kama umeacha likichwa lako hivyo peleka ujumbe kwa Mods mapema ubadilishe.

Kuna hili kundi maalum😂😂 kichwa chao cha habari kinakuwa Stories of Change, au Utawala Bora au Uwajibikaji kwenye nyanja mbalimbali
Bwana bwana, hawa wanafosi maneno haya yaonekane kwenye kichwa cha habari na kwenye maandiko yao wakati wanaongea pumba na cha maana ni hayo maneno. Embu kuwa serioua bwana. Milioni 20 sio mchezo, we unafikiri utaipata kirahisi hivi?

Una njia nyingi za kufanya usifosi kuweka maneno hayo kwenye kichwa cha habari au kuyataja maneno hayo mara kwa mara, sema moja moja unavyotaka mtu/sekta fulani iwajibike, sema vile unavyoona utawala bora uko vipi badala ya kutaja tu Utawala Bora halafu maudhui sifuri. Kwa kufanya hivi andiko lako litaeleka vizuri tu na hutaonekana hujui unachofanya.

Wanaodhani Utawala Bora au Uwajibikaji unalenga Siasa pekee🤔
Jamani, yaani unakuta mtu mchovu kwenye Siasa lakini anang'ang'ana aandikie Siasa kwakuwa amezoea kusikia Uwajibikaji na Utawala bora kwenye Siasa.

Hivi unajua unaweza kuongelea chochote kwenye jamii yako kuchochea Utawala Bora au Uwajibikaji? Watu hapa mnafanya kazi maeneo mbalimbali, inaweza kuwa kwenye sekta ya afya, burudani au hata urembo, usiniambie hapo ulipo kila kitu kipo sawa 100% na usingependa mambo yaboreshwe hata kidogo? Usiniambie hapo ulipo watu wanawajibika na majukumu yao kwa kiwako cha kuridhisha kiasi kwamba huoni sehemu ya kuboresha kufanya watu wawajibike zaidi na kuchangia kuwa na utawala bora unaomfaidisha kila mtu.

Watu mna malalamiko kibao kibao kwenye sekta ya afya, elimu, wastaafu, jeshini, burudani (tuzo za mziki zimetoka juzi tu hapo malalamiko kibao) malalamiko kwenye sekta ya ulimbwende (urembo) yapo kibaooo kweli unakosa kitu cha kuongelea kuchochea mabadiliko na kupendekeza mambo yawe bora? Wewe Mwalimu, Mwanajeshi, Daktari, Mwanafunzi, Mwanamuziki, Mchoraji, Mstaafu, Mama ntilie, Machinga, Bodaboda, nk, huna lolote la kusema kuhusu Uwajibikaji au Utawala wa sekta hiyo uliyopo? Umeridhika kabisa na kila kitu na hakuna pa kuboresha? Em kuwa serious bwana, lete nondo hizo.

Nadhani sasa mmepata mwanga na hii mada haitaonekana ngumu tena na watu wataacha kung'ang'ania mambo ya siasa ambayo hata hawayawezi. Kila mtu ataleta nondo zake kutoka sehemu aliyopo zinazooneaha kweli watu wanajua wanaongelea nini, hata mtu kukupigia kura asione mzigo au anakupigia kura sababu umemtumia ujumbe PM.

Mwisho ni hawa wenzangu na mimi ambao, pamoja na Vigezo na Masharti kuwepo hatasoma chochote, yaani ni kama vile yeye 'stafu' mwezenu. Si mnawajua hawa stafu wakiingia kwenye madaladala wanakuwa hawalipi nauli? Sasa hawa wanajikuta kama stafu wa stories of change🤣🤣🤣. Nyie ndugu zangu tunawaombea tu Mungu awarehemu🤣🤣🤣 kwani hili shindano haliwahusu.

Ndugu zangu ni katika kukumbushana tu, kama unataka kupata Milioni 20 kama mimi basi lazima ujipinde utoe kitu ambacho watu wakisoma wanaona yes umeleta nondo kweli. Na uzuri ni kwamba ukileta nondo yaani haiwezi kujificha, utaonekana tu.

Nawatakia ushandani mwema, mwenye kisu na atoboe. Kwenu Wakuu.
 

Attachments

  • vigezo.jpg
    vigezo.jpg
    38.6 KB · Views: 22
Wakumbushe pia wasiumize kichwa sana na kuumia Kwa pesa wanayo tarajia kuipata wakishinda,

Wasiwe kama wale wa kubeti shilingi mia (100) na kuanza kutukana hovyo baada ya yale matarajio ya kupata million moja (1000000) kufeli.

Lastly; Any one can get anything but not everything.
 
Umeshidwa kutambua kuwa hiyo 20ml ni kwa washindi wote na sio wa 1st

Umeshafeli tayari ilo shindano tuachie sisi
Acha kukurupuka, soma uelewe. Wapi nimesema Milioni 20 ni ya mtu mmoja pekee? Ndio nyinyi msiotuliza fuvu kusoma na kuelewa vigezo afu mnakuja kulialia huku mmefanyiwa hujuma
 
Lengo la hiyo kitu kwanza sio kupata hela, ni kuonesha njia ya mabadiliko wengine waipitie, kama njia yako ikiwa nzuri zaidi basi utapata hiyo unayosema kama zawadi kwa mchango wako, kuanzia mwanzo usiifanye kwa lengo la kupata hela
 
Lengo la hiyo kitu kwanza sio kupata hela, ni kuonesha njia ya mabadiliko wengine waipitie, kama njia yako ikiwa nzuri zaidi basi utapata hiyo unayosema kama zawadi kwa mchango wako, kuanzia mwanzo usiifanye kwa lengo la kupata hela
Una point hapa Mkuu, ila si vibaya kufikiria motivation ya mahela hayo
 
Aisee kwann huu Uzi usipewe tu hizo milion 20
Umeua Sana bablai na Mimi ntajaribu bahati yangu umeni inspire
Safi sana Mkuu, fanya hivyo...milioni 20 nyingi unaweza kubahatisha kunyakua za mshindi wa kwanza😁😁😁
 
Back
Top Bottom